Wagombea u-Rais Watofautishe Mipango ya Taifa na Ilani za Vyama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wagombea u-Rais Watofautishe Mipango ya Taifa na Ilani za Vyama

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Edwin Mtei, Sep 11, 2010.

 1. E

  Edwin Mtei JF Gold Member

  #1
  Sep 11, 2010
  Joined: Dec 13, 2008
  Messages: 181
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nchi yetu imekuwa na Mipango ya Taifa ya muda Mrefu ambayo imekubalika kwamba itatekelezwa. Kila mwaka wa fedha mipango hiyo hutengewa fedha kutegemea na jinsi mapato ya taifa yanavyogawanywa.

  Mifano ni barabara. Makubaliano hata na nchi jirani yanataja kwamba barabara itajengwa toka Dodoma kwenda kusini kuunganisha na ile barabara inayotoka Dar es Salaam kwenda Zambia. Barabara itajengwa pia toka Dodoma kupitia Kondoa mpaka Arusha ili kuunganisha na iendayo Kenya. Kwa mtindo huo kuna mipango ya Reli kupitia Arusha mpaka Musoma ili Uganda waweze kutumia bandari ya Tanga. Pia kutakuwa na barabara na Reli kwenda Burundi na Rwanda. Vivyo hivyo kuhusu viwanja vya ndege au bandari.


  Kama katika Mpango wetu wa muda mrefu (Long-term Plan) kuna miundombinu itakayotekelezwa. mgombea u-Rais asianze kuitaja kwamba eti chama chake kikipata ridhaa ya wananchi kitaitekeleza. Hakuna chama cha siasa kitakachofuta Mipango ya Muda Mrefu kuhusu miundombinu, huduma za kijamii au kiuchumi. Bandari, madaraja na vivuko pale ambapo vinahitajika vitajengwa na Serikali yoyote ile.


  Vyama vya siasa vijikite katika kueleza mikakati yao ya kupata nyenzo ( pamoja na kuzuia ubadhirifu wa mali ya umma) ili kutekeleza hiyo mipango. Mobilization of resources, including human resources and technology) ili kuleta maendeleo viwe ndio themes za kutofautisha vyama vya siasa.
   
 2. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  ni kweli Mzee Mtei, nashangaa wenzetu wanatoa takwimu za kudandia, eti kabla sijawa mbunge kulikuwa na shule 3 leo kuna 20, utadhani wanatoa hizo fedha mfukoni mwao. kwa nini wasiseme kabla sijawa mbunge pato la jimbo langu lilikuwa ni shilingi hizi na sasa ni hizi, umaskini ulikuwa hivi na sasa umepungua hivi.

  ninachukizwa sana na takwimu hizi za kitoto
   
 3. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #3
  Sep 11, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 156
  Trophy Points: 160
  Duh, Mzee Mtei, hii ilipaswa iwe kwa waandishi wote wa habari waieleze jamii. Leo Wagombea wanazungumzia mipango ambayo ipo kana kwamba wao ndio wanaianza. Kwa kufanya hivyo wanadanganya na ndio ufisadi tunaoupiga vita.

  Si ajabu ahadi zote za JK, kama zile kubwa kubwa za Meli Bukoba na kule Mbeya ziko kwenye mipango ya kitaifa. Maana yake wananchi wamesharubuniwa kwa maana awepo au asiwepo Kikwete ni kwamba zitatekelezwa. Jambo la kusikitisha ninaliona hata sisi wachache tuliojaliwa elimu hatuna taarifa kuhusiana na mipango hii ya kitaifa. Matokeo yake CCM hasa (nathubutu kutaja) wametumia udhaifu huu kutulaghai watanzania. Na pengine ndio maana hawataki midahalo, maana wachache wenu kama Mzee Mtei mnaweza mkaibua taarifa hizi, ambazo zitawaumbua.

