JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,309
- 5,464
Baraza hilo limetoa azimio hilo katika kikao cha dharura kilichofanyika mkoani Morogoro kutokana na kuwepo kwa changamoto kwa Wanachama wake wakiwa kazini.
Katibu Mkuu wa TRAWU Taifa, Raphael Kazyoba amesema “Rasimu inatakiwa ifanyiwe kazi haraka, wasipofanyia kazi tutatangaza mgogoro kwa maslahi mapana ya Wafanyakazi na Shirika la Reli kwa ujumla wake.”
Naye, Jacob Shindika ambaye ni Mwenyekiti wa TRAWU Taifa amesema “Kuna daraja ambalo Mtumishi wa TRC anaweza kufanyakazi kwa miaka 40 akaja kulipwa Tsh Milioni Moja anapostaafu lakini tunapokuwa na mkataba wa Hali Bora mambo kama hayo yanafafanuliwa na inawasaidia Wafanyakazi.
Chanzo: Azam TV