Wadau msaada wenu kuhusu gharama za ku print jarida

Roga Roga

JF-Expert Member
Dec 20, 2013
645
500
Wadau wa Jf naombeni mnisaidie nataka nianzishe jarida maalum la burudani na mziki. Wapi naweza kupata huduma ya gharama nafuu ya kuprint jarida hilo. Nategeme kutoa nakala 5000 awamu ya kwanza. Jarida nataka liwe coloured na liwe na page 30. Naombeni msaada wenu.
 
Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,070
2,000
kwa uzoefu wangu kwa vile unaprint nyingi inaweza kuwa kwenye 5,000 000 ( million 5 )
wewe utauza kwa 3,000 hivo utapata 15,000,000
ukiweka za kulipwa kutokana na matangazo unaweza pata 18,000,000
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,879
1,250
Maelezo marefu ya mdau kassamali ni zaidi nadharia kuliko kupata maelezo kwa watendaji wa kazi yenyewe. Wengi hutumia zaidi ya darasani wakati ukiingia kwenye utendaji utakutana na hali ambayo ya darasani yanaenda kusini wakati ya utendaji yanaelekea kaskazini. Hata hivyo umejitahidi kuleta ufafanuzi.

Kwa uzoefu wangu ni kama ifuatavyo:

Idara ya costing/estimation
Awe ni mwenye uwezo wa kujua hatua zote za mwanzo hadi umaliziaji wa kazi, kujua gharama za material, labor work, office expenses, salary, transportation, Revenue, fidia ya gharama za dharura, na gharama nyinginezo. Huyu ni mtu muhimu lazima awe na upeo, ujuzi, ubunifu, werevu, mvuto kwa wateja na kabisa awe ni mchumi na anayejua mambo ya procurement.

images (7).jpg
Ujipange kuwa na editorial board
Unahitaji jopo la wahariri wawe ni full time, au part time na wengine just writers na pengine reporters. Hiyo ndiyo source muhimu ya kukusanya news. Ukifanya peke yako kitakuwa kitu kama blog hivi kitu ambacho hakina hadhi kwa public media. Unahitaji watu wenye maono mbalimbali na tofautitofauti ambao watajenga kitu kikamilike. Hali kadhalika fani hii haitakiwi mwenye kuleta au kuandika habari aihariri, la hasha, lazima kuwa na mwingine anayehariri ndipo anaweza kuona zaidi makosa na lugha ambayo haistahili kwa public media isahihishwe.

images (6).jpg
Advertising
Matangazo ni muhimu na ndiyo yenye kulipa zaidi gharama za uendeshaji wa jarida lako. Kutegemea mauzo tu ya jarida ni kidogo sana na pengine utakuja kushtukia hata gharama za uendeshaji tu zinafikia kufuani tu badala ya kufikia kimo cha mtu mzima hadi utosini. Hiyo nayo ni idara muhimu na ndiyo yenye kulipa zaidi na pengine hata kukuletea faida zaidi katika biashara ya jarida lako.

plate-making.jpg Mtambo wa plate making, hiyo inaonekana na picha ni plate tayari kuchapisha nakala mtamboni
Publishing - Pre Press production
Hii ni hatua muhimu ambayo kazi za wahariri na idara ya matangazo zinapokusanywa na kuwekwa pamoja kwa utaratibu wa kutengeneza kurasa. Mratibu wa hatua hii ni mhariri mtengenezaji wa kurasa ambaye anatakiwa awe na ujuzi wa publishing. Jambo la msingi kuwa na ujuzi wa layout and design, paste up, graphic design, page format, input and output for films, paper or metal plates. Kwa kawaida metal plated hufanyizwa kwa mtambo wa plate making machine kwa kutumia mitambo mojawapo uitwao repromaster dublication machine. Sina muda wa kuelezea zaidi nafasi haitoshi. Kuna baadhi ya makampuni na hasa waanzaji hupenda kutumia mfumo wa zamani wa pre-press kwa kutumia vitendea kazi vya camera, projeters na processing liquids. Kama unaweza kufanya hatua hii wewe mwenyewe utakuwa umepunguza gharama kubwa za printing, maana huko wakianzia hatua hii watakunyofoa pesa nyingi.

Printing
Iwapo hatua ya pre-press umeifanya tayari kama nilivyoainisha hapo juu, basi utakachohitaji ni kupeleka kwenye mitambo ya uchapaji (printing).
Inategemea printing utakayo tumia, maana kuna aina mbalimbali za printing.

download.jpg images.jpg Letter press printing mashines
Letter press pringint ni wa zamani ambao hutumia muda mwingi katika kupanga herufi au kuzitengeneza kisha kufanya composing ili kukamilisha kazi.
images.jpg images (2).jpg Kushoto 6 color unit machine na kulia webpress for newspaper (offset)
Offset printing ni mtindo wa kisasa ambao katika uchapishaji lazima kuwe na maji yanayoenda sambamba na wino, kitaalamu kuna water dump rollers na ink rollers. Jambo gumu kwa wasio wataalamu na wazoefu katika masuala ya uchapishaji, kwa bahati mbaya sina nafasi ya kutosha kuleta maelezo namna inavyofanya kazi. Kifupi ni kwamba ni mfumo kama wa lugha ya computer kama ilivyo off -set, yaani yes or no. Kwa maana kwenye no basi maji yatapita, na kwenye yes maji yatakataa na wino utapita ndivyo inavyotokea taswira kwenye plate na kisha kuwa transfered kwenye karatasi. Wino utumikao katika uchapaji wa aina hii ni oil base ndio maana kwenye maji unakataa, na maji kwenye wino huo hukataa.

