Mkuu ni lazima kwanza uzingatie jinsi mfumo mzima wa Kibepari Unavyofanya kazi kabla hujalaumu watu.. Ule Mpango wa kijamaa wa kugoma kwa maslahi ya mtu mwngine ama kundi jingine haufanyi kazi ktk Ubepari..Kila mmoja wetu ktk makundi yetu atasimamia kwanza maslahi yake na wewe unaweza kuwaunga mkono ama kupinga kulingana na tatizo lenyewe..Kugoma kwa ajili ya maslahi yako binafsi sio jambo la kiungwana wala kishujaa, these people are self centred.
Watanzania wangapi hawana uhakika wa kula, watanzania wangapi wanakosa matibabu kwa ajili hawana pesa za kulipia matibabu, watanzania wangapi hawana ajira, watanzania wangapi wanashidwa kuwalipia school fees+uniforms watoto wao. Sasa hawa wasomi wenye mishahara mizuri na wengi wao wamesomeshwa bure na Watanzania hawa masikini bado wanagoma eti pension zao ziboreshwe ndio watafanya kazi(kazi ya kulipwa sio bure).
Mimi nilitegemea hawa wasomi wange goma siku nyingi hasa wakati serikali inaondoa sera ya free education kwenye higher institutions. Hawa wasomi nilitegemea wangeweza kubuni mikakati kabambe ya kuondoa umasikini uliokithiri kwenye nchi yetu na kugoma kama serikali ingeshindwa kuitekeleza, sasa hawa tunaotegemea wasaidie Taifa hili nao wanagoma tena kwa ajili ya manufaa yao binafsi. Hii ni hatri kubwa.
Hata siku moja usije tegemea kwamba mkulima atakuja tetewa kwa ngomo na mfanyakazi, ama tatizo la wanafunzi kushughulikiwa na wahadhiri hali wao wenyewe kula yao inatokana na wanafunzi..Ubepari ni biashara, ni mfumo wa biashara kwa maslahi ya wote hivyo Ubepari kwanza unawagawa watu kwa makundi kisha wanaanza kujitafuna wenyewe, mwenye nguvu ndiye ata survive..hali Ujamaa unalenga kuwa shida ya mwenzako ni shida yako pia, kwa umoja wenu mnaweza kukabiri tatizo la jirani yako kwa pamoja.
Kilichofanyika ni halali na safi sana.... hili ni somo jipya kwa makundi mengine kujitambua kuwa kila mmoja wetu kaubeba Msalaba wake. Na Uzito wa mzigo huo utajulikana tu ikiwa mbebaji atapiga kelele za kushindwa na kuutua mzigo huo...