Wahadhiri waeneza siasa za chuki vyuoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wahadhiri waeneza siasa za chuki vyuoni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by engmtolera, Mar 24, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  SERIKALI inawachunguza wahadhiri wa vyuo vikuu nchini wanaotumia muda mrefu madarasani kuzungumzia siasa badala ya kufanya kazi zinazohusu taaluma.

  Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, Serikali ina taarifa kuwa, baadhi ya wahadhiri wanatumia muda wa kutoa mihadhara ya masomo kwa kuzungumzia siasa hasa kupiga vita Serikali iliyopo madarakani.


  "Tunaendelea na uchunguzi wa kuwabaini baadhi ya wahadhiri wanaojihusisha na siasa kwa kuingia madarasani na kuzungumzia siasa kwa dakika kumi kabla ya kuanza kufundisha," amesema Mulugo.


  Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo, lengo la wahadhiri hao ni kuwafanya wanafunzi kuchochea migomo na maandamano na kupandikiza chuki baina ya Serikali na wanafunzi.


  Naibu Waziri ameyasema hayo katika mkutano kati ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili (Muhas), Dar es Salaam.


  Mulugo amesema, ingawa si katika chuo hicho, lakini kuna taarifa katika baadhi ya vyuo vikuu, wahadhiri wanafanya hivyo na kuwaonya kuwa kazi yao ni kuelimisha na si kuwavuruga wanafunzi akili kwa kuchanganya yale wanaojifunza na siasa na akawataka kujiepusha na siasa kwa kuwa wao ni wataalamu.


  "Tena siasa zenyewe ni za kupiga vita Serikali iliyopo madarakani, tutawachukulia hatua," alisisitiza.


  Kauli hiyo iliungwa mkono na Waziri Kawambwa ambaye aliongeza kuwa wahadhiri wasipojihusisha katika siasa, watasaidia kuweka utulivu katika vyuo na kuepusha migogoro.


  Awali, kabla ya onyo hilo, Dk. Kawambwa alisema Baraza la Mawaziri limeazimia kuanzia Machi mwaka huu wahadhiri wastaafu walipwe pensheni sawa na wastaafu wengine serikalini.


  Alifafanua kwamba uamuzi huo unatokana na malalamiko ya wahadhiri wastaafu kwamba wanapata mafao finyu kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF tofauti na wanaostaafu kutoka Serikali Kuu ambao hupata mafao yenye neema kutoka Mfuko wa Pensheni ya Wafanyakazi wa Serikali Kuu (GSPF).


  Mbali na Dk. Kawambwa, pia Rais Jakaya Kikwete katika shughuli tofauti ya kuzindua Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) jana, aligusia malalamiko ya wafanyakazi wote kuhusu tofauti kubwa ya sana katika utoaji wa mafao ya mkupuo na pensheni ya uzeeni.


  "Utakuta wafanyakazi wenye viwango sawa vya mshahara, muda sawa wa utumishi wanapostaafu, mmoja anapata hadi mara tatu zaidi ya mwenzake aliye mfuko mwingine," alisema Rais Kikwete.


  Kutokana na tofauti hiyo aliyosema imelalamikiwa na vyama vingi vya wafanyakazi, Rais Kikwete aliagiza SSRA iangalie tofauti hiyo kwa makini na kuhakikisha kunakuwa na uwiano sawa wa mafao kati ya mfuko na mfuko, lakini akawataka pia wazingatie ustawi wa mfuko huo.


  Lakini kuhusu maombi ya wahadhiri wa Muhas, kutaka kulipwa mafao kwa mkupuo kwa asilimia 50 ya mafao yao na kulipwa kwa miaka 15 baada ya kupokea mafao ya mkupuo, Dk. Kawambwa alisema bado yanafanyiwa kazi.


  Kati hilo, Dk. Kawambwa alibainisha wataalamu wanaangalia suala la malipo hayo kwa kuwa limeonekana na utata unaoweza kusababisha baadhi ya mifuko kufa iwapo itapata wastaafu wengi hivyo unaangaliwa mfumo utakaotumiwa na mifuko yote.


