OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 419
- 670
Leo nimesoma gazeti la HabariLeo, limeandika
'MKUU wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi ametoa wito kwa Jeshi la Magereza Iringa kuruhusu wafungwa wake kuchimba mitaro ya miradi ya maji inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Iruwasa) ili kupunguza deni la zaidi ya Sh milioni 300 wanazodaiwa na mamlaka hiyo.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Iruwasa, Gilbert Kayange kwa mkuu wa mkoa huyo ililitaja jeshi la Magereza kama moja ya taasisi za serikali ambazo ni wadaiwa sugu wa mamlaka hiyo'
Lakini tuangalie hili swala kiuchumi kwa kuwaangalia watu ambao wako mtaani ambao wanategemea ajira za pangu pakavu, zile za deiwaka.
Hii inamaanisha kuwa, kama Magereza watalipa pesa hizo idara ya maji italazimika kuwaajiri watu wa kuchimba mitaro, na watu hao wakipata hivyo vibarua vya kuchimba mitaro watapata unafuu wa maisha yao,
Lakini kwa hili analotaka muheshimiwa ni kuwa wafungwa wakifanya hizo kazi hakuna pesa itakayoingia kwa raia wa chini ambao hutumia nguvu zao kujiingizia kipato
Swala la wafungwa kufanyakazi limeshajadiliwa sana kwa kuwa lina athiri ajira za walio wengi mtaani, hebu tufikirie wafungwa wakitumika kujenga reli ya mwendo kazi, barabara, nk nk, watu mtaani watapata wapi hela kama sio kuzidi kuongeza idadi ya wafungwa ndani ya Magereza, kwa kuwa tunajua uchumi ukiwa mbaya maovu huongezeka.
Hapa serikali ni muhimu ijitathmini na kuona kuwa, sio sifa kumpeleka hata mwizi wa kuku magereza, au kuwaweka watu mahabusu miezi kibao kuhisi unamkomoa kumbe unaharibu uchumi kwa kuwa serikali inaingia gharama kuwaweka watu hao magereza.
Si busara, serikali nia yake iwe ni kutengeneza pesa na sio kutumia pesa kwa vitu visivyo na tija, hakuna adhabu zinauma kama kutoa pesa, faini na faini ni moja kati ya vyanzo vya mapato ya serikali, nafikiri faini ni kitu kizuri zaidi kuliko kupelekana jela,
Jela inawaumiza watu wetu kisaikolojia na kuharibu nguvu kazi kwa kuwa wanaotoka jela wengi huwa wamekata tamaa ya maisha uraiani, uharibufu wa nguvu kazi na kuathiri uchumi kwa gharama za kuwaweka jela, ni vyema yawepo makosa machache ya watu kustahili kukaa jela na mengine yawe ya kulipa faini watu wabaki mitaani serikali inapata pesa mambo yanakuwa saafi kabisa
Tujitathmini
SIgned.
Oedipus