Wagombea CCM Waanza Kumiminika Chadema! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wagombea CCM Waanza Kumiminika Chadema!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, Aug 16, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Aug 16, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Boniface Meena

  BAADA ya kukosa ridhaa ya kugombdea ubunge kwa tiketi ya CCM kutyokana na chekeche la mwisho la halmashauri kuu ya chama hicho, waliokuwa wagombea ubunge na wanachama waandamizi watano wamekitema chama hicho na kuhamia Chadema.Baada ya kumalizika kwa kura za maoni ndani ya CCM ambazo ziliripotiwa kuwa zilijaa rafu, ukiukwaji wa taratibu na wagombea kukamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), tegemeo la mwisho la wagombea wote lilikuwa kwa halmashauri kuu ambayo ilimaliza kikao chake Jumamosi.

  Chombo hicho chenye nguvu ndani ya CCM kilibatilisha ushindi wa wagombea watatu tu na kuidhinisha ushindi kwenye majimbo mengine yote licha ya kuwepo malalamiko na rufaa nyingi kupinga ushindi.

  Naibu katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe aliiambia Mwananchi kuwa wanachama wa CCM waliojiunga na chama chake kuwa ni Dk Raphael Chegeni, John Shibuda, Alatanga Nyagawa na Thomas Nyimbo.

  Alisema kuwa kwa sasa tayari wameshawachukua hao na wanafanya jitihada za kumpata aliyekuwa mshindi kwenye kura za maoni jimbo la Nzega, Hussein Bashe ili aweze kugombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema. Bashe alimuangusha mbunge aliyemaliza muda wake, Lucas Selelii kwa kura nyingi, lakini CCM imemteua mshindi wa tatu kugombea ubunge.

  Kabwe alisema kuwa tayari wameshampitisha Shibuda agombee ubunge wa jimbo la Maswa Mashariki kwa tiketi ya Chadema, huku Chegeni akipitishwa kugombea jimbo la Magu, Nyagawa jimbo la Njombe Kaskazini na Nyimbo jimbo la Njombe Magharibi.

  "Hao wanne tayari tumeshakubaliana nao na tunazidi kuwatafuta wengine kama aliyeshindwa jimbo la Nkenge ambaye sitamtaja jina kwa sasa ila tuna matumaini ya kumpata pamoja na mwingine wa Shinyanga Mjini," alisema Kabwe.

  Alisema kuhusu Bashe, Zitto alisema wanataka kumchukua ili kuwaonyesha Watanzania kuwa hawana ubaguzi wa rangi kwa CCM wanamjua Bashe kwa muda mrefu na inashangaza kwamba wakati huu ndio wamemgeuka kwa kigezo cha uraia.

  "Tuko katika mazungumzo na Bashe tunajitahidi tumpate ili akasimame kwa niaba ya chama chetu huko Nzega... kwanza alipitishwa kwa kura nyingi ikimaanisha kuwa ataweze kukitetea chama ipasavyo," alisema Kabwe.
  Alisema kuwa CCM si mamlaka ya kusema mtu fulani ni raia au si raia hivyo walichokifanya si sawa bali wameingilia mamlaka nyingine.

  "Baba yake Bashe yuko Nzega pale, kwa nini wasiende kumfuata na kumuuliza? Hawa CCM wamekuwa na Bashe kwa muda mrefu iweje wanamgeuka sasa," alihoji Kabwe.

  Aliongeza kusema: "Tunapinga ubaguzi kwa mtu yeyote, kwa hiyo tunamtaka."

  Alipoulizwa kuhusu habari za kuhamia Chadema, Dk Chegeni alikiri kufanya mazungumzo na viongozi wa chama hicho lakini akawaeleza kuwa alikuwa safarini na alitarajia kumalizia mazungumzo, ingawa alisema mpaka jana jioni hakuwa amefikia uamuzi.

