Wafungwa wakitumika kulipa madeni ya magereza, walioko mtaani wataajiriwa vipi?

OEDIPUS

Senior Member
Oct 12, 2019
177
500
Leo nimesoma gazeti la HabariLeo, limeandika

'MKUU wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi ametoa wito kwa Jeshi la Magereza Iringa kuruhusu wafungwa wake kuchimba mitaro ya miradi ya maji inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Iruwasa) ili kupunguza deni la zaidi ya Sh milioni 300 wanazodaiwa na mamlaka hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Iruwasa, Gilbert Kayange kwa mkuu wa mkoa huyo ililitaja jeshi la Magereza kama moja ya taasisi za serikali ambazo ni wadaiwa sugu wa mamlaka hiyo'


Lakini tuangalie hili swala kiuchumi kwa kuwaangalia watu ambao wako mtaani ambao wanategemea ajira za pangu pakavu, zile za deiwaka.

Hii inamaanisha kuwa, kama Magereza watalipa pesa hizo idara ya maji italazimika kuwaajiri watu wa kuchimba mitaro, na watu hao wakipata hivyo vibarua vya kuchimba mitaro watapata unafuu wa maisha yao,

Lakini kwa hili analotaka muheshimiwa ni kuwa wafungwa wakifanya hizo kazi hakuna pesa itakayoingia kwa raia wa chini ambao hutumia nguvu zao kujiingizia kipato

Swala la wafungwa kufanyakazi limeshajadiliwa sana kwa kuwa lina athiri ajira za walio wengi mtaani, hebu tufikirie wafungwa wakitumika kujenga reli ya mwendo kazi, barabara, nk nk, watu mtaani watapata wapi hela kama sio kuzidi kuongeza idadi ya wafungwa ndani ya Magereza, kwa kuwa tunajua uchumi ukiwa mbaya maovu huongezeka.

Hapa serikali ni muhimu ijitathmini na kuona kuwa, sio sifa kumpeleka hata mwizi wa kuku magereza, au kuwaweka watu mahabusu miezi kibao kuhisi unamkomoa kumbe unaharibu uchumi kwa kuwa serikali inaingia gharama kuwaweka watu hao magereza.

Si busara, serikali nia yake iwe ni kutengeneza pesa na sio kutumia pesa kwa vitu visivyo na tija, hakuna adhabu zinauma kama kutoa pesa, faini na faini ni moja kati ya vyanzo vya mapato ya serikali, nafikiri faini ni kitu kizuri zaidi kuliko kupelekana jela,

Jela inawaumiza watu wetu kisaikolojia na kuharibu nguvu kazi kwa kuwa wanaotoka jela wengi huwa wamekata tamaa ya maisha uraiani, uharibufu wa nguvu kazi na kuathiri uchumi kwa gharama za kuwaweka jela, ni vyema yawepo makosa machache ya watu kustahili kukaa jela na mengine yawe ya kulipa faini watu wabaki mitaani serikali inapata pesa mambo yanakuwa saafi kabisa

Tujitathmini

SIgned.
Oedipus
 

No retreat no surrender

JF-Expert Member
Apr 21, 2018
1,891
2,000
Weeee jamaa vipi? Hivi unafikiri ajira hutolewa kwa kuhurumia watu eti kasababu watu mitaani hawana ajira basi tuajiri? Ajira ni huduma inayotakiwa katika soko kama hiyo huduma inahitajika utaajiriwa kama haihitajiki utaajiri kwasababu hipi?

Kuwajaza watu hela kila mwisho wa mwezi wakati chakufanya hakuna ndo nini? "No demand no supply". Kama hakuna huitaji wa kuajiri unaajiri ili iweje? Wafungwa huko magerezani wanatumia huduma ambazo zinalipiwa! Sasa wasifanye kazi alafu maji yakatwe wewe ndo utaenda kuwachotea maji? Thinking capacity ni zero!
 

