KERO Wafanyakazi wa Manispaa ya Ubungo hapo Luguruni wajitathimini, baadhi wanatengeneza mazingira ya Rushwa

KERO Wafanyakazi wa Manispaa ya Ubungo hapo Luguruni wajitathimini, baadhi wanatengeneza mazingira ya Rushwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mhanga pia wa hao Manispaa ya Ubungo, ninaishi Kibamba, mwanzoni mwa Januari 2026 walipita wakikagua Leseni ya Biashara nikawaeleza week inayofuatia nitaenda ofisini, maana ilikuwa ni ya ku-renew na kweli nilienda tarehe 6 January nikahudumiwa na mdada mmoja baada ya kumaliza kunihudumia akasema nimpatie hela ya soda ili alishughulikie.

Jambo langu nipate control number, nilikuwa na Sh elfu 2 nikampatia, mpaka mwezi wa pili mwishoni sijaipata control number, ikabidi nimpigie akasema ananiangalizia, baadaye akanipigia anasema ime-expire natakiwa niombe upya.

Nikamuuliza ita-expire vipi na mimi sijaipata na wakati tunaomba niliweka namba zangu za simu? Akanijibu short kuwa hajui ni kwanini ila akasema nimtumie Sh 20,000 anitumie hiyo control number.

Nikamwambia nitaenda mwenyewe ofisini hiyo hela sina, alikata simu na hajawahi nitumia hiyo control number.

Mamlaka inayohusika na Wafanyakazi wa Manispaa ya Ubungo hapo Luguruni watusaidie wananchi tunapitia mengi bila rushwa hatupati huduma.
 
Back
Top Bottom