  Natamani watu wengi zaidi wa umri wako wangekuwa wanaona matatizo ya jamii yetu kama wewe.
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  nadhani hii post inastahili kuwa printed na kuwekwa kwenye ma-billboard na camapign trail vehicles.... itammaliza kabisa mgombea anayetumia migongo ya mipango kwa faida yake peke yake!!!!
   
 5. B

  Bunsen Burner Member

  #5
  Sep 12, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Yaani tanzania bwana tuna matatizo!! Huu ni ukweli mtupu, manake sisi wengine tulio pata bahati kufanya kazi nje ya nchi kama Botwana , Namibia etc utaona ubabaishaji wa mbunge kudanganya watu nitawaletea barabara au kitu fulani uwa hakuna manake wana mipango tayari ya short and long term ya serikali to be done, na mbunge wewe ni kufuatilia utekelezaji wake na hakuna mtu unayeweza kudivert kirahisi rahisi, kufavour kwako kama haikuwa kwenye mpango!!

  Sisi tunafanya mambo ovyo ovyo tu na ndio maana ukiwa na influence serikalini basi unaweza kujenga barabara kijijini kwako au mahali ambapo sio priority ukiacha sehemu zinazohitaji barabara kuleta maendeleo na mapato ya fedha za kigeni kwa taifa zikiwa hazina most important infrastructure!!

  Wasomi mmetuangusha sana bongo kwa kuruhusu upuuzi huu!!!
   
 6. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2010
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  When Mr. Jakaya Kikwete was asked by Economist Magazine (in Paris) why Tanzania was poor; he simply replied; even himself [Kikwete] didn't know why. Another fix, was Mr. Sumaye. When he came back from Boston after graduating from his MBA, was heard as saying: After my Education in USA now I know why we are so poor.

  At his capacity as a president who vied for presidency of Tanzania, didn't even know why Tanzania was so poor, this is too vague. Similary this fix from Boston; was a Prime Minister for 10 years, didn't even know what he was doing when he was a Prime Minister. 10 years of Sumaye and 10 years of Kikwete(if elected) will be 20 years, a two generation gap. About 30 years have been wasted. Including Mwinyi 10 (total Economic Collapse]. We are not serious in Tanzania. We are not serious for our next generations by giving votes to these liars.

  From your theory above, especially on your last paragraph I see a big information and knowledge gap. When the world is modernizing, Tanzania is going backwards; the young generation should know more than the older generation, but it is the opposite, bravo Mr. Mtei for that piece of knowledge.
   
 7. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  what a nation's treasure. Thanx Mzee kwa upambanuzi na hekima yako
   
 8. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 156
  Trophy Points: 160
  Ndio maana JK anaweza akapeleka investments ambazo hatuna uhakika nazo mahali kama Bagamoyo, Chalinze nk. Ndio maana tunatapanya maendeleo, badala ya kuwekeza pale ambapo ni rahisi kupata faida haraka na kwa jinsi hii kupata mtaji kutokana na hizo faida ili tuweze kuwekeza maeneo yale yenye kuhitaji lakini hayawezi kuzalisha ili kujiendesha
   
 9. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
 10. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #10
  Sep 12, 2010
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Sep 12, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kumbe hizi ahadi zote anazotoa muungwana ni vipaumbele vya kitaifa! Sikuwa nikilijua hili. Hii habari inabidi kila Mtanzania aijue ili vyama (hasa CCM) visiturubuni kwa ahadi hewa!
   
 12. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2010
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Sasa tunaongea, hii imetulia. Kusema ukweli wagombea wengi wanaanza kuingia kwenye trap ya CCM. Simply CCM wanachofanya ni kusoma mipango mbalimbali ya serikali na kuahidi kuwa watafanya hiki na kile kutokana na yale yaliyopo kwenye mipango ya serikali pamoja na bajeti.

