Wadau wa trekta, Mahindra vipi?

mboncalo

New Member
Sep 15, 2022
1
3
Habari, wadau nnaomba kuwasilisha hapa jukwaani, kuna aina mbalimbali za trekta hapa bongo, nimeona watu wanazungumzia sana Holland, Ford, Sonalika, Swaraj na mengineyo lakini sijaona sehemu wanayozungumzia Mahindra wakati nikiangalia kwenye mitandao wanasema ndo ya kwanza kwa mauzo.

Maswali

1. Kwanini hii mahindra sio maarufu sana hapa nchini
2. Gharama zake zimekaaje?
3. Vipi kuhusu ubora na uhai wake? yanadumu?
4. vipi suala la spare zake zinapatikana nchini hapa?
5. Kuna changamoto zozote umeziona kwa mtu mwenye uzoefu nazo?

Swali la mwisho kama kuna mtu yeyote ana uzoefu au taarifa zozote kuhusu Deutz Fahr tractors naomba msaada tafadhali wa experience yao...............
 
Chukua hiyo trekta, Mahindra ni moja kati ya trekta imara sana. Sio Tz tu, hata huko India. Sema zimemezwa na hizi kilimo kwanza zetu (Newholland). Yeyote anaekwambia Mahindra ni trekta mbovu au haifai, basi hajui lolote kuhusu matrekta, au hajui kutunza, au stori za vijiweni analeta hapa. Mahindra ni trekta nzuri sana.

-Trekta zote sasa hivi bei ipo juu. Bei inakua juu zaidi kulingana na kampuni na ukubwa wake(Hp na kama ni 2wd au 4wd, vyote hivi vitaamua ukubwa au udogo wa bei)

-Spare unazipata Tz hii hii wala hazisumbui kupatikana.

-Changamoto zake mara nyingi zinakuja kwa mmiliki mwenyewe analitunzaje
 
Back
Top Bottom