Wafanyabiashara Arusha wafunga Maduka ,waandamana ,kisa Machinga

Wafanyabiashara Arusha wafunga Maduka ,waandamana ,kisa Machinga

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
757
Reaction score
1,822
Mamia ya wafanyabiashara wa Maduka katika eneo la Ranger Safari,jijini Arusha wamefunga maduka yao na kuandamana ofisi ya Mkurugenzi wa jiji la Arusha kushinikiza kuondolewa kwa Machinga wanaopanga biashara mbele ya Maduka yao na kupelekea wao kukosa biashara.

Wakizungumza baada ya kujikusanya mbele ya Maduka yao ,wafabiashara hao wamesema kimsingi hawawachukii Machinga kufanyabiashara lakini wamekerwa na hatua ya Machinga kupanga biashara mbele ya Maduka yao na kusababisha msongamano mkubwa wa watu na magari kiasi cha Barabara kutopitika kirahisi.

"Sisi tunalipa kodi ya TRA ,tunalipa Jiji pamoja na malipo mengine mengi kwa hatua ya Machinga kupanga biashara zao mbele ya Maduka yetu kunasababisha sisi kukosa Wateja "

Wamedai pindi wanapowahoji Machinga hao kuhusu kupanga biashara zao mbele ya Maduka ya wanadai wao ni NYARA za serikali hawaguswi .

IMG_20190621_084423.jpeg
IMG_20190621_085957.jpeg
IMG_20190621_084412.jpeg
IMG_20190621_090004.jpeg
 
Mbona hii game simple, nipo Mtwara nimeamua kupanga 3/4 ya bidhaa zangu nje ya duka, nawalipa wamachinga kwa siku wananiuzia bila EFD wala shangazi yake EFD. Maana yake 1/4 ya bidhaa zilizobaki zipo ndani kushikilia frame tu. Na ukija kama sikujui ukiuliza bidhaa nakuambia sina, hata kama unaona ipo! Mpo hapo?
Mamia ya wafanyabiashara wa Maduka katika eneo la Ranger Safari,jijini Arusha wamefunga maduka yao na kuandamana ofisi ya Mkurugenzi wa jiji la Arusha kushinikiza kuondolewa kwa Machinga wanaopanga biashara mbele ya Maduka yao na kupelekea wao kukosa biashara.

Wakizungumza baada ya kujikusanya mbele ya Maduka yao ,wafabiashara hao wamesema kimsingi hawawachukii Machinga kufanyabiashara lakini wamekerwa na hatua ya Machinga kupanga biashara mbele ya Maduka yao na kusababisha msongamano mkubwa wa watu na magari kiasi cha Barabara kutopitika kirahisi.

"Sisi tunalipa kodi ya TRA ,tunalipa Jiji pamoja na malipo mengine mengi kwa hatua ya Machinga kupanga biashara zao mbele ya Maduka yetu kunasababisha sisi kukosa Wateja "

Wamedai pindi wanapowahoji Machinga hao kuhusu kupanga biashara zao mbele ya Maduka ya wanadai wao ni NYARA za serikali hawaguswi .

View attachment 1133208View attachment 1133210View attachment 1133212View attachment 1133214
 
Mda mwingine inaboa ww unalipa kodi laki3 au 5 mpaka milion kwa mwezi unalipa lesen manispaa unalipa TRA kwa mwaka tuseme laki 4 au 5 mpaka milion bado mlinzi, umeme, taka, nk ila anaelipa elf20 anapanga biashara mbele ya duka lako anakuziba hata biashara yaki haioneknani tena huu sio uungwana hata kiduku kitaleta kuchukiana tu cha msingi na cha secondary watafutiwe maeneo ya kuifanyia biashara zao wasilete bugudha kwa wenzao.
 
Kutesa kwa zamu...zamani mlikuwa mnawaitia mgambo wawapige...fungeni maduka pigeni uchinga na nyie...wapo ambao wamefanya hivyo.
 
Wao hawana kosa --walipewa uhakika wa kufanya biashara katika mazingira yao endapo watatoa hela za vitambulisho
ila wanakera sana kwa kweli
wanapanga bidhaa zao mpk mabalabala hayapitiki tena.
kama lzm bidhaa zao wapange barabarani basi mtukufu awajengee na ma fraiova kabisa ya kuweka bidhaa zao.
 
hawa jamaa hata wakipanga biashara nje ya geti la nyumba yako huwezi kuwafanya kiti maana hiyo ni nyara ya serikali wafanyabiashara hapo wajiongeze tu waache kulipa kodi ya frem na maushuru watoe mzigo wapeleke home halafu wawe wanawapa wamachinga kidogo kidogo mpaka mzigo uishe
 
Back
Top Bottom