Wahadhiri waeneza siasa za chuki vyuoni

What about those who teach Political Science? Wengine ndiyo taaluma yao kuchambua siasa 24/7! Kukiwa na migomo ndiyo kwanze research inaanza.

Jamani tutaua taaluma kwa kuingiza siasa vyuoni. huu ni mkakati maalumu wa kuwatisha Wahadhiri na wamesahau hizi sio zama za Chama kimoja cha siasa.

Wahadhiri wasitishike. Muajiri wa Wahadhiri ni baraza la chuo husika na Jukumu la kuangalia nani anafundisha nini sio la serikali bali la Mkuu wa idara inayohusika. Watakao fukuzwa waendelee kutafuta pesa zao kwingine kwani serikali itawalipa mishahara yao yote baadaye pamoja na riba baada ya kushinda kesi mahakamani.
 
Inanikumbusha sinema ya "SARAFINA".....Serikali ya Kikwete inaongoza nchi kwa wasiwasi kama serikali za wakoloni na ile ya makaburu wa Afrika kusini enzi hizo.Shughulikieni matatizo ya wananchi acheni kucheza mipasho ikulu!.
 
Hatuwezi kuwa wanasiasa wote kwa wakati mmoja mkuu...nani atmsikia mwenzake..nani atamkosoa mwenzake..inamaana watabaki kulumbana tu..ndo maana kuna "WACHAMBUZI"!

Je, CCM ingekuwa inasifiwa madarasani wangetamani kuwafanya waache? Ni mawazo mgando tu ya VIO..NGOZI tulio nao! wawajibike na kuboresha maisha ya waTZ waone kama haya yataendelea! kaz kwel kwel...itabidi waende basi mpaka kwenye vijiwe vya GAAWA mitaani, ndani ya vyombo vya usafiri etc- cjui huko watawawajibisha malecturers wa aina gani?

THE GOVERNMENT OF CCM-IS "THE GOVERNMENT OF THE FEW PEOPLE, BY THE FEW PEOPLE AND FOR SPECIFIC PEOPLE"! watafunga huko..na kufungua kwingine.. ushindi wao hauna uhakika!

hili jambo liangaliwe kwa umakini kwani unaweza kuta mhadhiri wa ualimu aananza chambua viongozi wa serikali na kupandikiza chuki miongoni mwa wanachuo.
kama wanapenda siasa basi wajiunge na vyama wanavyovipenda na kupanda majukwaani.
 
Masikini CCM.

Nadhani kwa wabunifu hapa kuna dili. Ukiweza pika data ktk research angalau wapate mtu mmoja ambaye ataitwa adui wa dini/No chama mradi awe adui wa mafisadi uweke na vi eveidence kidogo ambavyo kwa uwezo wao hawawezi shtukia unaukata.

Usishangae hotuba ya Rostam dhidi ya Mengi ilikuwa ikichekesha ila alipanda kwa ushujaa km Gaddafi na kuanza shuka mistari. Sijui kama Tido alichukua hela ya kipindi au alitoa hela ya ofisi ikajilipa kama amelipa na bado wakamtafuna.
 
Hii ni kwakuwa wanaipinga ccm ingekuwa waupinga upinzani basi wangeambiwa endeleeni. kama mtu anafundisha political science utamzuiaje kuongelea siasa za bongo darasani?
 
CCM ndio waanzilishi wa game hili. Sema sasa limekuwa kali kuliko na linawaelemea. Hata hivyo vugu vugu hili si rahisi kwisha. Mwenzio akimwaga mboga wewe mwaga na wali au ugali kabisaaaaaaaa.

Bado watapata cha moto. Mie ni mmoja wa wahadhiri hao nitaendeleza harakati. teh teh teh teh teh
 
Sasa hivi hata ukiongea na simu utaambiwa unaeneza siasa za kuipinga serikali..
 
Serikali ya ccm imesahau majukumu inakalia mipasho na ze comedy kulalamalalama ka kahaba aliyedhulumiwa.timizeni ilani yenu kwa wananchi na siyo kuogopa kivuli chenu mafisadi wakubwa nyie!!!!!pambafuuuu mi wananiudhiiiii!!!!
 
