Wafanyakazi wa G4S tuliohamishiwa Zanzibar tunaomba ofisi ihamishie michango yetu ya Hifadhi ya Jamii NSSF kutoka ZSSF

Wavisiwani

Member
Feb 8, 2022
13
28
Sisi ni wa wafanyakazi tuliohamishiwa Zanzibar toka Bara kwa ajili ya kufanya kazi za ulinzi kwa miaka na siku tofauti.

Tulipohamishiwa hapa visiwani kampuni yetu ya G4S ilitupatia mishahara yetu na kutuma michango yetu ya mifuko ya hifadhi ya jamii kama ada katika mifuko yetu ya hifadhi za jamii tuliyokuwa wanachama.

Lakini tangu oktoba 2017 kampuni ilisitisha kutuma michango yetu kama kawaida kwa madai hawakujua ni wapi wapeleke michango hiyo kati ya ZSSF ama mifuko ya awali. Pia tulielezwa na uongozi kuwa fedha zetu zilikuwa salama kwani zilihifadhiwa katika akaunti ya dharura ila benki yenyewe ilipokuwa akaunti hatukujulishwa.

Tangu hapo tuliendelea kuahidiwa tu bila muafaka wowote na mwishowe kampuni yetu G4S walituma barua kuomba ufafanuzi juu ya suala hilo toka ZSSF na wakaombwa na ZSSF watume majina yetu, akaunti zetu za Mifuko ya awali na kumbukumbu za michango ya nyuma ndipo ZSSF iliiagiza kampuni yetu kupeleka michango yetu kwenye mifuko yetu kwani ajira zetu hazikuanzia Zanzibar bali tulihamishiwa huku tu kikazi na tulikuwa wanachama wa mifuko mingine.

Hiyo ilikuwa novemba 2019 lakini badala ya kufanya hivyo kampuni iliipeleka hiyo michango ZSSF kinyume cha maelekezo ya ZSSF. Sisi tunashangaa ni kwanini walifanya hivyo!? Baada ya kuulalamikia uongozi wetu mwishowe fedha zetu za michango zinapelekwa NSSF ambako sisi ni wanachama na kwa miezi kumi sasa wamekuwa wakituwekea michango yatu.

Shida yetu ni hizo fedha za miaka mitatu ambazo ziko ZSSF kimakosa na wala sisi si wanachama.

Tunaiomba kampuni yetu na mfuko wa ZSSF waturejeshee fedha zetu kwenye mfuko wetu wa NSSF kwani wanakaa nao bila sababu ya msingi kwa sasa na ni fedha haramu kwao.

Ni sisi waathirika,

G4S Zanzibar.
 
Mnapatikana Zanzibar wapi tuwape msaada wa kisheria.
 
Hilo jambo ni kero nzito, kinachosikitisha wanasiasa wapo kimya hawalipiganii. Kwa nini SMZ ikwapue fedha za watu wasio wazanzibari? ni wizi tu
 
Pwani mchangani Neptune hotel

Mkuu unaweza kuyaeleza malalamiko yenu kwa mpangilio halafu tukajaribu kuyafikisha kwa wanasiasa alau wajaribu kukemea, pengine inaweza kusaidia kuanzisha vuga vugu. Nitajarbu kuwafikishia watu ambao wanaweza kuyasogeza mbele yakasemewa.
 
Sisi ni wa wafanyakazi tuliohamishiwa Zanzibar toka Bara kwa ajili ya kufanya kazi za ulinzi kwa miaka na siku tofauti.

Tulipohamishiwa hapa visiwani kampuni yetu ya G4S ilitupatia mishahara yetu na kutuma michango yetu ya mifuko ya hifadhi ya jamii kama ada katika mifuko yetu ya hifadhi za jamii tuliyokuwa wanachama.

Lakini tangu oktoba 2017 kampuni ilisitisha kutuma michango yetu kama kawaida kwa madai hawakujua ni wapi wapeleke michango hiyo kati ya ZSSF ama mifuko ya awali. Pia tulielezwa na uongozi kuwa fedha zetu zilikuwa salama kwani zilihifadhiwa katika akaunti ya dharura ila benki yenyewe ilipokuwa akaunti hatukujulishwa.

Tangu hapo tuliendelea kuahidiwa tu bila muafaka wowote na mwishowe kampuni yetu G4S walituma barua kuomba ufafanuzi juu ya suala hilo toka ZSSF na wakaombwa na ZSSF watume majina yetu, akaunti zetu za Mifuko ya awali na kumbukumbu za michango ya nyuma ndipo ZSSF iliiagiza kampuni yetu kupeleka michango yetu kwenye mifuko yetu kwani ajira zetu hazikuanzia Zanzibar bali tulihamishiwa huku tu kikazi na tulikuwa wanachama wa mifuko mingine.

Hiyo ilikuwa novemba 2019 lakini badala ya kufanya hivyo kampuni iliipeleka hiyo michango ZSSF kinyume cha maelekezo ya ZSSF. Sisi tunashangaa ni kwanini walifanya hivyo!? Baada ya kuulalamikia uongozi wetu mwishowe fedha zetu za michango zinapelekwa NSSF ambako sisi ni wanachama na kwa miezi kumi sasa wamekuwa wakituwekea michango yatu.

Shida yetu ni hizo fedha za miaka mitatu ambazo ziko ZSSF kimakosa na wala sisi si wanachama.

Tunaiomba kampuni yetu na mfuko wa ZSSF waturejeshee fedha zetu kwenye mfuko wetu wa NSSF kwani wanakaa nao bila sababu ya msingi kwa sasa na ni fedha haramu kwao.

Ni sisi waathirika,

G4S Zanzibar.
Huu ni uonevu unaofanywa na serikali ya SMZ, kwann wachukue hizo fedha wakat sio zao? Wamezoea kuwadhulumu wafanyakazi wa ma hotelini naona wamenogewa Sasa.
Serikali ya Tanganyika inatakiwa kuingilia kati hili swali.
 
Serekali ya Tanganyika haijawahi kuwajali raia wake.
 
Back
Top Bottom