Hali tete, Hospitali nchini zaishiwa vitanda

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Wakati Serikali ikiendelea kuongeza idadi ya hospitali na vituo vya afya nchini, bado changamoto ya uhaba wa vitanda vya kulazia wagonjwa inaendelea kuiandama sekta ya afya, hasa katika vituo vya umma.

Ripoti ya ‘Tanzania in figures 2021’ inayotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), inaonyesha hospitali za mikoa, hospitali nyingine na vituo vya afya (vyote vya umma), vinakabiliwa na tatizo la kupungua kwa vitanda, huku uchunguzi wa Mwananchi ukionyesha katika baadhi ya hospitali wagonjwa wawili wanalazimika kutumia kitanda kimoja.

Ripoti hiyo imeonyesha hospitali za mikoa nchini ambazo ni nyeti na zinazochukua wagonjwa kutoka ngazi za chini, kwa mwaka 2020 zilikuwa na vitanda 7,307, idadi ambayo ilipungua hadi vitanda 7,239 mwaka 2021.

Hata hivyo, ripoti hiyo ilizitaja hospitali nyinginezo za umma mwaka 2020 zikiwa na jumla ya vitanda 1,820 kabla ya kushuka hadi kufikia vitanda 1,098 mwaka 2021 ikiwa ni tofauti ya asilimia 39.

Kwa upande wa vituo vya afya, takwimu zinaonyesha idadi ya vitanda imepungua kwa asilimia 11.4 kwa muda wa mwaka mmoja.

“Mwaka 2021 vituo vya afya vyote nchini vilikuwa na vitanda 14,363 ikilinganishwa na vitanda 16,211 mwaka 2020,” sehemu ya ripoti hiyo ilionyesha.

Hata hivyo, wakati idadi ya vitanda hivyo ikipungua, Serikali imeendelea kuongeza idadi ya hospitali, vituo vya afya na zahanati, ambapo hospitali zimeongezeka kutoka 369 mwaka 2020 hadi 404 mwaka 2021.

Vituo vya afya vimeongezeka kutoka 926 mwaka 2020 hadi 956 mwaka 2021, hali kadhalika idadi ya zahanati iliyoongezeka kutoka 7,163 mwaka 2020 hadi 7,189 mwaka 2021.

Gharama za vitanda

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Mavere Tukai, bei ya vitanda hutofautiana kulingana na kituo husika, lakini akataja kuwa kwa kitanda cha kawaida gharama huwa ni Sh606,462.

Alisema kwa kitanda kinachogawanyika mara mbili huku kikiwa na sehemu ya kuzuia mgonjwa asianguke na sehemu ya kushikilia dripu, hununuliwa kwa Sh628,998 na kilichogawanyika sehemu nne ambacho mara nyingi kinapelekwa hospitali za rufaa, ni Sh930,000.

“Kwa upande wa kitanda cha kujifungulia mama mjamzito kuna aina mbili, kilichogawanyika mara mbili kinachouzwa kwa Sh1,214,710 na kilichogawanyika sehemu tatu kikiwa na kila kitu muhimu ambacho pia ni kipana zaidi, hiki ni Sh1,411,769,” alisema Tukai.

Alisema kuna vitanda vya aina nyingi, vikiwamo vinavyowekwa katika vyumba vya mahututi, vyumba vya upasuaji na vile vinavyotumia umeme.

Athari

Baadhi ya vituo vya afya vilivyopo pembezoni, hasa vijijini vimekumbwa na changamoto ya ufinyu wa vitanda, kikiwamo kituo cha afya Katoro kilichopo Halmashauri ya Geita, ambapo kinamama waliojifungua walikuwa wakilazimika kulala wawili kwenye kitanda kimoja.

Wanawake 30 hadi 40 hujifungua kila siku katika kituo hicho na kusababisha wodi ya wazazi yenye uwezo wa kulaza wanawake 30 kuzidiwa, hivyo kuwalazimu kulala wawili kwenye kitanda kimoja.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, John Wanga alisema ongezeko la wananchi katika mji wa Katoro na maeneo jirani, ndiyo sababu ya msongamano kwenye kituo hicho na kwamba tayari halmashauri imeagiza vitanda 50 kukabiliana na ongezeko hilo.

“Tumeagiza vitanda 50, jana tumepokea 20 lakini kwa ile wodi havitoshelezi pale, menejimenti itaona wabadili ile wodi iliyojengwa kwa ajili ya wanaume itumiwe na kina mama, lakini juhudi kubwa tunazofanya ni kukamilisha hospitali ya Katoro yenye hadhi ya wilaya, ili Januari ianze kufanya kazi. Hii itasaidia kupunguza msongamano kwenye kituo hiki,” alisema Wanga.

Mganga mkuu wa Wilaya ya Geita, Modest Burchard alisema kituo cha afya Katoro kina vitanda 66, idadi ambayo inazidi mwongozo wa Wizara ya Afya inayoelekeza kituo cha afya kuwa na vitanda 50 na hiyo imetokana na wingi wa wakazi katika eneo hilo na maeneo jirani.

Dk Modest alisema kituo cha afya Katoro kinawahudumia wananchi 180,000 na kutokana na ongezeko la wananchi kwenye maeno hayo, Serikali inajenga hospitali yenye hadhi ya wilaya katika eneo la mji mdogo wa Katoro, ili kukipunguzia mzigo kituo hicho, ambacho kimeelemewa na msongamano wa wagonjwa.

