Serikali yaagiza Wanawake wanaotoka gerezani wapewe mikopo

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
624
934
Serikali Mkoani Mbeya imeziagiza halmashauri zote za mkoa huo kuwaingiza kwenye mkopo wa asilimia 10 wanawake wote wanaomaliza kutumikia vifungo vyao gerezani ili wautumie ujuzi walioupata kuanzisha shughuli za ujasiriamali.

Aidha, imeagiza kuundwa Kamati za Ulinzi na Usalama wa Wanawake na Watoto kwenye kila kata kukabiliana na matukio ya ukatili ambayo makundi hayo yamekuwa yakikabiliana nayo na kuyakwamisha kupata maendeleo.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera, ametoa maagizo hayo kwa kusema kwenye magereza yote wafungwa wanapatiwa mafunzo ya ufundi ambayo yanawasaidia kuwa na ujuzi wa kufanya shughuli za ujasiriamali, hivyo ili kuwaendeleza ni lazima wapewe mikopo.

Aliwataka wakuu wa wilaya na wakurugenzi kusimamia jambo hilo ili litekelezwe katika kila eneo na kwamba litapunguza vitendo vya uhalifu kwenye jamii.

“Hili ni agizo ambalo watendaji wetu wa halmashauri lazima walisimamie kikamilifu. Kwenye magereza yetu kuna vyuo vya ufundi ambavyo vinatoa mafunzo ya ujasiriamali, hivyo naagiza wanawake wote wanaomaliza kutumikia vifungo wapewe mikopo,” alisema Homera.

Pia aliwaomba viongozi wa dini na mila katika mkoa kusaidia kutoa elimu itakayosaidia kupunguza matukio ya watu kuuana kwenye jamii kwa sababu ya wivu wa mapenzi.

Homera alisema kwa sasa katika Mkoa wa Mbeya huo, Jeshi la Polisi limefanya kazi kubwa ya kuzuia matukio hayo kwa kuwakamata watu wote wanaohusika kwenye matukio ya mauaji.

Alisema hivi karibuni walikamatwa watu waliodaiwa kumuua Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwanyanje katika Kata ya Uyole pamoja na waliodaiwa kumuua Ofisa Ustawi wa Jamii wa Gereza la Watoto la Kabwe jijini Mbeya.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Dk. Angelina Lutambi, alisema ofisi yake itaendelea kusimamia sheria ili kuhakikisha halmashauri zote za mkoa zinatoa mikopo ya asilimia 10 kwa makundi maalumu.

Alisema kwa sasa katika mkoa wanawake wamekuwa wakijituma kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo zikiwamo biashara na kazi za kilimo na kwamba kundi hilo ndilo linaloongoza kwa uzalishaji.

Source: Nipashe
 
Ni ukweli usiopingika kwamba kundi hilo ndilo linaloongoza kwa uzalishaji lakini pia kundi hilo ndilo linaloathirika zaidi katika nyanja ya Udhalilishwaji, Kunyanyapaliwa, Kuonewa na Kunyanyaswa. Hatari ninayoiona hapa ni hususan kwa wale wanawake walioolewa.

Endapo kama TAHADHARI hazitachukuliwa mapema (Kabla ya kupewa Mkopo), Uzoefu unaonesha kwamba wapo baadhi ya Wanaume ambao ni wakorofi ambao wanaweza kumlazimisha Mnufaika(Mwanamke/Mke wake) aende kinyume na Malengo ya Mkopo au hata kumlaghai, kumdhulumu/kumnyang'anya/kumpokonya fedha hiyo na kwenda kuitumia tofauti na Kusudio la Mkopo (Wengine huishia kudundwa, kutishiwa endapo wataghairi kutoa fedha hiyo kwa "Mzee" wa boma). Tujifunze Uzoefu kutoka TASAF 1 na TASAF 11.
 
Tatizo kwa wanufaika... Tassaf ipo na mfuko wa maendeleo kwa wanawake, vijana na walemavu upo kila wilaxa...
 
Kwa mantiki hiyo, iwekwe bayana kwamba Wanawake wanaotoka magerezani ni lazima wawezeshwe kuomba Mkopo katika mifuko hiyo na Wapewe kipaumbele cha makusudi katika kupata Mikopo.
 
Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom