#COVID19 Wagonjwa wa COVID19 waongezeka na kufikia 507

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Wizara ya Afya imetangaza visa vipya 18 vilivyothibitishwa baada ya sampuli 1,086 kufanyiwa vipimo jana, maambukizi nchini humo yamefikia 507.

Kwenye sampuli 1,086 zilizopimwa, 774 ni kutoka mipakani na 312 ni sampuli za wananchi wa kawaida na wale ambao wamekuwa karibu na wagonjwa.

Katika visa vipya 18, wanne ni madereva wa malori waliotokea nchini Sudan Kusini na kuingia Uganda kupitia mpaka wa Elegu. Visa viwili ni kutoka Malaba na 12 ni watu waliokuwa karibu na wagonjwa.

Vilevile, Wizara imesema madereva 21 waliokutwa na COVID19 wamerudishwa katika nchi zao. 13 ni Wakenya, 3-Watanzania, 4 ni raia wa Eritrea na mmoja ni Mcongo.

====



 
HUMO nchini bado wanapambana na corona, mbona nchini HUMU tushamalizana nayo na tunafanya mishe zingine?
 
Back
Top Bottom