  Alisema kuwa hawezi kuzugumzia kwa kina suala hilo kwa sasa kwa kwa sababu bado hajafanya uamuzi wa kujiunga na Chadema.

  Kabla ya kujiunga na Chadema, Shibuda alikuwa katika ziara za kuaga wazee na marafiki zake wa siku nyingi ndani ya chama hicho tawala.
  Shibuda, mwanasiasa mwenye historia nzito ndani ya CCM tangu enzi za Mwalimu, alifafanua kwamba asingeweza kufanya maamuzi magumu bila kuagana na wazee waliomlea katika chama.

  Mbunge huyo wa zamani wa Maswa, alifafanua kwamba wapo wazee ndani ya CCM ambao anawaheshimu kwa kuwa ndio waliomtoa gizani na kumpandisha chati katika siasa.

  Katika safari hiyo ya kuaga wazee, Shibuda alisema wiki iliyopita alikuwa visiwani Zanzibar alikokuita kuwa ndiko alikokulia na kukomaa kisiasa.

  "Mimi niko Zanzibar nakutana na kuagana na wazee wangu. Nimelelewa Zanzibar ambako ndiko nilikokulia na kulelewa katika mazingira mazuri ya kisiasa," alifafanua.

  Dk Chegeni, ambaye alikuwa mbunge wa Busega aliangushwa kwenye kura za maoni na Dk Titus Kamani Mlengenya, wakati Shibuda ambaye aliangushwa na Martine Makondo kwenye jimbo la Maswa Mashariki.

  Naye Nyimbo alishinda kwenye kura za maoni lakini jina lake lilienguliwa na kupitishwa Gerson Lwenge na kwa upande wa Nyagawa atapambana na mwenyekiti wa CCM mkoani Iringa, De Sanga (Jah People) akiibeba Chadema.

  Katika kura za maoni za CCM, zaidi ya wabunge 60, wakiwemo mawaziri watano, waliangushwa na halmashauri kuu haikuwa na huruma kwa mawaziri hao na wabunge wa muda mrefu, akiwemo mwanasiasa mkongwe na waziri wa zamani, John Malecela ambaye aliangushwa kwenye kura za maoni za jimbo la Mtera.

  Mbali na kigogo huyo ambaye alianza kuitumikia nchi tangu nchi ilipopata uhuru, wabunge wengine walioanguka ni Joseph Mungai (Mufindi Mashariki), Jackson Makweta (Njombe Kaskazini), Prof Philemon Sarungi (Rorya) na Dk Ibrahim Msabaha (Kibaha Mjini).

  Wengine ambao wameshaanguka ni Bujiku Sakila (Kwimba), William Shelukindo (Bumburi), Raphael Mwalyosi (Ludewa) na Zainab Gama (Kibaha Mjini).

  Wabunge wengine ambao hawajakitumikia chombo hicho kwa muda mrefu, lakini wameanguka kwenye kura za maoni ni Ludovic Mwananzila (Kalambo), Ponsian Nyami (Nkasi Kaskazini), Yono Kevela (Njombe Magharibi), Felix Mrema (Arusha Mjini), Ramadhan Maneno (Chalinze) na George Lubeleje (Mpwapwa).

  Mawaziri walioshindwa vibaya kwenye kura za maoni ni pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Diodorus Kamala, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera (Korogwe Mjini) na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, James Wanyancha.


  Source: Mwananchi.
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  :mad2:
   
 3. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Du twendeni taratibu!!!
   
 4. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  "I, ME AND MYSELF" ndo inawasumbua!
   
 5. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Muda ndo unatubana!! nakubaliana na wewe..........mkuu consultative meetings usiku kucha.........watu hawalali!!!
   
