Wafanyabiashara wanaonunua mizigo kwa kupewa risiti zenye kodi ya VAT wana sababu ipi ya kukwepa kodi kwa kuuza bidhaa bila kutoa risiti ya VAT?

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
kwa wanaonunua mizigo bila kodi ya vat 18% naweza kuwaelewa kwamba wapo kundi moja na wale wa magendo, ila hawa wanaonunua mizigo yenye vat inakuwaje sasa.

Mfano mfanyabiashara kaenda kufunga mzigo flani, huo mzigo alionunua ni mkubwa na kafaidika kwa punguzo la bei ya jumla, akipiga hesabu ya bidhaa moja moja ni takribani shilingi elf 20,.... kwa hii bei ina maana kwamba kwenye risiti ya tra kwa hizo bidhaa za elf 20 kalipia kodi ya vat asilimia 18% sawa na 3,050.

akienda kuuza kwa reja reja hizo bidhaa anaweza kuuza kwa shilingi elf 25,000, akiuza kwa kutoa risiti ni kwamba ndani ya hio bei kuna hela yake shilingi 21,186 pamoja na kodi ya vat anayolipia mteja shilingi 3,814, ndani ya hii kodi ya vat mfanyabiahara atajilipa mwenyewe ile kodi ya shilingi 3,050 aliyolipa wakati anafunga mzigo, wao TRA watachomdai ni ile kodi iliyozidi ukiachana na ile aliyojifidia 3,814 - 3,050 = 764

hata auze kwa faida ya jero bado atajilipa vat aliyolipia wakati ananunua mzigo

unakomboa hela ya kununua mzigo + faida + unafidia vat uliyolipa mwanzo ...

Ni kipi hasa kinawafanya wafanyabiashara kukwepa kukomboa kodi walizolipa na kujiingiza kwenye matatizo ya kupigwa faini nzito, kufungiwa account, kupelekwa mahakamani, n.k.
 
Iko hivi!
A)Kwa mtu anayetoa efd receipts
Manunuzi ya 10,000,000
Mauzo 12,000,000
B) Kwa asiyetoa efd receipts kisawasawa
Manununuzi 10,000,000
Mauzo 12,000,000 au 11,000,000
Mwisho wa mwaka Efd sales zitasoma labda 5,000,0000
Tafsiri yake: Huyu anachokwepa ni Kodi ya mapato (PIT/CIT) kuja kuwa kubwa na sio VAT Kodi.
Kiujanja atakuwa anarekodi mamunuzi yawe chini au 4,000,000 i.e manunuzi mengine hatarekodi.

Nini kifanyike kwa TRA/Mwigulu?
Efd machine zisiweze kutoa risiti bila kuweka TIN ya mnunuzi.
Wafanyabiashara wanashusha manunuzi pale wanapokuwa hawatoi efd receipts.
Sasa ikiwa manunuzi hayafichiki mark up itumike kufikia mauzo tarajiwa.
 
Kiufupi tu kodi za TRA nazo ni kizungungumkuti.

Na ukiwaendekeza, unaweza kujikuta unawafanyia wao hiyo biashara. Hivyo wakati mwingine ujanja ujanja wa kukwepa kodi, haukwepeki.
 
Back
Top Bottom