Waepuke wanawake masikini

Sasa tukisema wote tukimbilie kwa wanawake wenye hela na wale wenye connection, hao wanawake wanaotokea familia masikini wataolewa na nani?
Na vipi na sisi tunaotokea familia masikini si ni bora tukawaoa masikini wenzetu kuliko hao wanawake wenye hela?

Binafsi nashauri kila mtu ashinde mechi zake. Fainali uzeeni.
 
kama ndo hao naunga mkono hoja, tena apo ni kukimbia ata peku !
#Hallelujah!!!
 
Angekuwa na pesa basi angekuwa ni mtu tofauti kabisa. Hakuna mtu anazaliwa akiwa mtu tayari, mapito ya duniani ndio hutupa utu. Moja kati ya mapito ni pesa.
Pesa haimbadilishi mtu, isipokua inafichua uhalisia wake
Kwahiyo hapa unamhukumu mtu mmoja kwa tabia za mtu mwingine tofauti(ambaye pia umekisia sana tabia zake kwasababu hayupo na humjui).
Suala la wanawake ku-prefer mwanaume wa daraja la juu zaidi sio individual cases. Hilo ni suala ambalo linaenda ndani mpaka kwenye nature yao.
Licha ya hayo yote, mahusiano/ndoa ndio jambo lenye risk kubwa zaidi kwenye maisha na hiyo risk haikwepeki. Mada kama hii haiwezi kuwa na hitimisho kwasababu mahusiano ni fumbo. Hakuna jibu sahihi, kuna machaguo tu.
Ofcourse ninachokiandika sio sheria, na ninatambua kuna wenye mawazo mbadala. Mwisho wa siku kika mtu atafanya maamuzi yake binafsi
 
Kuna ukweli kwa asilimia kubwa, japo hao unaoita maskini ndo wanaotoa furaha ya kweli kwa wanaume, angalia katika mahusiano wanandoa ambao wote wanakazi nzuri na maisha mazuri upande wa mahusiano hawako vizuri baba atatamani house maid angakuwa mke wake, na anaweza kuwa na mahusiano na mhudumu ofisini au dada wa mgahawa au pub. Cha msingi wanaume tutafute hela ili tuwe na uwezo wa kuhudumia. Asili ya mwanamke akiwa na hela zake hahitaji mwanaume wa kuanza kumghasi anataka uhuru zaidi ndo furaha yao, anahitaji mamlaka n.k.
 
Kwakutumia kigezo chako hiko hiko vipi wanawake nao wakisema hawawezi kumvumilia mwanaume ambaye bado hajajipata watakuwa wanakosea?
 
Mkuu smart ladies wako haijalishi wako kwenye hali gani. Na ukipata mmoja ume-win
Natambua hilo na nimetilia mkazo kwenye results zaidi ya potential, because results is a tangible measure for her smartness. Exception is everyshere, but dating a broke woman the outcome is rarely favourable
 

ni bailojia ya wanawake, tangia zama za kale wakati binadamu tunaishi mapangoni (tulifundishwa hata shuleni) wanawake walitafuta mwenza ambaye angeweza kuwalinda yeye na mzao wake i.e mwenye uwezo wa kuwinda na kuleta chakula watoto wasife njaa, kuwasha moto kufukuza wanyama wakali n.k. hata kwenye animal kingdom ni hivyo kwa mfano kwa masokwe, yule sokwe mkubwa na mwenye nguvu ndiyo hupata wanawake na kuendeleza kizazi wale masokwe dhaifu hawapati demu wanakufa hivyo.

hivyo kuanza kuchallenge kitu kama hicho unapoteza muda wako kwa maana hauwezi kubadilisha kitu, kwa mf. ukiwa unatembea na demu wako ghafla mkavamiwa halafu wewe ukakimbia ukamuacha nyuma akaporwa bila ya kumkingia kifua unafikiri ataendeleza mahusiano na wewe? au hata akiendeleza unafikiri atakuchukulia the same?

women date up, i.e pale alipo anaangalia labda pale pale au juu ya pale lkn siyo chini ni ukweli ambao ulipaswa kuuzoea kama bado haujaelewa, hivyo ukitaka kuendeleza kizazi kuwa kama sokwe work on your self vinginevyo no chance ya kupata mwenza ...
 
Kuombaomba ni suala jingine na umasikini ni suala jingine. Jaribu kuelewa vizuri msingi wa hoja.

Ndiyo hapo tunashindwa kuelewana ,kati ya masikini na ombaomba...Wewe unazunzumzia tusidate na masikini lakini context ni ya ombaomba.

Ndiyo maana nikasema hapo awali hata hao unaowaona siyo masikini(wenye vipato vyao either kuajiriwa /kujiajiri) ni ombaomba wa kutupwa.

Kama tegemezi ,hakuna binadamu ambaye si tegemezi ,hata wewe ni tegemezi either kama umeajiriwa unategemea huruma ya HR/mwajiri au kama umejiajiri unategemea wateja ,hivyo hivyo kwa hao unaosema broke pia wana michango yao katika uhusiano.

Hizo tabia za broke ladies hata hao ladies walijipata wanazo ,na kama issue ni masikini wapo pia broke ladies hawapigi mizinga.
 
Kwakutumia kigezo chako hiko hiko vipi wanawake nao wakisema hawawezi kumvumilia mwanaume ambaye bado hajajipata watakuwa wanakosea?
Kusema hawezi kumvumilia mwanaume ambae hajajipata hapo anakosea, kwa sababu hakuna mwanaume aliekuja hapa duniani kwa ajiri ya kuboresha maisha ya mwanamke. No man owe her better life.

Lakini mwanamke akisema hawezi kuwa na mwanaume ambae hana hela au hajajipata hapo yupo sahihi. Is her choice, it's not evil
 
Mimi
Nawataka hao wanawake maskini.
Ukiniletea kama 10
Kwa kila mmoja nitakuzawadia milion moja za kitanzania.
Wahi mapema
Nafasi ni chache.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…