Waganga wa Kienyeji Mkoani Rukwa: Mkoa wa Rukwa tunaonewa sana huku hakuna Uchawi kama tunavyochafuliwa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,689
109,117
"Yaani ukisema tu unatokea Mkoa wa Rukwa unaanza Kuogopwa na kuhisiwa vibaya. Sisi kama Waganga wa Kienyeji tunasema Watu wa Rukwa siyo Wachawi na ni Watu Wastaarabu mno kuliko Mikoa mingine ambayo ndiyo ina Uchawi mwingi kuliko hapa Kwetu" amesema Mmoja wa Waganga wa Kienyeji aliyewawakilisha Wenzake.

Chanzo: Nipashe ya Radio One Leo.

Nami GENTAMYCINE nawajibu hawa Waganga wa Kienyeji kutoka Mkoa wa Rukwa kuwa kuna Kiongozi Mmoja wa Kiserikali ( sasa ni Marehemu ) ambaye aliwahi kuwa Rafiki wa Familia yangu aliweka Rekodi Kipindi cha Rais Mwinyi baada ya Kulitundika Koti lake la Suti Hewani katika Chumba cha Mikutano na Wakatoka Baru ( Wakakimbia ) mpaka akaenda Kuwatuliza na Kurejea Ukumbini humo.

Na hata Yeye Mwenyewe alikuwa akiogopwa kwa Ulozi ( japo alipendwa kwa Kupeleka Maendeleo kwa Wakazi wa Mkoa na Jimbo lake ) ila Siku aliyofariki wapo Wakazi Wengi wa Mkoa huo wa Rukwa walifurahia wakisema Gwiji Sumbufu Kiuchawi limeondoka.

Kaka yangu Makongoro Nyerere sasa umehamishiwa Mkoa huo wa Rukwa hivyo nakuonya kuwa makini sana na zile Tabia zako Kubwa mbili usizopenda Kuziacha vinginevyo Wazanaki Wenzako tutakupoteza kwa ama Kuondoka mazima au kuwa Chizi Tukuka.
 
Back
Top Bottom