  Kwa kiwango kikubwa hii inatokana na uelewa mdogo wa wananchi wanaoshindwa kuwauliza maswali magumu. Ofcourse sasa hivi vyombo vingi vya habari ni vuvuzelas za vyama vya siasa na hatuoni hasa sera na mwelekeo. Wanasiasa na wagombea wananadi zaidi ahadi na mipango ya serikali.

  Tunachotaka kusikia wengine ni mbinu za kibunifu za kuiondoa nchi katika matatizo. Kwa mfano mtu anapozungumzia kupunguza ukubwa wa serikali na kupunguza matumizi makubwa ya kodi yanayoelekezwa kwenye uendeshaji wa serikali, hii ni mbinu ni mkakati. Labda tu aende zaidi kwa kutoa takwimu, serikali sasa hivi inatumia kiasi gani; ikija serikali ndogo ya ukubwa X itaokoa kiasi Y cha fedha. Fedha hii itaingizwa katika miradi ya maendeleo kama ukuzaji wa bandari ya Dar es Salaam n.k.

  Vile vile tungependa tusikie takwimu halisi; Ni kiasi gani cha fedha leo hii kinatumia kulipa posho za vikao (sitting allowances), Posho za safari za viongozi ndani na nje ya nchi, tunapoteza kiasi gani kwa viongozi kutumia zaidi ya asilimia 50% ya muda wao wa kazi nje ya vituo vya kazi (wakibangaiza viposho), Tunapoteza kiasi gani cha fedha kwa biashara zinavyofanyika kiholela mitaani bila kufuata kanuni na sheria zilizopo. Je tukileta ufanisi kwenye maeneo hayo tunatarajia kuokoa kiasi gani, na tutazielekeza kwenye maeneo gani.

  Uchumi wetu uko hoi bin taaban kwa sababu mbali mbali, ni zipi hizo? Wagombea waseme sababu hizo watapambana nazo kivipi. Kwa mfano, miundo mbinu chakavu kama reli, bandari, bara bara, usafiri wa anga nchi kavu na majini, upatikanaji wa umeme wa uhakika, maji, n.k. Mgombea makini inatakiwa aje na Takwimu; kwa mfano sasa hivi bandari zetu zote zinashughulikia shehena za mizigo kiasi gani? Kwa nini shehena inayopitia kwenye bandari zetu ni sehemu ndogo tu ya mizigo inayopitia bandari ya Mombasa. Kutakuwa na mbinu gani ya kuziongezea bandari zetu competitive advantage na kuzifanya zitumiwe zaidi na waagizaji wa mizigo kutoka nchi jirani na kuongeza mapato ya bandari zetu (kwa kiasi gani), n.k.

  Ubunifu katika ukusanyaji wa kodi kwa kupanua wigo wa kodi; Maeneo ambayo leo hii hayaguswi na wigo wa kodi kama kodi za nyumba (na za kupangisha), kodi nyingi za biashara ambazo hazisimamiwi vizuri na kuboresha usimamizi wa ukusanyaji wa kodi. Mapato ya serikali yanatarajiwa kuongezeka kwa kiwango gani na yakishaongezeka yataelekezwa wapi?

  Kwenye kilimo kwa mfano ni mbinu zipi zitatumika kuhakikisha uzalishaji unaongezeka kwa viwango vinavyopimika. Mfumo wa masoko ya mazao ya wakulima ndo eneo lenye matatizo makubwa. Ikiwa ruzuku kwa mfano zitatolewa kwenye mbolea, ni mbinu gani itatumika kuhakikisha wakulima wanapata bei zinazolingana na gharama wanazotumia kuzalisha. Kwa nini Wagombea wasizungumzie jinsi ya kuwaunganisha wakulima moja kwa moja na wanunuzi ili kitakachozalishwa kiwe kinauzwa kwa faida. Wagombea wawe wanaongea kwa kutumia takwimu badala ya kuongea kama kasuku; kusema kweli kauli zingine za kusema simply tutafanya hili na lile bila kueeleza kwa undani zaidi zinatia wasi wasi hasa kama wanaosema hivyo wanaelewa wanavyoahidi... ndo mambo ya kuahidi viwanja vya ndege maeneo ambayo wanaotumia usafiri wa ndege ni viongozi tu.