Eti uchochezi! Kinachochewa kinachowaka. Nani aliyewasha? Masuala ya msingi ya nchi lazima yaongelewe, iwe darasan , vyumbani, barabaran na hata maofisin, watachunguza wengi sana.
 
Mi najua inayoongelewa ni udsm, waadhiri hawawez kutujengea chuk na serikali, chuk tayar zpo, kama watu 2nadai 5000 haitoshi, wao wanakuja na washawasha na mabomu nin maana yake?
 
Kawambwa kachemka kwenye ujenzi ataweza Elimu matokeo yake ndio hayo majungu kutwa kucha! Waache siasa wafanye kazi hizi habari za wahadhiri wawaachie wanafunzi wenyewe kama wanaona inakosewa basi wafute facult ya political science na masomo yake yote pamoja na somo la uraia mashuleni!
Jamani, wahadhiri wa vyuo vikuu hawaokotwi mitaani bali ni wasomi waliobobea, Mlugo, naibu waziri wa Elimu na Kawambwa wake wanalifahamu hili. Iweje wanakuja na matamko ya kutatanisha kama ya UVCCM?

Kawambwa, umesahau kitu kinaitwa 'Academic freedom' ambacho wahadhiri wamepewa? Mulugo anaweza akawa hajui kwani hakupitia huko, lakini Kawambwa unachekesha!
 
Ni kitu kisicho ingia akilini sna. Labda huyu aliyesema kwenye shule za kata kufanyika hili nakubaliana naye, ila mwanafunzi wa chuo kikuu huwezi kumburuza hata siku moja.

Wanafunzi wa vyuo vikuu wanajuwa wapi pa kupata ukweli, wana access na sehemu nyingi za kupata taarifa, wanauwezo wa kupima yanayoendelea, wanautashi wao binafsi ambao hauingiliani na waadhiri kabisa (mara nyingine kutofautiana kabisa), pia waadhiri na wanafunzi wengine hiyo siasa ndiyo fani yao. Sasa kama huyo TISS aliwasikia katika mjadala husika asidhani walikuwa wanaeneza chuki, ndiyo kipindi chenyewe.

Ugomvi wao na waadhiri pamoja na wanafunzi vyuo vikuu kuhusu maslai yao yasiwaongezee kisingizio kingine.
 
kujadili siasa kama part ya somo ni tofauti na hichi kinachozungumziwa hapa, ni ukweli usiofichika kuwa wahadhiri wamejiingiza mno katika siasa "ufuasi wa vyama vya siasa" kiasi kwamba hata majukumu ya kazi yao yanakuwa nyuma siasa kwanza kazi baadae, wanavunja sheria za kazi, nadhani ni muafaka sasa kwa serikali kuwafanyia kazi, mhe rais na waziri msirudi nyuma wawajibishwe wahadhiri wa namna hii, story nyiiingi kazi hawafanyi
 
'Wahadhiri ni watu OBJECTIVE wanajua nini cha kufanya kwa wakati na mahali gani
ukiona lecturer analeta siasa kwenye theatre ni ZUZU' - Dr. Mkumbo
 
zipo coz ambazo huwezi kuacha kuzungumzia siasa mfano Political Science au hata sheria kwa mfano Constitutional lw, Human Rights, Administrative law na zingine.

Serikali iseme kuwa imeshndwa kazi na wanatafuta mbaya wao wakat wanamjua aka ufisadi.

Nadhani ni muhimu kwa wahadhiri kulitolea kauli hili ili kuwakemea mawazir wa JK kuwa makini na kauli zao.

Serikali inataka kumfunga mdomo kila mtu sasa, mwishowe watatuambia wananchi tusizungumze chochote mpaka kwenye vikao.
 
Naona kaburu kaingia Tanzania, kama yaliyokuwa yanafanyika SA kabla ya uhuru. Mrs Masambuka.
Wanasahau kuwa binadamu ana utashi lazima aeleze kinachomsumbua, aluta continua hata sie wa chekechea tuendeleze.

Hapo kwenye red nakupa thanks,kuchukia tabia ya ufisadi/ugonjwa wa ufisadi tiba yake kwa sasa lazima Chekechea waanze kufundishwa kuwa ufisadi in zaidi ya Ukimwi!
 
Back
Top Bottom