Wahadhiri waeneza siasa za chuki vyuoni

Wahadhiri waeneza siasa za chuki vyuoni

Mimi naona vyama vya wanataaluma vyuoni waweke petition huyo Waziri aondolewe haraka sana maana hayupo katika kuangalia maslahi ya wanataaluma na nchi kwa ujumla ila maslahi ya kundi la watu serikalini, anashindwa hata kutafsiri maana ya serikali je hao waalimu wao si sehemu ya serikali? Au anafikiri serikali ni CCM?
 
Mimi nafikiria kuwa kwenye vyuo vyetu ndio kuwa chimbuko la ukombozi hata mawazo mbadala badala ya kubakia kusema siasa marufuku vyuo America na Ulaya kuna vyama na matawi kila vyama kwenye vyuo vikuu mathali America kuna tawi la Republicans na democratic katika kila vyuo Je kama sio Siasa hata JK angeanzia wapi??

Jamani haya ni mawazo gani kutolewa na waziri?
 
Hii nchi sasa imefikia patamu...

Wahadhiri wanataka kuleata vurugu na kuchuchea chuki, CHADEMA wanaleta vurugu na kuchuchea chuki, Mwanahalisi linaleta vurugu na kuchuchea chuki, Mwakyembe & Sitta n.k wanaleta vurugu na kuchuchea chuki, wanafunzi vyuoni wanaleta vurugu na kuchuchea chuki, walimu wanaleta vurugu na kuchuchea chuki n.k

Alfu Mufti nae anajiunga kwenye ujinga huu!! Hapa ni kwamba Serikali imekufa......sasa inatafuta mchawi wa kusingizia kuwa ameiroga! ilhali imejiroga yenyewe kwa kuwa na viongozi wabovu kama Kikwete na wenzake.....

Nasio vuo tu kwa taarifa yao sasa hivi hata waalimu wa sekondari wanaichongea mno serikali kwa wanafunzi! na wanafunzi wanahamasika kweli!!! Dawa sio kulia lia na kuwasumbua UWT kuchimba watu....
 
Wanatapa tapa sana katika kipindi hiki kila mtu wanamuona mchawi wao ila ukweli ni kwamba CCM haina Jipya kabisa katika siasa za vyuo vikuu
 
Iundwe tume ya kuwachunguza na ipite kila chuo kuwahoji wahadhiri na wanafunzi wao!
 
Sasa hapo ni vyuoni tu, ktk shule za sekondari hasa za kata walimu wanaongelea sana siasa na kuiponda serikali kwa wanafunzi na hii ni kwa sababu ya maslahi duni ya walimu.

Wameamua kuwaharibia, yaani serikali ya CCM mna kazi mnashambuliwa kila kona mtasalimika kweli?

Dawa ni ccm kuanguka mweleka hakuna atakayeongelea siasa maana na umaskini tutauaga. MUNGU SAIDIA AFRIKA-MUNGU SAIDIA CHADEMA
 
SERIKALI inawachunguza wahadhiri wa vyuo vikuu nchini wanaotumia muda mrefu madarasani kuzungumzia siasa badala ya kufanya kazi zinazohusu taaluma.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, Serikali ina taarifa kuwa, baadhi ya wahadhiri wanatumia muda wa kutoa mihadhara ya masomo kwa kuzungumzia siasa hasa kupiga vita Serikali iliyopo madarakani.

"Tunaendelea na uchunguzi wa kuwabaini baadhi ya wahadhiri wanaojihusisha na siasa kwa kuingia madarasani na kuzungumzia siasa kwa dakika kumi kabla ya kuanza kufundisha," amesema Mulugo.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo, lengo la wahadhiri hao ni kuwafanya wanafunzi kuchochea migomo na maandamano na kupandikiza chuki baina ya Serikali na wanafunzi.

Naibu Waziri ameyasema hayo katika mkutano kati ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili (Muhas), Dar es Salaam.

