wagonjwa wanalala chini muhimbili kutokana na upungufu wa vitanda wodini

Mtende

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
6,385
7,295
ndugu zangu wana jf,ni jana tu nilitoka kumtizama ndugu yangu katika hospitali ya taifa ya muhimbili,ndipo nilishuhudia jambo amalo naliwaza na kuwazua pasipo kuelewa umuhimu wa serikali yetu

wagonjwa wamelazwa chini kutokana na upungufu wa vitanda wodini,yaani idadi ya wagonjwa ni kubwa kuliko vitanda vilivyopo

kitu ninachojiuliza hivi kweli hayo ndo maisha bora kwa kila mtanzania?au ndo nguvu zaidi kazi zaidi na ari zaid? kwa kweli hali ya hapo hospiltalini inachefua siwezi hata kusimulia

hizo ahadi za kujenga reli na viwanja vya ndege kwanini hiyo bajeti isiingizwe kwenye sekta ya afya kufanya maboresho? cant tell anymore wana jf nisaidieni
 
Ukifuatilia hao wanaolala chini utakuja kuta siku ya uchaguzi wanaipigia kura CCM.
Sijui hawaoni connection au wanadhani serikali ni chama tofauti na CCM thus assuming kuwa hayo yanatokana na SERIKALI NA SIO ccm.
Ndo maana Baregu alisema ujinga wa watz ndo mtaji wa CCM
 
kwa style hii watanzania tufunguke,mabadiliko ni muhimu,nchi inaelekea wapi?????????????????
 
hebu pata hii picha, kama Muhimbili wagonjwa wanalala chini vipi kwenye hospital zetu za vijijini?
 
hebu pata hii picha, kama Muhimbili wagonjwa wanalala chini vipi kwenye hospital zetu za vijijini?

ukizungumziz vijijini unenda mbali sana temeke na mwananyamala kitanda kimoja wagonjwa wawili haijalishi wanaumwa magonjwa tofauti,hawajali kwamba wataambukizana,halafu piga hesabu ya hospitali za vijijini,kweli maisha bora kwa kila mtanzania
 
Ndo maana sisi ccm tunampango kabambe wa kuondoa haya yoote msijali subilini maisha bora kwa kasi,nguvu na kila kitu zaidi
 
ndugu zangu wana jf,ni jana tu nilitoka kumtizama ndugu yangu katika hospitali ya taifa ya muhimbili,ndipo nilishuhudia jambo amalo naliwaza na kuwazua pasipo kuelewa umuhimu wa serikali yetu

wagonjwa wamelazwa chini kutokana na upungufu wa vitanda wodini,yaani idadi ya wagonjwa ni kubwa kuliko vitanda vilivyopo

kitu ninachojiuliza hivi kweli hayo ndo maisha bora kwa kila mtanzania?au ndo nguvu zaidi kazi zaidi na ari zaid? kwa kweli hali ya hapo hospiltalini inachefua siwezi hata kusimulia

hizo ahadi za kujenga reli na viwanja vya ndege kwanini hiyo bajeti isiingizwe kwenye sekta ya afya kufanya maboresho? cant tell anymore wana jf nisaidieni

subiri turudi tena madarakani hayo ndio mikakati yetu CCM 2010 moto kwenye afya na kilimo tatu
pole sana hiyo hali watasema tangu enzi za mwinyi anynjia...
 
Ndo maana sisi ccm tunampango kabambe wa kuondoa haya yoote msijali subilini maisha bora kwa kasi,nguvu na kila kitu zaidi

awamu ya kwanza mmeshindwa kutatua hili,hali inazidi kuwa mbaya katika sekta muhimu halafu mnadai awamu ya pili mtarekebisha kwa nguvu zaidi,kasi zaidi na ari zaidi,hehe mbona nguvu mpya na kasi mpya imeshindikana lol msituchezee akili hatudanganyiiiiiki!
 
Hayo ndo maisha bora kama vile foleni za Dar. Pia tujue kuwa wagonjwa hulala chini siyo tu National Hospital bali hospitali karibu zote nchini!. JK hongera kwa kufanikisha hilo kla kulaza wagonjwa chini ikiwa ni pamoja na wajawazito kujifungulia sakafuni.
 
Back
Top Bottom