Tuna mi-vyama isiyo na itikadi wala falsafa! Ni mi-vyama ya matumbo ya u-binafsi tu!
Fikiria, mtu mwenye cheo cha Mkuu wa Mkoa, Prof. mzima, Daktari (Mganga) au Katibu Mkuu anaacha kazi hiyo kwa ajili ya kutaka kuwa m-Bunge!
Nilishasema kuwa kadiri taifa linapozidi kuongeza mishahara mikubwa na marupurupu kwa wa-Bunge wetu, ni kukaribisha umwagaji damu!
CCM inajua wazi kuwa rushwa, kadi feki na wizi wa kura vilitendeka. Lakini CCM inafumba machio kwa kuogopa kuwa mafisadi hao na wezi hao kuwaadhibu kwa kuwakataa watahamia upinzani (CHADEMA, hasa). Kwahiyo, ni sharti wakumbatiwe!
CHADEMA, kwa ajili ya kupalilia unga wa ushindi, inawakaribisha, inawakumbatia na inawatuza wakimbizi kutokaa CCm kwa kuwapa nafasi ya kugombea ubunge!