Wahariri wa Vyombo vya Habari mmetuangusha sana

Paf

JF-Expert Member
May 25, 2021
1,703
3,304
Hongereni kukutana na Mhe. Rais. Hongereni kupata vinywaji Ikulu.

Hakika hamkujipanga,mlitakiwa wahariri mkutane kwanza muandae maswali Magumu na mazuri na mngegawana maswali na majina mngempa MC kwaniaba ya wahariri.

Mhariri umetoka mkoani unamuuliza Rais anauonaje Urais (mwandishi kweli) hujui neno Urais. Alisema Bunge halina afya. Alisema kesi zenye ukakasi zifutwe. Mnashindwa kuhoji miradi ambayo haikupita bungeni.

Mmeshindwa kuhoji serikali kulipa wabunge hewa,wakati uchaguzi ulikuwa wa ushindi wa 80%. Mnashindwa kuhoji bandari 3 zilizopo nakukimbilia ya Bagamoyo.

Mnashindwa kuhoji miaka 60 watoto hawana madawati, upungufu wa walimu, wauguzi, madaktari nk. Mnauliza Urais ukoje wakati ndege inapashwa kila mda ili imrushe Rais popote

Mmetuangusha sana.
 
Kwa akili zako hao waliomo humo wameenda tu bila kupangwa


Hmn ufala kama huo na hioo haijirudii tena.
 
Katika michezo kuna kitu kinaitwa "home court advantage" kwa muktadha huo serikali walikuwa wapo uwanja wa nyumbani. Kwa hiyo basi wanahabari walijikuta wakicheza mchezo huu wa ugenini kwa uoga kwa kutambua nguvu, madaraka na mamlaka ya yule aliyewaalika
 
Sijafuatilia kilichoendelea, mi Sina habari, niko busy katika kujinasua kwenye dimbwi zito la umasikini, serikali yangu haina msaada wa moja kwa moja na mimi so acha wafanye yao mi nifanye yangu.
 
Back
Top Bottom