  Kampeni zimezama kwenye mipango na mikakati ya muda mfupi ya serikali. Hatusikii viongozi wakitueleza mikakati hasa inayopimika ni jinsi gani wataielekeza nchi hii kwenye ubepari wenye sura ya kibinadamu. Jinsi watakavyohakikisha mfumo wa masoko unadhibitiwa kuwalinda walaji na wauzaji vile vile, n.k.

  Labda wito huu wa Mzee Mtei utasaidia. Ahadi tu hazioneshi jinsi tulivyo makini. Mikakati iko mingi na kuna taasisi zinazoendesha nchi kama TRA, benki kuu, Mabenki ya biashara, Makampuni ya simu, n.k. Wagombea inatakiwa watuoneshe mbinu mbadala wa kurekebisha taasisi hizo na sekta mbali mbali zilizopo ili zendeshwe kwa ufanisi zaidi na kuchochea ukuaji wa uchumi na biashara.

  Kwenye matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano kama chombo cha kutawala na kutoa huduma bora, kama chombo cha kuleta ufanisi ndani ya serikali, kama chombo cha kutoa ajira na kukuza biashara, n.k. Ni maeneo gani hasa ambayo wagombea wanadhani hatujafanya ya kutosha kuweza kuvuna nguvu iliyopo kwenye matumizi makubwa ya teknolojia ya habari na mawasiliano. Kwa mfano kwenye maeneo ya ukusanyaji wa kodi kwa mfano Dar es Salaam nzima ni ofisi moja tu inayotoa huduma za ukusanyaji wa kodi za leseni za magari, usajili na kadhalika. Je matumizi ya teknolojia ya habari hayawezi kutusaidia kutawanya huduma hii maeneo mengi na kwa gharama nafuu na kuongeza ufanisi na ukusanyaji wa kodi za magari? Ni watu wangapi wenye magari wanaolazimika kuwalipa vijana uchwara waliojazana pale samora ili kuwasaidia kutokana na misongamano ya walipa kodi ndani ya eneo moja! Ni walipa kodi wangapi wanaochelewa kulipa ushuru na tozo mbali mbali (au kutolipa kabisa) kutokana na mfumo huu mbovu usiotumia mbinu za kisasa zilizopo?

  Wagombea wetu watuambie watatumia mbinu gani mbadala kuongeza ufanisi (kwa viwango vinavyopimika) wa makusanyo ya mapato ya serikali; je inatakiwa VAT ishuke au iongezeke. PAYE je? ....n.k....n.k.

  Hizi kampeni za kusema nitaleta maji, nitaleta meli, nitaleta bajaj, n.k. naona kama zinaakisi upungufu mkubwa uliopo kwenye timu za kampeni. Inaonekana hakuna watalaamu, kumejaa wabangaizaji na waganga njaa tu. Bahati mbaya hao ndo watakaohamia serikalini vyama vyao vitakaposhinda.
   
 13. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Wako watu wachache sana Tanzania wenye busara na uelewa kama Mzee Mtei. Marais (hata Kikwete) wangekuwa wanawaomba watu kama Mzee Mtei wawe washauri wao rasmi. Kwani Mshauri lazima awe mwana CCM? Jibu ni hapana.
   
 14. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  How praiseworthy it is for a prince to keep his word and to live by integrity and not by deceit everybody knows; nevertheless, one sees from the experience of our times that the princes who have accomplishes great deeds are those who have cared little about keeping their promises and who have known how to manipulate the minds of men by shrewdness; and in the end they have surpassed those who laid their foundation upon honesty.

  -- Niccolo Machiavelli, The Prince.

  Kikwete is, sadly, playing right out of the Machiavellian book.
   
Loading...