  Akizungumzia madai ya wahadhiri wa chuo hicho kuhusu posho ya nyumba ambazo hawajalipwa kuanzia mwaka jana, alisema hali hiyo ilitokana na ufinyu wa bajeti, lakini tayari wamepeleka malalamiko yao kwa Wizara ya Fedha ili walipwe katika bajeti ijayo.


  Kabla ya kauli hizo za mawaziri, Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Kisali Pallangyo alielezea changamoto anazopata ikiwemo ya miundombinu michache ya chuo hicho.


  Kutokana na uhaba huo wa miundombinu, kati ya wanafunzi wanne wanaostahili kujiunga na chuo hicho, ni mmoja tu anayepata nafasi wakati Taifa linakabiliwa na uhaba mkubwa wa wataalamu wa afya.


  Dk. Kawambwa akijibu hoja hiyo, alisema, katika kuongeza wataalamu hasa katika masomo ya sayansi, Serikali imejipanga katika mpango wa maendeleo ya elimu ya juu kuboresha miundombinu ya vyuo hivyo ili wanafunzi wote wenye sifa wajiunge na vyuo stahili.


  Chanzo: HabariLeo
   
 2. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Sasa hapo ni vyuoni tu, ktk shule za sekondari hasa za kata walimu wanaongelea sana siasa na kuiponda serikali kwa wanafunzi na hii ni kwa sababu ya maslahi duni ya walimu.

  Wameamua kuwaharibia, yaani serikali ya CCM mna kazi mnashambuliwa kila kona mtasalimika kweli?
   
 3. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Vyuo vikuu ni chemchem ya mabadiliko wanafunzi hao wanapaswa kufahamu kwa undani namna serikali inavyoteleleza majukumu yake na namna pesa za umma zinavyotumika na kwa maslahi ya nani.

  Vyuo vikuu wanafundishwa watu wa kada mbalimbali hivyo ni vema wakaelewa mapungufu na mazuri ya serikali yao.

  Isitoshe kuna masomo vyuo vikuu ambayo yakifundishwa mtu hawezi kukwepa kuzungumzia siasa e.g. Public administration, political science, public resource management, human resource management etc..

  Serikali itimize wajibu wake ipasavyo wala haitasikia harufu ya migomo.
   
 4. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Wanafunzi wa vyuo vikuu siyo watoto, wanaona, wanachambua taarifa na kufanya maamuzi kwa kadri ya uwezo wao.

  Kumjengea mwanafunzi uwezo wa kuona madudu/kufikiri juu ya uzalendo wa nchi yake ni namna moja ya kumuelemisha. Walimu ni jukumu lao kufanya hivyo ila kwa kufuata misingi ya kazi zao na si kuzidi mipaka yao.

  Nikiingia darasani, lenye wanafunzi 200, nikakuta wanafunzi hawajatulia/wanapiga piga kelele na kama hawataki kutulia kuwafanya wanisikilize nitajaribu kuongea kitu chenye mvuto na kuwatuliza kabla ya somo kuanza.
   
 5. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  BIG UP Serikali- CHUNGUZA -CHUNGUZA - CHUNGUZA.

  Jana nilikuta kikundi cha wakulima na pia wamachinga na kinyozi wakijadili kuhusu siasa badala ya kufanya kazi kujiletea maisha bora naomba tuwasiliane ili mtume wachunguzi wakawachunguze.

  Kazi kwelikweli
   
 6. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Waziri hana kazi ya kufanya.

  Nani hapo analalamika, wanavyuo au wanasiasa?

  Kutokuwa na kazi ni kazi pia?
   
 7. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #7
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Waanze na 'Dr' Benson Bana
   
 8. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Serikali ya CCM jamani imeoza na inanuka sana.

  Hapa Tanzania nani mchochezi kati ya wahazili na ccm? Hapa ni CCM ni wanafiki, wazandiki, walafi na wezi sasa unapotoa uovu wao wanaona wewe mchochezi jamani. WAHADHIRI JUU... Kaza buti chochea moto wa uraia kwa wanachuo.

  WE KIONGOZI AU WAZIRI UFUTE HIZO KAULI ZAKO AU UZIPELEKE NYUMBANI KWAKO KWA WATOTO WAKO SIO KWA WATZ.
   