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
12,977
2,000
Wakikosa ajira watafanya uhalifu watafungwa na kuja kuchimba mtaro yaani mbili jumlisha mbili sawa na mbili mara mbili, simple
 

abou

JF-Expert Member
Mar 4, 2011
209
250
Weeee jamaa vipi? Hivi unafikiri ajira hutolewa kwa kuhurumia watu heti kasababu watu mitaani hawana ajira basi tuajiri? Ajira ni huduma inayotakiwa katika soko kama hiyo huduma inahitajika utaajiriwa kama haihitajiki utaajiri kwasababu hipi? Kuwajaza watu hela kila mwisho wa mwezi wakati chakufanya hakuna ndo nini? "No demand no supply". Kama hakuna huitaji wa kuajiri unaajiri ili iweje? Wafungwa huko magerezani wanatumia huduma ambazo zinalipiwa! Sasa wasifanye kazi alafu maji yakatwe wewe ndo utaenda kuwachotea maji? Thinking capacity ni zero!
Mkuu hata huko shule ulikuwa ukiandika hivi hivi? Au ni vile mleta mada amekuudhi??

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
12,311
2,000
Weeee jamaa vipi? Hivi unafikiri ajira hutolewa kwa kuhurumia watu heti kasababu watu mitaani hawana ajira basi tuajiri? Ajira ni huduma inayotakiwa katika soko kama hiyo huduma inahitajika utaajiriwa kama haihitajiki utaajiri kwasababu hipi? Kuwajaza watu hela kila mwisho wa mwezi wakati chakufanya hakuna ndo nini? "No demand no supply". Kama hakuna huitaji wa kuajiri unaajiri ili iweje? Wafungwa huko magerezani wanatumia huduma ambazo zinalipiwa! Sasa wasifanye kazi alafu maji yakatwe wewe ndo utaenda kuwachotea maji? Thinking capacity ni zero!
hujamuelewa mleta mada,

Mfano mdogo.
Una Ndugu zako wakiume wawili na wakike wawili wamejazana hapo Nyumbani kwako na wewe ndio mkubwa,

Unaghalamia kula yao, vaa yao na kila kitu kiusucho pesa wanakutegemea wewe kiasi kwamba mpaka unazidiwa na kumuomba Mungu akupunguzie huo mzigo mzito,

Ndugu zako hao wananguvu za kutosha na wana hali ya kufanya kazi siyo wavivu, lakini imetokea kila wanapoenda kuomba kazi mfano,
Kwenye ujenzi wa SGR, wanakuta wamejazana wafungwa,
Wanaenda manispaa walau wapate kazi za ufagizi wanakuta wafungwa,
Wanaenda Tanesco nako wanakuta wafungwa ndio wafanyakazi,
Hawakati Tamaa wanaenda Duwasa wapate ata kuchimba mitaro nako wapate kitu nako wanakuta wafungwa,

Wanaenda kwenye kampuni za ujenzi wa majengo ya serikari nako wanakuta wafungwa ndio wanaofanya kazi huko.

Unafikiri hao wadogo zako watapata wapi kazi ili wakupunguzie wewe majukumu.

Hao wadogo zako wa kiume itafikia kipindi nao watachoka kukaa na kukutegemea wewe watataka wajitegemee, wakiangalia upande wa pili chaneli hazisomeki ndio hapo utasikia mdogo wako mkubwa kakamatwa Garisa akiwa na ma al shababi wakifanya shambulizi,

Mdogo wako ulieona ndie mwenye uelekeo kidogo unasikia Kachomwa moto kariakoo alipotaka kumpora kibegi mama ambae ni mpita Njia,

Ukija kwa hao dada zako wa kike, yule mtulivu na ambae ulitegemea kitu toka kwake unasikia ameanza kupanga foreni pale Manzese Darajani akijuza utajisikiaje,

Ukija kwa huyo wa pili, Asubuhi unaamka unafungua data upate update yaliyojiri mtandaoni unakutana na Video ya huyo dada yako mdogo Akiliwa Ndogo na jamaa kwa makubaliano ya kupewa kiasi kadhaa cha pesa,

Utajisikiaje.?

Ajira Ajira Ajira Trump siyo mpumbavu kuweka Sera za kupanua ongezeko la Ajira katika Nchi yake.


Cc zero IQ

Sent using Jamii Forums mobile app
 

OEDIPUS

Senior Member
Oct 12, 2019
177
500
Ila wafungwa wanapaswa wajitosheleze kwa kuzalisha pia
Nadhani nimeshauri pale

Serikali iwe na nia ya kukusanya mapato, watu wapigwe faini, viboko kiasi, makosa machache ndio yawe ya kwenda jela.

Gharama za kumuweka mtu mahabusu ni kubwa nimesema pale hata ucheleweshaji wa kesi mtu akiwa mahabusu ni hasara kwa serikali,

Sasa hatuna haja ya kuwa na mifumo kwa sababu ya kurith ila tuangalie tija
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom