‘Wachambuzi’ wa kandanda letu na mpasuko kwenye jamii

fredito13

JF-Expert Member
Sep 3, 2012
213
145
Hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la wadau wa mchezo wa mpira wa miguu ambao wanafanya kazi ya kutathmini na kuchambua michezo mbali mbali hapa nchini, hasa mchezo wa soka (gozi la ng’ombe, kandanda au bolu). Ongezeko hili la wadau hawa ambao wanajitambulisha na kutambulika kama wachambuzi ni suala ambalo lipo kila nchi ya Africa na kila nchi ina namna ambavyo inawapa nafasi hawa ‘wachambuzi’.

Hapa kwetu Bongoland wachambuzi wamejaa kuanzia vijiwe vya bolu huko mitaani, kwenye mitandao ya kijamii na kwenye vyombo vya habari (gazeti, radio, televisheni). Wakati baadhi ya wachambuzi ni wastaafu wa mchezo wa mpira, wengine ni wale ambao wamejifunza mpira kwa kuutazama tu, ila wote wanafanya kazi inayofanana!

Wingi wa wachambuzi wa bolu umeambatana na ongezeko la ‘vishoka’ au ‘makanjanja’ ambao wanatumia jukwaa la uchambuzi kutengeneza mpasuko kwenye jamii kwa sababu ya utendaji wao! Ndio maana ukipita kwenye mitandao ya kijamii, kila wakati utakuta wachambuzi wakitukana au kutukanwa na baadhi ya wadau huku wengine wakiwapongeza (kwa kuangalia hoja iliyotolewa na namna ilivyowasilishwa). Haya ni baadhi ya matatizo ambayo yanaletwa na ‘wachambuzi’ wa mpira wa miguu hapa nyumbani!

Baadhi ya wachambuzi kwa makusudi au kutokujua wamekuwa wakitoa maoni ambayo yanavunja utu na heshima ya wadau wengine wa michezo! Hili linafanyika kupitia machapisho ya kwenye mitandao ya kijamii au vyombo vingine vya habari, hasa redio na TV!

Baadhi ya wachambuzi wana maslahi binafsi kwenye suala zima la uchambuzi wa Timu, mechi au mchezaji! Mfano, kuna wachambuzi wa bolu ambao pia ni Mameneja wa wachezaji kwenye ligi hii hii! Wachambuzi hawa, kwa makusudi wamekuwa wakiwazungumzia vibaya baadhi ya wachezaji na kuwapamba wachezaji wanaowasimamia! Hili linafanyika kwa lengo la kutengeneza soko la wachezaji wanaowasimamia!

Pia, kuna wachambuzi ambao kwa makusudi kabisa, wanajikita zaidi kujadili maisha binafsi ya mchezaji au wachezaji nje ya uwanja na kuwaharibia sifa wachezaji husika! Hili limefanyika mara nyingi na athari zake tumeziona!

Zaidi, wachambuzi wengi ni wachambuzi wa ‘SIMBA na YANGA’ na sio timu 16 au zaidi zinazoshiriki ligi zetu! Katika kila kipindi cha michezo, wachambuzi wamekuwa wakihakikisha kuna jambo linalohusu moja ya timu hizo mbili au zote! Wanaojiongeza kidogo basi watazungumzia Azam FC! Liwe zuri au baya, lililothibitishwa au halijathibitishwa, wachambuzi hawa watalazimisha hoja hiyo iwe ndefu na kunyima nafasi kwa timu zingine kuzungumziwa, hata kama kuna jambo kubwa! Hatuwezi kuwa na ligi yenye ushindani stahiki kama wachambuzi wanachagua

Mbaya zaidi, wachambuzi wetu wengi wamekuwa watu wa hisia zaidi kuliko uhalisia! Wachambuzi wetu wako kwenye kujadili matukio ya timu zaidi kuliko kufanya tathmini ya kiufundi kuhusu timu yao! Mfano, mchambuzi kuzungumzia namna timu ilivyofika uwanjani kwa muda wote wa mapumziko na kushindwa kusema hali hiyo imemuathiri nani au imeathiri Vipi mbinu za timu husika!

Wachambuzi wetu wamekuwa bora zaidi kuandika mambo ya nje ya uwanja ambayo hayajitaji ufundi na kuacha kazi ya msingi kutathmini michezo na uwezo wa Timu au wachezaji! Wengi wanaoitwa ‘Wachambuzi’ ni kama watoa habari tu na sio wachambuzi kama tunavyowaita!

Wakati suala la kufanya tathmini na uchambuzi wa michezo ni sehemu muhimu ya ajira, lakini pia haki ya kikatiba mtu kuzungumza kile anachotaka, kuna umuhimu wa TFF na mamlaka zingine za kiserikali kuandaa semina na mafunzo kwq hawa wachambuzi ili kupunguza utitiri wa habari zinazorushwa kwenye jamii na kutengeneza mipasuko!
 
𝐖𝐚𝐜𝐡𝐚𝐦𝐛𝐮𝐳𝐢 𝐰𝐞𝐧𝐠𝐢𝐧𝐞 𝐰𝐚 𝐦𝐜𝐡𝐨𝐧𝐠𝐨 𝐭𝐮, 𝐰𝐚𝐧𝐚𝐭𝐚𝐟𝐮𝐭𝐚 𝐚𝐭𝐭𝐞𝐧𝐭𝐢𝐨𝐧, 𝐥𝐢𝐤𝐞𝐬 𝐧𝐚 𝐟𝐨𝐥𝐥𝐨𝐰𝐞𝐫𝐬
 
Mchambuzi wa mpira alikuwa mmoja tu Tanzania Mwalimu kashasha..

Hawa wengine ni wachambuzi uchwara, wasakatonge.
 
Wacha- mbuzi ni wale wanaongelea ongelea na tu mpira na wanasimulia matukio ya kwenye mpira, hawa ni wengi sana wamejitokeza siku hizi
 
WANANCHIIIIIIIIIIOOOOOOOOO. LEO NDIO ILE SIKU AMBAYO WANAYANGA WOTE TUNA BANG NAYO .
YAANI MAKOLO LEO NDIO RASMI WANAGEUZA VYOO MAHALA PAO PA KULILIA.
TUNAENDA KUTINGA FAINALI RASMI KWENYE ARDHI YA UGENINI.
MARK MY WORDS
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom