Wafanyabiashara Arusha wafunga Maduka ,waandamana ,kisa Machinga

Wafanyabiashara Arusha wafunga Maduka ,waandamana ,kisa Machinga

Mbona hii game simple, nipo Mtwara nimeamua kupanga 3/4 ya bidhaa zangu nje ya duka, nawalipa wamachinga kwa siku wananiuzia bila EFD wala shangazi yake EFD. Maana yake 1/4 ya bidhaa zilizobaki zipo ndani kushikilia frame tu. Na ukija kama sikujui ukiuliza bidhaa nakuambia sina, hata kama unaona ipo! Mpo hapo?
Bora ulichofanya kuliko kukaa kulialia kila siku
 
Machinga ni shida,kule makoroboi mhindi hana hamu nao
Mmmmh! Ila kwa hili mheshimiwa rais kuwaruhusu wafanyabiashara, imeleta usumbufu sana. Yaani kama huku Mwanza wamepanga biashara hadi sehemu za watembea kwa miguu.
Pia kuna sehemu karibia na soko kuu yaani wanaziba hadi njia za kuingia ndani ya soko kuu!!!
Ni kweli alikuwa na nia njema ya kuhakikisha vijana wa raia wote wanajengewa uwezo lakini uwiiiiiii, imekuwa holela holela hata sura ya miji imeharibika.
 
Machinga ni shida,kule makoroboi mhindi hana hamu nao
Hata barabara ya Nyerere kutokea pale kwenye mataa ya makutano ya barabara ya posta, stesheni na Nkurumah uwiiii!!!
Wamenikera wameziba hadi lile duka la pombe za Jumla pale karibu na S.H. Amon na dula la dawa la Makalwesi, yaani nikitaka kununua Robertson napata shida hadi kuingia dukani 🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄
 
Mda mwingine inaboa ww unalipa kodi laki3 au 5 mpaka milion kwa mwezi unalipa lesen manispaa unalipa TRA kwa mwaka tuseme laki 4 au 5 mpaka milion bado mlinzi, umeme, taka, nk ila anaelipa elf20 anapanga biashara mbele ya duka lako anakuziba hata biashara yaki haioneknani tena huu sio uungwana hata kiduku kitaleta kuchukiana tu cha msingi na cha secondary watafutiwe maeneo ya kuifanyia biashara zao wasilete bugudha kwa wenzao.
Sasa hivi unakuta mtu amechukua fremu jirani na wewe amefungua kasupamarket analipa 20,000/=huku akijidai mtaji wake mdogo ,lakini kodi ya fremu analipa kama wewe anakwepa tra,anakwepa leseni ya biashara na tozo nyingine kwa kisingizio cha 20,000/=je huyu anayefanya biashara inayofanana na yako we unakadiriwa na tra yeye anaweka 20,000/=mtalingana kweli na ama kweli hao ni NYARA.
 
Mpuuzi ni mpuuzi hata wakitengenewa maeneo yao ya biashara bado kuna wapuuzi watalalama kuwa hawajatendewa haki maadam tu JIWE achukiwe.
Wewe ni mbwa wa jalala la Tandale.
 
Mbona hii game simple, nipo Mtwara nimeamua kupanga 3/4 ya bidhaa zangu nje ya duka, nawalipa wamachinga kwa siku wananiuzia bila EFD wala shangazi yake EFD. Maana yake 1/4 ya bidhaa zilizobaki zipo ndani kushikilia frame tu. Na ukija kama sikujui ukiuliza bidhaa nakuambia sina, hata kama unaona ipo! Mpo hapo?
Kwa io machinga umewalipia 20,000 kila mmoja?
 
Mbona hii game simple, nipo Mtwara nimeamua kupanga 3/4 ya bidhaa zangu nje ya duka, nawalipa wamachinga kwa siku wananiuzia bila EFD wala shangazi yake EFD. Maana yake 1/4 ya bidhaa zilizobaki zipo ndani kushikilia frame tu. Na ukija kama sikujui ukiuliza bidhaa nakuambia sina, hata kama unaona ipo! Mpo hapo?
Wenye maduka fuateni huu ushauri
 
Sioni sababu ya wao kufunga maduka maana hata kariakoo wamachinga wapo mbele ya maduka miaka nenda rudi.
 
Mbona hii game simple, nipo Mtwara nimeamua kupanga 3/4 ya bidhaa zangu nje ya duka, nawalipa wamachinga kwa siku wananiuzia bila EFD wala shangazi yake EFD. Maana yake 1/4 ya bidhaa zilizobaki zipo ndani kushikilia frame tu. Na ukija kama sikujui ukiuliza bidhaa nakuambia sina, hata kama unaona ipo! Mpo hapo?
Genius
 
Kwa arusha nilitegemea hili kutokea!tena limechelewa sana!! Bado na sisi watembea kwa miguu tutaandamana kupinga wamachinga kuziba barabara na kutuzuwia kupita!tukimaliza sisi na waendesha magari nao watakuwa njiani kuandamana!! Arusha imekuwa kituko kabisa jamani! Pale kilombero stand ndio hakufai hata,maana wamama wauza mboga wamejaa,wauza mitumba ni kama wote,wauza mitishamba ni wakutosha,matunda ndio usiseme,eneo dogo linalobaki ndilo wanaloshea daladala na masheikh wanaofanya mihadhara yao kila kukicha!pembeni kule kuna manabii na maspika yao wanahubiri umuhimu wa sadaka!! Juzi kati Mwenge nao ulikuwa pale,wakazuia hiace zisikae upande ule,leo TCRA na Nida wamechukua eneo lote la juu wameweka mahema yao wanasajili simu! Wauza viwanja wa Kambele nao wamekita gari lao la matangazo humo humo!! Kha! Yaani ni vurugu tupu mazee!! Kuna roho mbaya imewekezwa arusha aisee! Pale friends corner napo jioni hapapitiki! Ni mishikaki,kuku wabichi,samaki,maparachichi,daladala,na mazaga yote!! Acheni tu tuandamane wakuu!

Bwahaaaaa bwahaaa, nimecheka sana hiyo eti wanahubiri umuhimu wa sadaka. Kwa hiyo hapo stand mmejazana vibaya sana. Nadhani hiyo inaitwa tupendane.
 
Wanaolipia kodi za maduka na za serikali wanauza bei juu, wale wanaopanga chini wanauza bei rahisi maana hawana gharama za kodi, sasa mteja ananunua za kupanga chini, na wao wapo kwa tamko la Rais la vitambulisho vya ujasiria mali
 
Wamejazana vibaya halafu wakali hao ukiteleza ukakanyaga bidhaa zao walizotegesha njiani

Back
Top Bottom