Mulugo amesema, ingawa si katika chuo hicho, lakini kuna taarifa katika baadhi ya vyuo vikuu, wahadhiri wanafanya hivyo na kuwaonya kuwa kazi yao ni kuelimisha na si kuwavuruga wanafunzi akili kwa kuchanganya yale wanaojifunza na siasa na akawataka kujiepusha na siasa kwa kuwa wao ni wataalamu.

"Tena siasa zenyewe ni za kupiga vita Serikali iliyopo madarakani, tutawachukulia hatua," alisisitiza.

Kauli hiyo iliungwa mkono na Waziri Kawambwa ambaye aliongeza kuwa wahadhiri wasipojihusisha katika siasa, watasaidia kuweka utulivu katika vyuo na kuepusha migogoro.

Awali, kabla ya onyo hilo, Dk. Kawambwa alisema Baraza la Mawaziri limeazimia kuanzia Machi mwaka huu wahadhiri wastaafu walipwe pensheni sawa na wastaafu wengine serikalini.

Alifafanua kwamba uamuzi huo unatokana na malalamiko ya wahadhiri wastaafu kwamba wanapata mafao finyu kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF tofauti na wanaostaafu kutoka Serikali Kuu ambao hupata mafao yenye neema kutoka Mfuko wa Pensheni ya Wafanyakazi wa Serikali Kuu (GSPF).

Mbali na Dk. Kawambwa, pia Rais Jakaya Kikwete katika shughuli tofauti ya kuzindua Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) jana, aligusia malalamiko ya wafanyakazi wote kuhusu tofauti kubwa ya sana katika utoaji wa mafao ya mkupuo na pensheni ya uzeeni.

"Utakuta wafanyakazi wenye viwango sawa vya mshahara, muda sawa wa utumishi wanapostaafu, mmoja anapata hadi mara tatu zaidi ya mwenzake aliye mfuko mwingine," alisema Rais Kikwete.

Kutokana na tofauti hiyo aliyosema imelalamikiwa na vyama vingi vya wafanyakazi, Rais Kikwete aliagiza SSRA iangalie tofauti hiyo kwa makini na kuhakikisha kunakuwa na uwiano sawa wa mafao kati ya mfuko na mfuko, lakini akawataka pia wazingatie ustawi wa mfuko huo.

Lakini kuhusu maombi ya wahadhiri wa Muhas, kutaka kulipwa mafao kwa mkupuo kwa asilimia 50 ya mafao yao na kulipwa kwa miaka 15 baada ya kupokea mafao ya mkupuo, Dk. Kawambwa alisema bado yanafanyiwa kazi.

Kati hilo, Dk. Kawambwa alibainisha wataalamu wanaangalia suala la malipo hayo kwa kuwa limeonekana na utata unaoweza kusababisha baadhi ya mifuko kufa iwapo itapata wastaafu wengi hivyo unaangaliwa mfumo utakaotumiwa na mifuko yote.

Akizungumzia madai ya wahadhiri wa chuo hicho kuhusu posho ya nyumba ambazo hawajalipwa kuanzia mwaka jana, alisema hali hiyo ilitokana na ufinyu wa bajeti, lakini tayari wamepeleka malalamiko yao kwa Wizara ya Fedha ili walipwe katika bajeti ijayo.

Kabla ya kauli hizo za mawaziri, Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Kisali Pallangyo alielezea changamoto anazopata ikiwemo ya miundombinu michache ya chuo hicho.

Kutokana na uhaba huo wa miundombinu, kati ya wanafunzi wanne wanaostahili kujiunga na chuo hicho, ni mmoja tu anayepata nafasi wakati Taifa linakabiliwa na uhaba mkubwa wa wataalamu wa afya.

