Ofisini kwa kawaida huwa nafika saa kumi na mbili kamili asubuhi, mida hiyo lile kampuni la kufanya usafi ofisini kwetu wafanyakazi wake wanafika hapa saa kumi au kumi na moja kasoro asubuhi, nawakuta wameshamaliza usafi sasa wanaelekea vyooni kusafisha.
Kuna msichana mmoja hapa amekuwa akinipiga mzinga wa nauli mara kwa mara anasema hana nauli, ni msichana mzuri sana hata huwezi amini kwanini anafanya kazi za usafi maofisini.
Siku moja al manusura shetani anishinde, lakini nilishinda nusu, nilimjaribisha kuomba mzigo, hakusita kukataa nikajuta kwanini nimemwomba halafu amekubali moja kwa moja ila hataki kufanyia ofisini anataka nje ya ofisi, nijajiuliza kwanini amekubali haraka hivi? halafu, kwanini nitembee na mfanya usafi ofisini anayeishi uswahilini huko? nikamwacha kama alivyo na nikaona huyu malaya tu kumbe na huo ulikuwa mtego wangu kwake kumfahamu ombaomba ya nauli yake.
Miezi mitano imeshapita sasa, anafanya usafi floor nzima wako na wanaume wawili vijana wenzie lakini yeye mcheshi kweli. Kuja kugundua, kumbe zile nauli alikuwa anatuomba wanaume wa vyumba vyote kwenye floor yetu kila mtu akimpiga kibuti cha nauli anakusanya kama konda wa daladala.
Kufanya utafiti, ametembea na wanaume wa floor nzima kasoro mimi, hapo ndipo nilichoka. Nikajiuliza kumbe hawa wasichana wa usafi ni wabaya hivi, si wanaweza kuambukiza UKIMWI ofisi au hata gorofa zima? halafu ni wazurii hadi unajiuliza inakuwaje msichana mzuri kama huyu anafanya kazi za usafi? kuweni makini wandugu.