Wafugaji Wilaya ya Mvomero wahamishia Minada yote Wilaya ya Kilosa

blackberry m

JF-Expert Member
Apr 16, 2012
563
413
WAFUGAJI wa wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wameamua kuhamishia minada ya mifugo katika wilaya zilizo karibu na wilaya hiyo kutokana na sintofahamu iliyoibuka hivi karibuni.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti, wafugaji hao walieleza kuwa wamekuwa wakinyanyaswa na Mkuu wa Wilaya ambaye ameletwa wilayani humo hivi karibuni.

"Mkuu wa wilaya huyu mpya ambaye ameletwa hivi karibuni, amekuwa chanzo kikuu cha mgogoro baina yake na wafugaji kwani alianza kukamata wafugaji hovyo na kuwapa kesi za uchochezi pasipo hatia. Alikamata wafugaji wapatao 20 na kisha kuwapa kesi hizo za kubambika na baada ya hapo wakahukumiwa vifungo vya nje vya mwaka mmoja mmoja,"

"Baada ya hapo akawatisha kuwa wakifanya makosa yoyote yale, basi hakutokuwa na mjadala bali ni kwenda magereza moja kwa moja. Wale wote waliofungwa vifungo hivyo, hawakuwahi kupatiwa nakala za hukumu zao licha ya wao kutaka kupatiwa nakala hizo" alisema mmoja wa wafugaji hao.

Kutokana na hatua hiyo ya DC huyo, viongozi wa wafugaji waliamua kukaa kikao cha pamoja kwa wilaya yote na kufikia uamuzi wa kuhamishia minada yote ya mifugo kwa wilaya za Kilosa na Kilindi ambazo zimepakana na Mvomero.

"Baada ya kuona kuwa tunanyanyasika kwa kiasi cha kutisha, tumeamua kwa pamoja kuhamishia minada yote ya mifugo kwa wilaya hizo za Kilosa na Kilindi ili kuepuka kuwachangia mapato watesi wetu,"

"Hatuwezi kumpa mapato mtu anayetukamata na kutuhukumu kwa kesi zisizo na mbele wala nyuma. Huwezi ukashinikiza zitolewe hukumu kwa kesi ambazo hazina ushahidi wala msingi wowote halafu wakati huo huo ukusanye mapato kutokana na mifugo ya wale unaowanyanyasa" alisema mmoja wa wafugaji aliyehukumiwa kifungo cha nje cha mwaka mmoja.

Wafugaji hao wametoa wito wao kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutupia jicho wilaya hiyo kwani wananyanyaswa na DC huyo.
 
Back
Top Bottom