Wafungwa waliomaliza kutumikia vifungo vyao kutumia ujuzi waliupata Gerezani kujitegemea

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Serikali imewataka wafungwa watakaomaliza kutumikia vifungo vyao gerezani kutumia ujuzi waliopata kujitengenezea kipato ili kuepuka kujiingiza tena katika uhalifu.

Maagizo hayo yametolewa Novemba 20, 2023 na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (Mb) Mhe. Jumanne Sagini wakati alipokuwa akihitimisha Ziara yake ya Kikazi katika Gereza la Mahabusu Mugumu Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara.

d647c82a-eac5-45fe-a4e5-19ceab6b3a48.jpeg

07926fd2-70ae-4f1a-a08c-ef620b931c28.jpeg

"Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona watu wake wakipanda kiuchumi ndio maana hapa gerezani sio sehemu ya mateso bali ni sehemu ya mafunzo na tunawapa mafunzo wafungwa ili wakitoka watumie ujuzi huo kujitengenezea kipato". Alisema Sagini

Pia Sagini amelipongeza Jeshi la Magereza kwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo Ufyatuaji tofali, Ushonaji, Uashi, Uchomeleaji vyuma, Uselemala, Ufugaji, kwani miradi hiyo imechochea wafungwa kuwa na ujuzi ambao utawasaidia huko uraini.

c1464830-a40a-462c-845c-80da99fb1510.jpeg

b3a7b5e4-327e-45dc-83f3-f3f942c2d4e2.jpeg
 
Jambo jema magereza sio jehanam ni sehemu ya kukarabati tabia wanaokwenda sio wote wana hatia ukifuatilia kisa cha Abdallah zombe na mfanyabiashara wa madini mtwara utagundua
 
Serikali imewataka wafungwa watakaomaliza kutumikia vifungo vyao gerezani kutumia ujuzi waliopata kujitengenezea kipato ili kuepuka kujiingiza tena katika uhalifu.

Maagizo hayo yametolewa Novemba 20, 2023 na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (Mb) Mhe. Jumanne Sagini wakati alipokuwa akihitimisha Ziara yake ya Kikazi katika Gereza la Mahabusu Mugumu Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara.

"Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona watu wake wakipanda kiuchumi ndio maana hapa gerezani sio sehemu ya mateso bali ni sehemu ya mafunzo na tunawapa mafunzo wafungwa ili wakitoka watumie ujuzi huo kujitengenezea kipato". Alisema Sagini

Pia Sagini amelipongeza Jeshi la Magereza kwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo Ufyatuaji tofali, Ushonaji, Uashi, Uchomeleaji vyuma, Uselemala, Ufugaji, kwani miradi hiyo imechochea wafungwa kuwa na ujuzi ambao utawasaidia huko uraini.

KWA MTAJI GANI? ACHENI KUDHIHAKI WATU

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Hii inapatikana Tanzania zaidi ya kokote kwani hata wanafunzi wanaomaliza Sekondari na Vyuo vikuu wanajitegemea kwa kuwa wamachingas!!
Wawekee rule au kamba hizo tumbo utajua kwa nini ni wao!
 
kama tuna dhamira ya dhati kabisa, mtu anayekaa jela zaidi ya mwaka ananafasi kabisa yakusoma online na kuhitimu degree, masters au hata PHD kabisa.

Hizi magereza zote zingetengewa fungu nakuwa production centres tena ile mass production inayotumia skills na sio ngungwangungwa, hizi magereza ukiziunganisha na kambi za jeshi ambazo unaziequip na technolojia ndani ya miaka kadhaa Taifa litakuwa na skilled labor force kubwa sana.
 
Ningekua rais hao watu wangekua wanatumikia na kuajiriwa katika mashamba ya serikali na kazi nyingine tungekua mbali kama taifa kuliko kumueka ndani kula bure matokeo yake akitoka kazeeka hana chakufanya kapoteza kila kitu anamua kufanya uhalifu tena afie jela tu,,, wachina wanaleta wafungwa wao Africa wajenge miondombinu na majengo na wanalipwa sisi sasa
 
Back
Top Bottom