Dk. Kawambwa akijibu hoja hiyo, alisema, katika kuongeza wataalamu hasa katika masomo ya sayansi, Serikali imejipanga katika mpango wa maendeleo ya elimu ya juu kuboresha miundombinu ya vyuo hivyo ili wanafunzi wote wenye sifa wajiunge na vyuo stahili.



habari leo chanzo

Hii craps ingine yaani waziri unasimama kuutangazia uma kuwa tunachunguzi wahadhiri eti wanahutubia wanafunzi siasa hii mada na elimu wapi na wapi wee mweshimiwa embu tupe mikakati ya malengo yajao na jinsi utavyotatua matatizo ya elimu kwa ujumla wake. tatua matatizo ya elimu na sio siasa kwenye matendo.
 
Kwa kweli ninawapa pole sana wahadhiri wenzangu wa fasihi. Kwanza vitabu vitamu vya fasihi vingi vinajadili matatizo ya kijamii na namna ambavyo serikali ilivyo dhaifu katika kutatua matatizo haya.

Waandishi wanaokubalika ni wale wenye mtazamo kama wa Ngugi tofauti na hapo siwezi chagua kitabu cha mwandishi anayesifu serikali kwani sio wajibu wangu kusifu.

Huyo Mulugo ndiyo maana amesoma OUT angekwenda akakaa kampasi asingesema upuuzi wake. Ninamkumbusha na kumtaka huyu waziri atafute kitabu cha Issa Shivji Intellectuals at the Hill.

Humu ndani kuna makala nzito inayotafakari huo upupu anaousema. Wahadhiri tunaelewa gharama ya kujitenga na serikali puuzi ya CCM na tunasema tupo tayari kwa hilo na akileta ujinga wake kwa hakika patachimbika
 
Ila na nyie si ndio mnaotumika kwenye kuhesabu kura na kuiba kura na baada ya hapo mkishatumiwa mnatelekezwa saingne hata posho yenu mnakua hamlipwi hayo ndio matokeo yenu.

Amkeni msitumiwe kama vibaraka
 
Hilo la kuwalipa pensheni wahadhiri wastaafu nimelipenda.

Hiyo ni Rushwa ili waseme mazuri.
Utakuta wanaosemwa ni CCM wao wanageuza eti serikali!

Chama tawala eeee! Imekula kwenu

 
Kumbe vyuo vikuu ndo maadui wa umoja wetu!
Anzeni na REDET

Lakini nanyi CCM na serikali yenu, adui gani ni mbaya zaidi ya wote? Mara Slaa, mara Chadema, mara Vyuo vikuu, mara idd amin, mara sijui mbwa mwitu duh!

Mbona wakati wa uchaguzi mulisema UDOM ni wenu? au wamegeuka ghafla.
 
Basi wawapatie scheme of work na lesson plan!! aaahh na silabasi. Na kila darasa liwe na muintelejensia mmoja kila lecture. HUYO WAZIRI NI KILAZA, HAJUI MAANA YA KUTOA LECTURE NA KUFUNDISHA!!!! NI MUOGA, ANAOGOPA CRITIQ ZA UOZO WAO SERIKALINI!! Inabidi aingie darasani kwanza mwenyewe. na ajifunze definition ya kuitwa mhadhiri na si mkufunzi, ama mkurufunzi ama mwalimu!!!!

huyu waziri hajawahi kuhudhuria chuo chochote, anafikiri kuwa sekondari na vyuo vikuu vina mfumo sawa wa utoaji elimu, kama anabisha kauli hiyo ajitokeze wazi na atupe cv yake. so simshangai akiongea maneno kama hayo.
 
Akimaliza zoezi hili vyuo vikuu vya Umma aende vya Binafsi, Then vyuo vya elimu ya Kati, ashuke hadi High schools, nadhani round ya kwanza itaishia hapo akianza round ya pili ni Secondary schools halafu ahamie kwenye ofisi zingine za umma na binafsi kwani ndiyo hayo tu yanayo ongelewa. Badala ya kuhangaika na Kutibu matokeo ya ugonjwa angeshughulikia chanzo cha ugonjwa!

KUWA NA SERIKALI SAFI YENYE KUFUATA NA KUTOA HAKI KWA RAIA WAKE WOTE.
 
