Jamani leo ni tarehe 27/4 ambayo wahadhiri waliahidi kugoma wamefanya hivyo? au zilikuwa kelele za mlango, mwenye taarifa zaidi atujuvye au mtu yeyote aliye karibu na vyuo hivyo atupe taarifa nini kinaendelea.
Mkuu, wamegoma, kwamba wameonewa vyakutosha, wamenyonywa vya kutosha, sasa wanataka mapinduzi!
Hayo waliyasema baada ya Jaji warioba ambaye ni mwenyekiti wa kanseli ya chuo kuja kuwasihi wasitishe mgomo! ambao baadhi pia walidai ushauri wake umechelewa ni sawa na kuokoa mtoto aliye kwisha fariki kwa kuzama!
Kikubwa hasa, kwamba waziri kiongozi kasema swala hilo la mafao ni la kisera ambalo linahitaji uamuzi wa baraza la mawaziri ambao haijulikani watakaa lini?
Kwa mtaji huo wamekubaliana kugoma mpaka hapo serikali itakapo pata nafasi ya kukaa kuwapa ufumbuzi wa madai yao.
Hii ndiyo habari!
Kama ni kweli basi wameandika historia! wasomi wetu wakati mwingine wamekuwa waoga na makuwadi wakubwa! Nawapongeza sana pamoja mnaweza msiogope vitisho nyie ni learned minority wengine tutawafuata
Ulie tu. Aliyebadili ni William Ngereja, ngosha mzembe aliyebanwa kama mjusi kwenye mlango hapo juzi mjengoni. Hakuwa na jinsi ya kujitetea wala kuomba utetezi kwa Kikwete kwa sababu Kikwete alikuwa kakwama na moshi wa Volcano Ulaya. Natamani ule moshi uanze tena siku akisafiri na udumu hadi uchaguzi uishe. Kukosekana kwake siku chache tu, kumeleta sheria nzuri ya madini. Akikosekana milele itakuwaje?
Mkapa kama si uwezekaji wa kijinga na kuuza mashirika na pia WIZI wake alioufanya mwisho, sasa hivi angelikuwa na heshima kubwa kama NYERERE. Wote wasubiri siku watakuja kuanza kupanda kizimbani kama walivyowapandisha wenzao akina Mramba. CCM oyeeee, Kiwete oyeeee, moshi wa volcano oyeeee.....
NB: Mbona unawachukia sana Wakatoliki? Ehhh, kuna Padri alikufanyia kale kamchezo nini? Wahi na wewe uombe Mamilioni kwa PAPA wa Kijerumani. Unaweza kuambulia walau ki-VX 6 kipya
Thanks Rwabugiri tusubiri kama serikali itawapelekea FFU kama inavyowafanyia wanafunzi wanapogomaMkuu, wamegoma, kwamba wameonewa vyakutosha, wamenyonywa vya kutosha, sasa wanataka mapinduzi!
Hayo waliyasema baada ya Jaji warioba ambaye ni mwenyekiti wa kanseli ya chuo kuja kuwasihi wasitishe mgomo! ambao baadhi pia walidai ushauri wake umechelewa ni sawa na kuokoa mtoto aliye kwisha fariki kwa kuzama!
Kikubwa hasa, kwamba waziri kiongozi kasema swala hilo la mafao ni la kisera ambalo linahitaji uamuzi wa baraza la mawaziri ambao haijulikani watakaa lini?
Kwa mtaji huo wamekubaliana kugoma mpaka hapo serikali itakapo pata nafasi ya kukaa kuwapa ufumbuzi wa madai yao.
Hii ndiyo habari!
Mkapa ujinga wake mkubwa alikuwa akiwasikiliza wezi wenzake kutoka kanisani..
NB: Mbona unawatetea sana Wakatoliki? ehhh na kuwasifia wewe ni chakula ya maaskofu na mapdre nini? endelea kuwatetea maana wanakufanyia kale -kamchezo kachafu pole.
Mkuu, wamegoma, kwamba wameonewa vyakutosha, wamenyonywa vya kutosha, sasa wanataka mapinduzi!
Hayo waliyasema baada ya Jaji warioba ambaye ni mwenyekiti wa kanseli ya chuo kuja kuwasihi wasitishe mgomo! ambao baadhi pia walidai ushauri wake umechelewa ni sawa na kuokoa mtoto aliye kwisha fariki kwa kuzama!
Kikubwa hasa, kwamba waziri kiongozi kasema swala hilo la mafao ni la kisera ambalo linahitaji uamuzi wa baraza la mawaziri ambao haijulikani watakaa lini?
Kwa mtaji huo wamekubaliana kugoma mpaka hapo serikali itakapo pata nafasi ya kukaa kuwapa ufumbuzi wa madai yao.
Hii ndiyo habari!
Kama ni wasomi wenye credentials zilizokamilika kwa nini wasitafute ajira kwingine? Kuna haja gani ya kuikamua nchi ambayo haina hata kipato cha kuwanunulia watoto wa shule madawati ? Ubinafsi umeota mizizi sana tz
Sometimes don't be cynic!
Mtanzania yeyote ana haki ya kudai haki yake badala ya kukimbilia kwingine.
Maoni yangu ktk hili nadhani serikali yetu ni kama club ya walevi wanaoamua hata kuimba matusi kwa pamoja.
Mifuko hii ya hifadhi ya jamii (hasa PPF) imelalamikiwa na watumishi kwa muda mrefu sana bila majibu. Ni mifuko ya hifadhi ya jamii, ni mingi kwa nini PPF tu ndo ionyeshe upuuzi kama huo na iachwe hivyo hivyo?
Pamoja na kwamba ni mgomo wa vyuo vikuu, hapo Tanzania kila aliye na uhusianao wa pensheni na PPF ni kilio tu. Ina maana watumishi wote wa mashirika ya umma.
Yasemekana PPF wanaitegemea serikali iwasaidie mgogoro huu kwa sababu hawana pesa. Pesa nyingi zimechukuliwa na serikali kujenga majengo ya kifahari bila hata mikataba (ref. Mh Zitto). Bahati mbaya zaidi hata palipo na mikataba bado serikali hailipi madeni kwa kuamini ilichukuwa toka chombo cha serikali. Haioni sababu za kulipa madeni ya mifuko hii.
Niliwahi kuambiwa mifuko hii ni kama mfuko chakavu wa vikao vya harusi hapo Bongo. Wanachukua pesa kila wakijisikia kufanya hivyo. Lakini ktk yote haya wastaafu wanapunjwa bila sababu za msingi tena kwa nguvu na vitisho.
Naamini mgomo huu ni hatua ya mwisho baada ya kukosa mbinu mbadala. Huyo anayeitwa Rais yabidi pia aambiwe kwamba maisha bora siyo kwa wanasiasa tu!