Wahadhiri vyuo vikuu vya umma kugoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wahadhiri vyuo vikuu vya umma kugoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Apr 23, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wahadhiri wa Vyuo Vikuu vya umma nchini wametangaza kuanza mgomo kuanzia Aprili 27, mwaka huu. Hatua ya wahadhiri hao imefikiwa jana kwenye ukumbi wa Cafteria One sehemu ya Mlimani Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  Mwenyekiti wa Chama cha Wahadhiri wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (Udasa) Dk Damasi Nyaoro alisema wahadhiri hao walifikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na ahadi hewa zinazotolewa na serikali kuhusu malipo ya madai yao.

  Alisema kuwa mgomo huo utavihusisha vyuo vikuu vyote vya umma nchini, yaani Chuo Kikuu cha Dar es salaam sehemu ya Mlimani UDSM, Chuo cha Sayansi ya Afya na Tiba Muhimbili, Chuo cha Ualimu ChangÂ’ombe (Duce), Mkwawa (Muce), Chuo Kikuu cha Sokoine (Sua), Chuo Kikuu cha Mzumbe (Mu) na Chuo cha Ushirika Moshi.

  Kura zilizopigwa jana za kupata maoni ya kugoma au kutogoma zilikuwa 439 ambapo kura 415 kati ya hizo ziliafiki mgomo na kura mbili ziliharibika na kura 22 hazikuafiki wala kukataa mgomo.
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  out of curiosity, wahadhiri wanadai nini?
   
 3. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Sawa lakini wamekumbuka shuka wakati kumepambazuka. Ngoja wajaribu, labda matokea yatawapatia fundisho.
   
 4. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  - mishahara minono
  - marupurupu
  - taxi relief kwenye pato
  - maisha bora kwa ujumla
  -
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Umesahau merekebisho ya kiinua mgongo (pension).
   
 6. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  kazi ipo kwa serikali na ina wakati mgumu sana kuelekea uchaguzi mkuu
   
 7. K

  Kagasheki Member

  #7
  Apr 23, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawaunga mkono kwa asilimia 100 maana kwa muda mrefu sana wamekuwa wavumilivu vya kutosha kutokana na wengi wao
  kuegemea kwa kiasi kikubwa upande wa Serikali.Ilifikia hatua hata mambo ya msingi ktk taifa yasioenda sawa baadhi yao walikuwa wakiyasapoti kana kwamba hayawaathiri na wao.Sasa wameligundua hilo na uvumilivu umewashinda wakiona baadhi yao wanajitoa kwenye kazi hiyo kwenda kwenye siasa kupata manono zaidi.Hivyo ni hatua nzuri na muhimu kuelekea kwenye mabadiliko ambayo wengi wetu tumeyapigia kelele kwa muda mrefu.Kila la kheri kama kweli mmedhamiria kutimiza hilo
   
 8. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hakuna kitu hapa. Tanzania hakuna cha msomi. Tena afadhali wakulima na wafugaji wa kule kijijini wanaweza mara nyingine wanakuwa na msimamo wa kweli. Kwa hawa wasomi wetu serikali haina pressure yoyote. Hapa serikali itawapa watu wachache ulaji na wengine watabaki kushangilia na kukitukuza chama!
   
 9. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye red; hiyo ndiyo gharama ya upuuzi wao, kwani walidhani kuwa wanasiasa wanaweza kuwa marafiki zao. Ilifikia mahali wahadhiri wakawa wanawaona wanafunzi wanaopigania haki zao kama vichaa. Sasa ni zamu yao. Natamani kuona mwisho wa hii kitu.

  Sidhani kama hawa watu wako kwenye huo matazamo wa kupigania mabadiliko. Kama wangeamua toka zamani kuwaunga mkono wenzao wachache kama akina Prof Baregu tungekuwa mbali sana. Hapa wanachohangaikia ni ulaji wao tena baada ya kuona wanapigwa bao na walimu wa shule msingi kwenye kiinua mgongo. Wahadhiri wengi wa Tanzania hawana muda kabisa na mabadiliko ya kweli kwa ajili ya kuhuisha demokrasia.
   
 10. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Duu?? Kumekucha, wacha tuone, serikali imezoea, madaktari wakigoma, hukimbilia kuleta askari magereza /jkt, jw wakatibu watu, sasa tusubili kuona JKT wakiwapiga shule vijana wetu huko vyuoni!