Ila na nyie si ndio mnaotumika kwenye kuhesabu kura na kuiba kura na baada ya hapo mkishatumiwa mnatelekezwa saingne hata posho yenu mnakua hamlipwi hayo ndio matokeo yenu.

Amkeni msitumiwe kama vibaraka

Kweli wewe ndio ziro brain kweli. Hivi umeona wahadhiri wa wapi wanaoenda kuhesabu kura ndugu yangu! acha kuropoka kama hauwafahamu wahadhiri siolazima uchangie huu upupu wako. Haijawahi kutokea wahadhiri wa kweli wanaotekeleza wajibu wao vema wakapongezwa na serikali haipo na wala haitakuja kutokea
 
Jana kada mmoja wa chama tawala alisema mahali fulani nikiwepo ikitokea DILI YA KWA BABU ika back fire tumekwisha kabisa maana hatuna tena la kuwaeleza wananchi wakatuelewa. Tumetumia ujanja wetu wote umeisha. Bahati tu limetokea hili la Loliondo ku divert attention ya watu nasi tupumue kidogo.

Hivyo uchunguzi uanzie kwa makada na viongozi waandamizi waliokata tamaa hata nusu mwaka bado haujaisha.
 
List hii ni nzuri naomba waanze nayo.....

  1. Dr Benson Bana(UDSM)
  2. Prof Rwekaza Mukandala(UDSM)
  3. Dr Ahmed Ame (UDOM)
 
BIG UP Serikali- CHUNGUZA -CHUNGUZA - CHUNGUZA.

Jana nilikuta kikundi cha wakulima na pia wamachinga na kinyozi wakijadili kuhusu siasa badala ya kufanya kazi kujiletea maisha bora naomba tuwasiliane ili mtume wachunguzi wakawachunguze.

Kazi kwelikweli

hii serikali kwa kweli ni sawa na mfa maji kutapatapa hakuishi. Watachunguza sana tu badala ya kutatua matatizo ya wtz na kuwatia adabu mafisadi
hata mimi nikiwa mkewangu baada ya mechi huwa tunaiponda serikali na mdadudu yake. Waje wanijunguze pia.
 
Wafukuze walimu hao. Waajiri akina profesa maji marefu,nchimbi n.k hawatafanya siasa. Ila kweli udsm kuna m1 akienda ku lecture,nusu saa anaongea siasa,dk10 international law,au communication skillz na kuishia zake daily. Watu wana uchungu na nchi. Gvt.imeua primari,imekuja sekondari/cheki f4 last yr,sasa wanakuja vyuoni. Sawa kabisa,ukitaka kumtawala mjinga mnyime elimu,endeleeni.
 
Huyu Waziri nina wasiwasi naye, kama si mpumbavu basi ni mtumwa kifikra, jamani hivi anashindwa kufikiri "(si kuwaza)" kuwa hawa wanafunz si watoto ni watu wazima sasa. Swala la wanafunzi kudai kuongezewa pesa za kujikimu kutokana na ugumu wa maisha chanzo chake ni wahadhir? Au wanafunz kugoma kutokana na kukosa mafunzo kwa vitendo chanzo ni wahadhiri? Wao hawaelew umuhimu wa mafunzo kwa vitendo?

Halafu mhadhiri anafundisha "political science" ndani yake kuna "African politics" sasa hapo mnataka afundishe nini? Siasa za magharib na kuziacha za Tanzania? Jaman kwa nini hivi mbona viongoz wetu wana FIKRA MGANDO kwanin lakin? Upumbav wafanye wao halaf waogope kuambiwa ukweli.

Waziri inatakiwa aanze kufikiri na si kuwaza maana chuo kikuu ni sehemu ambayo mtu anatakiwa ajengeke kifikra na si kuwa mtumwa kifikra. Au waziri anataka wanafunzi wafundishwe maswala yale ya "ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI" huu si wakati wake na akumbuke wale ni wahadhiri na walimu ya shule za msing.

Ni hayo tu kwa leo.
 
Back
Top Bottom