Baadhi ya wataalamu wamesema vitanda vingi vinapoharibika, hakuna wataalamu wa kuvirejeresha, hali inayochangia uhaba huo.

Hata hivyo, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ilisema kwa upande wake ina idara ya ufundi ambayo imekuwa ikifanya utaratibu wa matengenezo mara kwa mara.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano MNH, Aminiel Aligaesha alisema kwa sasa hakuna uhaba wa vitanda, kwani vilivyopo eneo la Upanga ni 1,530 na Mloganzila 608.

“Hospitali ina idara ya ufundi ambayo pamoja na mambo mengine, ina utaratibu wa matengenezo kinga wa vifaa vyake vyote, vikiwemo vitanda ambapo vinakarabatiwa na kupakwa rangi kulingana na mpango kazi wa matengenezo kinga uliopo,” alisema Aligaesha.

Nini kifanyike?

Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Mugisha Ntiyonza Nkoronko alitaja sababu kuu nne za kutokuwa na vitanda vyenye utoshelevu nchini.

Alitaja sababu ya ukuaji wa uchumi wa nchi kuwa ni mdogo unaokua kwa kasi ya asilimia tano hadi sita, ilhali nchi ina mahitaji yanayotaka uchumi ukue kwa asilimia tisa hadi 10 kwa mwaka.

Dk Mugisha ambaye ni daktari bingwa wa upasuaji alitaja sababu ya pili kuwa ni sekta ya afya kutengewa bajeti finyu ya kati ya asilimia saba hadi nane, kinyume na mkataba ambao nchi iliridhia (Abuja 2001) kwamba ni lazima kila nchi mwanachama wa Umoja wa Afrika, itenge asilimia 15 ya bajeti yake kushughulikia afya.

‘‘Serikali ya hayati Magufuli iliwekeza kwenye majengo, lakini haitoshi tunahitaji miundombinu ya huduma. Wanaopanga vipaumbele waangalie mahitaji, kama ambavyo inaangaliwa kwenye madawati. Huwezi kuwa na madarasa bila madawati, ni aibu nchi inasherehekea miaka 60 kuna wagonjwa wanalala chini,” alisema.

Dk Mugisha alisema kuna ongezeko la watu na wagonjwa lakini miundombinu mingi ilijengwa miaka ya nyuma ilhali idadi ya watu inaongezeka.

“Wagonjwa 5,000 wanapokelewa Muhimbili na asilimia kubwa wanahitaji kulazwa. Magonjwa yanaongezeka, uchumi unavyoongezeka aina ya magonjwa yanaongezeka pia, lazima tujipange kikamilifu,” alisema Dk Mugisha.

Jambo linalopaswa kufanyika kuondokana na uhaba wa vitanda analoshauri mtaalamu wa maabara kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Alex Mlwisa ni Wizara ya Afya kufanya tathmini ya kina kila mwaka kuhusu takwimu za vitanda kupungua ikilinganishwa na ongezeko la wagonjwa.

“Wanapaswa kufanya utafiti kujua kwa nini wagonjwa wanaongezeka kila mwaka waje na njia za kuondoa hayo magonjwa, kwa nchi zetu kama Tanzania magonjwa mengi ni ya kuambukizwa ukilinganisha na magonjwa yasiyo ya kuambukiza,” alisema.

“Kwa hiyo magonjwa ya kuambukizwa kama yanaongezeka, yanaweza kupunguzwa na namna ya kwanza ya kupunguza ni kuhakikisha watu wanapata maji salama na wananchi wanakuwa na vyoo safi na salama ili kupunguza magonjwa yanayoshambulia njia ya mkojo (UTI),” alisema.

Kwa upande wake, Dk Mturi alisema Serikali ifanye tahmini ya upatikanaji wa vitanda kuanzia ngazi ya zahanati hadi hospitali za mikoa.

“Hapo wataweza kufanya jitihada za kuhakikisha vitanda vinapatikana kulingana na mahitaji ya eneo husika na kwa muda,” alieleza.

Naibu Katibu Mkuu Tamisemi anayeshughulikia Afya, Dk Grace Magembe alisema kupungua kwa vitanda kunasababishwa na idadi ya vituo vya afya na zahanati kubadilika mara kwa mara, hivyo kuongeza ama kupunguza uhitaji wa vitanda.

“Hapa kuna vituo vya umma na binafsi, vile vya binafsi wakati mwingine vinafungwa kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo kuachana na hiyo biashara au kubadilisha, wengine wanafungiwa kwa sababu ya kukosa vigezo vya ubora, idadi ya vituo vya afya na zahanati huwa inabadilika,” alisema.

MWANANCHI
 
Mhhhhhh
 
Tungekuwa tunazalisha chuma ingekyww kazi rahisi sana kuunda vitanda. Hata vingine tungeshindwa pa kuviweka.
 
Mtanikumbuka
 
Kuna hospital moja ya wilaya ya Rombo inaitwa KARUME aisee hakuna vitanda kabisa,yaani huwezi amini ni hospital ya serikali ina hali kama ile
 
Naibu waziri wa afya Moleli si alidai mama kapeleka Tsh. 500 Trilion sekta ya afya?
 
Attachments

  • 8506B7B4-40D4-4F0A-B264-03617805D1B3.jpeg
    8506B7B4-40D4-4F0A-B264-03617805D1B3.jpeg
    24.6 KB · Views: 5
Back
Top Bottom