 6. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Zitto kabwe basi atakuwa anafanya kazi kubwa ya kuwashawishi wote waliotema ccm. Hiyo inaleta raha kidogo ingawa ndani yao kuna mamluki watakuwemo
   
 7. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Zitto kabwe anatumika tu yeye mwenyewe ni "unwanted product" huko kuna wenyewe mkuu lazima..utokee kas au ni m-G
   
 8. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2010
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  chadem, chadema, chadema, taratibu eeh,
  huyo bw. nyimbo si alishakuwa upinzani
  akautosa dakika karibu na uchaguzi kisha
  akarudi "nyumbani kwake ccm"? mbona mnakuwa wasahaulifu
  kiasi hiki?

  halafu hizi mbio za watu "wanaosemekana" ni watendaji wa
  "ile ofisi kuu" nyinyi hamshtuki? utasikia mara ooh hawa jamaa
  wanayohistoria ya mageuzi mara ooh wanauchungu na nchi n.k.
  mbona hao jamaa hawakujiunga chadema wakati mwengine na wameamua
  sasa? msije sema hamjaonywa!!!
   
 9. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Kazi ipo this season.
   
 10. M

  MLEKWA Senior Member

  #10
  Aug 16, 2010
  Joined: Aug 18, 2007
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  UKWELI NI HUU KIKWETE KAONYWA NA MWINYI KUWA BAADA YAKUFANYA UCHUNGUZI WA KAMATI YAKE YA MGAWANYIKO KUNDI LA MAFISADI SIO LA KUCHEZEA.
  someni taarifa hii hapa chini
  Are corruption
   
 11. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #11
  Aug 16, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Chadema taratibu maana wengine walishalewa madaraka wasije waklewesha na huku. Ebo
   
 12. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #12
  Aug 16, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Wataharibu chama
   
 13. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #13
  Aug 16, 2010
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  sijui huyu dogo Zitto atakua lini na kuacha kuropoka ovyo, Chegeni kasema bado anatafakari hii pupa na papara ili aoanekana kazi kafanya yeye sio?
   
 14. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #14
  Aug 16, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hivi wanaposema wanajadiliana na mtu ili ahamie chama chao wana maana gani? Wanawaahidi nini ili wahame? Ahadi hizo si rushwa kwa maneno mengine? Na ni nani anawapitisha kugombea ubunge kwa niaba ya chama chao kipya?

  Hicho chama chao kimekuwa timu ya mpira? Lengo ni kushinda kwa njia yeyote hile, to hell with principles. Wanaanza kutia wasiwasi.

  Amandla....
   
 15. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #15
  Aug 16, 2010
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145

  U see now.... yuko wapi Zitto Kabwe na kupayuka kwake ovyo
   
 16. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #16
  Aug 16, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Zitto

  Chegeni

  Ina maana Zitto Kabwe muongo au huyu Chegeni kawageuka CHADEMA baada ya kukubaliana nao ? Either way, this is not a good look.

  Kama alivyosema Fundi Mhundo pale juu na nilivyosema katika posts zilizotangulia, CHADEMA kukumbatia mamluki yeyote anayetoka CCM ni kujionyesha hakina principles, hakijiamini na hakina wagombea wake wenyewe wa kutosha kuweza kuchukua nafasi hizi.
   
 17. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #17
  Aug 16, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,846
  Likes Received: 11,965
  Trophy Points: 280
  Watu wengine jamani mtu umeshasema chama chao, so what is your concern with others party leave them alone to do what they want to do and build yours the way you want it to be.
   
 18. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #18
  Aug 16, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hiki ni chama kinachotaka kipate nafasi ya kutuongoza watanzania wote kwa hiyo mwenendo wake unatuhusu wote. Hiki si chama cha mpira au burudani!

  Amandla.....
   
 19. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #19
  Aug 16, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,477
  Likes Received: 1,214
  Trophy Points: 280
  wana ccm wasafi wakaribishwe chadema ila mafisadi noooooooooooooooooooooo
   
 20. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #20
  Aug 16, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakuu mnalumbana kujadili wanasiasa? Ukishaita mtu mwanasiasa, tegemea lolole, no surprises anymore!
   
Loading...