  Lakini bwana serikali imezidi, wao wanacho jua ni siasa tu kwa kwenda mbele, hakuna kipa umbele katika mambo ya msingi, yaani haingii akilini, mtu kwenda kusinzia kwenye mjengo Dodoma kwa myaka mitano, afu eti anapewa milioni 46! Prof, anapinda mgongo zaidi ya myaka 30 kumfunza mtaalamu wa kuokoa uhai wa watu na mipango endelevu ya taifa, anaambulia milioni 25! huu ni upuuzi usio vumilika!

  Japo vijana wetu watateseka , lakini kwakweli huu unyanyasaji hauvumiliki!
   
 11. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #11
  Apr 23, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Haya tusubiri na tuone.
   
 12. R

  Rayase Member

  #12
  Apr 23, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ndugu wana JF ninaungana na wahadhiri hawa katika kilio chao. Ningependa kujua zaidi kuhusiana na hii sheria mpya THE SOCIAL SECURITY (REGULATORY AUTHORITY) ACT, 2008. Ukisoma section 30 inasema "Every employer in the formal sector shall be required to register his employee with any of the mandatory scheme, provided that it shall be the right of the to choose the mandatory scheme under which the employee shall be registered". Now my question ni kwanini mpaka kesho hii mamlaka haijaanza kufanya kazi ili kurekebisha kasoro zilizopo? kwan kwa mtazamo wangu kama hii mamlaka ingekuwa active pengine madai ya wahadhiri yangekuwa tayari yanatekelezwa. Nisadieni jamani kifanyike nini
   
 13. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Kwa hilo la mgomo ambao wahadhiri wanataka kuufanya ni kaswali kadogo hapo.

  Je Serikali yetu ya Tanzania na vingozi wake wa nyanja mbalimbali ni kuwa wameamua kutupeleka ki dictator? mbona hii hali ya kufukuta(Migomo) kwa taasisi na maofisi mbalimbali kuanza kugoma kumeshamili sana hii inashiria nini zaidi?
   
 14. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #14
  Apr 23, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wao walisema kuwa wafanyakazi wanagoma kwa kivipi??
   
 15. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,168
  Likes Received: 5,593
  Trophy Points: 280
  Raisi kikwete nenda katubu dhambi ulizofanya ndugu yetu
  mwaka unao uu vinginevyo kazi unayo hizi zote ni dhambi tupu
   
 16. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #16
  Apr 23, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Very simple ku-deal na hii issue,

  Funga university za umma peleka watoto wote university za kanisa st..augustine wakasome mapambio
   
 17. Mnyisunura

  Mnyisunura Member

  #17
  Apr 23, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 69
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Kufanya kazi masaa zaidi ya kumi
  darasa moja wanafunzi 600 hadi 1200 CKD
  Mshahara ndo hivyo tena
  kiinua mgongo kiduchu
  security ya kazi inategemea unahem vipi utawala wa ccm
  >>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
  Kweli tunawapenda wasomi wetu!
  Je serikali inawajali hawa watu
  Tunafikiri matokeo yake ni nini
  Wahadhiri wako busy na mambo yao hakuna research wala kuandaa material kwa wanafunzi
  sylubus haziishi which means wanafunzi hawapati kile wanachotakiwa kukipata
  >>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
  Wanafunzi wa siku hizi bwana hamna kitu
  Kiwango cha elimu kimeshuka kweli! Wanafunzi wavivu hawasomi siku hizi!
  >>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
  Tunataka asome nini wakati hana cha kusoma jamani! Profesor ndo huyo mmemfratruate hafundishi yuko busy kutafuta maisha!
   
 18. Mnyisunura

  Mnyisunura Member

  #18
  Apr 23, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 69
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15

  Una uhakika kuwa vyuo vya kanisa wanasoma mapambio mkuu au ndo unasema tu mradi kusema ionekane umesema!
   
 19. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #19
  Apr 23, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Best unahakika na ulichokiandika? Kweli SAUT kuna mapambio? Chunguza best usilete mijadala isokuwa mizuri. Fuatilia kama faculties za SAUT kuna inayooffer mapambio. Tatizo lako bado una mawazo yaleyale kwamba kila shule ya kanisa inafundisha sala na nyimbo tu!
   
 20. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #20
  Apr 23, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  UDOM hawapo? au wao mambo yao shwari?????????????/
   
Loading...