Wafanyakazi 3,600 wa Muhimbili kupewa elimu ya fedha kabla ya kukopa au kuwekeza

DodomaTZ

Member
May 20, 2022
71
107
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imekubali ombi la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH-Upanga & Mloganzila) la kutoa elimu kwa wafanyakazi wake 3,600 juu ya masuala ya kifedha, fursa mbalimbali zilizopo na vihatarishi vyake ili waweze kuchukua hatua stahiki kabla ya kukopa au kuwekeza.

Ahadi hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi (Maalum) kutoka NBC Makao Makuu, Bi. Ashura Waziri alipomtembelea Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Mohamed Janabi ili kujadiliana naye kuhusu masuala mbalimbali na fursa za ushirikiano.
43f5bd04-2e8f-4c13-a319-9e7f571693cd.jpg

Bi. Ashura Waziri, Mkuu wa Kitengo Wateja Binafsi (Maalumu) NBC na Prof. Mohamed Janabi, Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa MUHIMBILI​

Kwa upande wake Prof. Janabi amesema, pamoja na mambo mengine, ameiomba Benki hiyo kusaidia kutoa elimu kwa wafanyakazi kuhusu masuala ya kifedha ili kuwaepusha na msongo wa mawazo pale ambapo mategemeo yao yanaenda kinyume na matarajio baada ya kukopa au kuwekeza.

“Ningependa kuona wafanyakazi wakikopa mahali sahihi, kwa utaratibu sahihi na kujiepusha na mikopo ya haraka haraka kwani baadhi yao inawaletea changamoto kubwa pale wanaposhindwa kulipa kwa wakati, kupata msongo wa mawazo na kushindwa kutimiza majukumu yao kikamilifu” amesisitiza Prof. Janabi.
 
Back
Top Bottom