Wafanyabiashara Arusha wafunga Maduka ,waandamana ,kisa Machinga

Wafanyabiashara Arusha wafunga Maduka ,waandamana ,kisa Machinga

Mpuuzi ni mpuuzi hata wakitengenewa maeneo yao ya biashara bado kuna wapuuzi watalalama kuwa hawajatendewa haki maadam tu JIWE achukiwe.
 
Mbona hii game simple, nipo Mtwara nimeamua kupanga 3/4 ya bidhaa zangu nje ya duka, nawalipa wamachinga kwa siku wananiuzia bila EFD wala shangazi yake EFD. Maana yake 1/4 ya bidhaa zilizobaki zipo ndani kushikilia frame tu. Na ukija kama sikujui ukiuliza bidhaa nakuambia sina, hata kama unaona ipo! Mpo hapo?
Hii inaitwa kumkoma nyani giladi, safi sana mkuu hakuna namna.
 
Mbona hii game simple, nipo Mtwara nimeamua kupanga 3/4 ya bidhaa zangu nje ya duka, nawalipa wamachinga kwa siku wananiuzia bila EFD wala shangazi yake EFD. Maana yake 1/4 ya bidhaa zilizobaki zipo ndani kushikilia frame tu. Na ukija kama sikujui ukiuliza bidhaa nakuambia sina, hata kama unaona ipo! Mpo hapo?
Duuuh kwel binadam wana akili Sana, huwezi pambana nao
 
Kwa arusha nilitegemea hili kutokea!tena limechelewa sana!! Bado na sisi watembea kwa miguu tutaandamana kupinga wamachinga kuziba barabara na kutuzuwia kupita!tukimaliza sisi na waendesha magari nao watakuwa njiani kuandamana!! Arusha imekuwa kituko kabisa jamani! Pale kilombero stand ndio hakufai hata,maana wamama wauza mboga wamejaa,wauza mitumba ni kama wote,wauza mitishamba ni wakutosha,matunda ndio usiseme,eneo dogo linalobaki ndilo wanaloshea daladala na masheikh wanaofanya mihadhara yao kila kukicha!pembeni kule kuna manabii na maspika yao wanahubiri umuhimu wa sadaka!! Juzi kati Mwenge nao ulikuwa pale,wakazuia hiace zisikae upande ule,leo TCRA na Nida wamechukua eneo lote la juu wameweka mahema yao wanasajili simu! Wauza viwanja wa Kambele nao wamekita gari lao la matangazo humo humo!! Kha! Yaani ni vurugu tupu mazee!! Kuna roho mbaya imewekezwa arusha aisee! Pale friends corner napo jioni hapapitiki! Ni mishikaki,kuku wabichi,samaki,maparachichi,daladala,na mazaga yote!! Acheni tu tuandamane wakuu!
 
Mmmmh! Ila kwa hili mheshimiwa rais kuwaruhusu wafanyabiashara, imeleta usumbufu sana. Yaani kama huku Mwanza wamepanga biashara hadi sehemu za watembea kwa miguu.
Pia kuna sehemu karibia na soko kuu yaani wanaziba hadi njia za kuingia ndani ya soko kuu!!!
Ni kweli alikuwa na nia njema ya kuhakikisha vijana wa raia wote wanajengewa uwezo lakini uwiiiiiii, imekuwa holela holela hata sura ya miji imeharibika.
 
Hahaha yaani uko sahihi. .taifa ripo kwenye raiti track
Wakiichagua tena kira machinga tutampa stigrajoji yake, pia tutawaruhusu wapange bidhaa zao kwenye standadi geji.
 
Heri yako mkuu lakini sio bidhaa zote unaweza kuuza nje ya duka. Mfano vitu kama simu ni ngumu kumuuzia mtu ukiwa umezipanga nje. Sasa kama duka lako la simu limebanwa hamna access ya wateja unakua huna ujanja labda ubadilishe biashara au kuhama eneo.

Back
Top Bottom