 9. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,980
  Likes Received: 20,372
  Trophy Points: 280
  Nadhani ingekuwa vema kama kina Tambwe Hizza wangekuwa wahadhiri,
   
 10. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #10
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Hilo la kuwalipa pensheni wahadhiri wastaafu nimelipenda.
   
 11. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Hivi ni vita. Vita kati ya serikali ya kifisadi ya Kikwete dhidi ya wananchi wa Tanzania walioasi kifikra. Serikali hii haitofanikiwa kamwe katika vita hivi.

  Sijui kama ahadi za Kikwete alizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi zitatekelezwa; maana naona kila kukicha serikali inajipa kazi mpya.
   
 12. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,880
  Likes Received: 1,050
  Trophy Points: 280
  Basi wawapatie scheme of work na lesson plan!! aaahh na silabasi. Na kila darasa liwe na muintelejensia mmoja kila lecture. HUYO WAZIRI NI KILAZA, HAJUI MAANA YA KUTOA LECTURE NA KUFUNDISHA!!!! NI MUOGA, ANAOGOPA CRITIQ ZA UOZO WAO SERIKALINI!! Inabidi aingie darasani kwanza mwenyewe. na ajifunze definition ya kuitwa mhadhiri na si mkufunzi, ama mkurufunzi ama mwalimu!!!!
   
 13. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  are these people serious??? hakyamungu maofisi ya serikali ndio vijiwe vikubwa vya siasa za upinzani kwa serikali na ccm so watamchunguza nani watamuacha nani? nishapata kusafiri na maafisa waandamizi wa serikali mfani makatibu wakuu, manaibu katibu wakuu wa wizara, naibu waziri fulani woote wanaisema vibaya ccm. kama ni hivyo TISS watakuwa bize na kusaka wapinzani wa ccm kuliko kuchunguza ishu za usalama wa taifa.
   
 14. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #14
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Huu ni mkakati wa kuficha uozo wa serikali ambao hautafanikiwa.
   
 15. w

  wazo mbadala Member

  #15
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hili jambo liangaliwe kwa umakini kwani unaweza kuta mhadhiri wa ualimu aananza chambua viongozi wa serikali na kupandikiza chuki miongoni mwa wanachuo.
  kama wanapenda siasa basi wajiunge na vyama wanavyovipenda na kupanda majukwaani.
   
 16. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Naona kaburu kaingia Tanzania, kama yaliyokuwa yanafanyika SA kabla ya uhuru. Mrs Masambuka.
  Wanasahau kuwa binadamu ana utashi lazima aeleze kinachomsumbua, aluta continua hata sie wa chekechea tuendeleze.
   
 17. b

  bulunga JF-Expert Member

  #17
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 290
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwanini akasemee MUHAS, kama si chuo hicho inaelekea wanajua ni wapi ,
   
 18. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #18
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  Amechanganyiliwa huyu. anachosema ni kuwa wahadhiri wafundishe theory na wasitoke ndani ya box!
   
 19. N

  Ntandalilo Member

  #19
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NO!!!........Kuambiwa ukweli kuhusu hali ya maisha ya sasa na nini kinaendelea katika nchi yako si kupandikiza chuki bali ni kutoa mwongozo na mwanga kwa jamii especially kwa generation kama ya wanavyuo ambayo ndiyo tunaitegemea sana kutupa viongozi wazuri ambao watajifunza kutokana na makosa ya wengine!!! . I thought you'd appreciate what wahadhili are doing na si kusema hayo uliyoyasema!!!! by the way ni siasa zilizokufikisha hapo ulipo mkuu. Pole sana!!!!
   
 20. maulaga

  maulaga JF-Expert Member

  #20
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 472
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jamani, wahadhiri wa vyuo vikuu hawaokotwi mitaani bali ni wasomi waliobobea, Mlugo, naibu waziri wa Elimu na Kawambwa wake wanalifahamu hili. Iweje wanakuja na matamko ya kutatanisha kama ya UVCCM?

  Kawambwa, umesahau kitu kinaitwa 'Academic freedom' ambacho wahadhiri wamepewa? Mulugo anaweza akawa hajui kwani hakupitia huko, lakini Kawambwa unachekesha!
   
Loading...