Kwa arusha nilitegemea hili kutokea!tena limechelewa sana!! Bado na sisi watembea kwa miguu tutaandamana kupinga wamachinga kuziba barabara na kutuzuwia kupita!tukimaliza sisi na waendesha magari nao watakuwa njiani kuandamana!! Arusha imekuwa kituko kabisa jamani! Pale kilombero stand ndio hakufai hata,maana wamama wauza mboga wamejaa,wauza mitumba ni kama wote,wauza mitishamba ni wakutosha,matunda ndio usiseme,eneo dogo linalobaki ndilo wanaloshea daladala na masheikh wanaofanya mihadhara yao kila kukicha!pembeni kule kuna manabii na maspika yao wanahubiri umuhimu wa sadaka!! Juzi kati Mwenge nao ulikuwa pale,wakazuia hiace zisikae upande ule,leo TCRA na Nida wamechukua eneo lote la juu wameweka mahema yao wanasajili simu! Wauza viwanja wa Kambele nao wamekita gari lao la matangazo humo humo!! Kha! Yaani ni vurugu tupu mazee!! Kuna roho mbaya imewekezwa arusha aisee! Pale friends corner napo jioni hapapitiki! Ni mishikaki,kuku wabichi,samaki,maparachichi,daladala,na mazaga yote!! Acheni tu tuandamane wakuu!