images (4).jpg Flexo Printing unit with flexo plate mounted to the press cylinder
Flexo Plate Printing, huu ni mtindo wa uchapati kama wa Offset lakini hautumii maji bali ni wino tu ambao ni water base ink. Plate zake ni za plastic na watumiaji wengi wa mtindo huu ni wachapishaji wa majarida na magazeti kwa vile hudumu muda zaidi kuliko metal plate taswira husha upesi. paper plate nayo ndio mbaya zaidi inahitaji nakala chache sana.

Gravure-Printing-Machine-HYA-81200FX-.jpg images (3).jpg
Sehemu ya mtambo wa engrave printing unit sehemu ya kwanza na sehemu ya pili inayokusanya na kufunga bundle pesa zinapochapishwa
Engrave printing hii ni giant printing ambayo hutoa nakala za mamilioni, kwa afrika bado hatuna sababu ya kuwa na mitambo aina hii kwa vile ni ghali na inahitaji sana kutumika kwa nakala nyingi malaki na zaidi ni mamilioni. Pre press huhamishia taswira kwenye cylinder mchuma uliokuwa composite na material mengine, mcylinder huyo hufungwa kwenye mtambo. Kawaida aina hii ya uchapaji haitumii wino kidogo, bali kuna visima kama ilivyo gas station hivyo wino husafiri kwenda kwenye mtambo na unaobaki hurudi kwenye matanki. Uchapaji aina hii mitambo mingi huendeswa automatic na mingi ni robotical interface system. Nisingependa kuelezea zaidi hiyo kwa vile kwa mazingira ya Afrika to earlly kwa vile production haijafikia kiwango cha kuwa na mitambo ghali hivi. Mtambo huu huenda kasi sana na kama ni majarida au vitabu ndani ya 24 hour huzalisha nakala pengine zaidi ya milioni, ndio maana finishing huhitajika robot kukusanya vitabu kwa vile kasi yake kwa binadamu ni vigumu, na kwa kawaida kuna conveyor ambayo husafirisha printed material hadi unit ya binding.

images (1).jpg Mtambo wa digital printing
Digital printing, huu ni mpango mzima wa kisasa wa kuchapisha ambao operator hutumia zaidi touch screen monitor. One heading press ni mamilioni ya $, kama ni full color ambapo inahitajika four heads hapo ni makampuni makubwa yenye uwezo nazo na ni very complicated. Mara nyingi kuna online service na kama kuna tatizo manufacture hufanya service online. Kwa mazingira yetu bado kidogo hatua hii, ni ghali inahitaji wataalamu waliobobea kwa kizazi hiki cha digital.

images (9).jpg printing_copying.jpg
Copy printing machine
Kuna baadhi ya kazi zinazoweza kuchapwa kwa njia hii, lakini njia hii si nzuri na huwa taswira haidumu muda mrefu. Sababu kwa njia hii mashine hazitumii wino bali toner ambayo ni ungaunga usioweza kudumu muda mrefu na pengine unaweza kufuta tu ukifanya jitihada, wino haufutiki kwa vile unaingia kwenye pours za karatasi lakini toner huwa imetapakaa juu tu. Iwapo uchapishaji ukifanyika kwenye karatasi yenye fine texture basi hapo madhara ni makubwa. Kwa jarida uchapishaji aina hii haufai, hii ni kwa shughuli za msimu mfupi tu.

images (5).jpg
Marketing/distribution
Idara hii ni muhimu pia kwa vile production baada ya kukamilika unahitaji idara hii kutafuta soko na kusambaza. Hali kadhalika ndo ni idara ya kushughulikia matangazo ujuavyo ulimwengu wa leo wa biashara ni matangazo.

images (8).jpg copies-Roanoke.jpg
Full color printing
Katika mada yako umeongela kuwa unapendelea jarida lako liwe full color kwa lugha ya kitaalamu, yaani kama kuna picha basi ziwe za rangi badala ya rangi moja kama tulivyozoea kuita black and while. Kumbuka kuwa kuchapisha rangi ni ghali zaidi, na kwamba gharama huwa zaidi katika material kwa sababu rangi moja unahitaji unit moja ya printing, lakini full color lazima uwe na 4 printing unites. Full color kuna cyan color (blue), magenta (nyekundu), yellow na nyeusi. Hivyo kila rangi lazima iwe na unit yake pekee inayojitegemea na karatasi lazima lipitie unit zote ili kuwa na picha ya full color. Pia kuna utaalam wa color separation kwa mpangilio wa half tone dots na kila color kuna angle yake. Bila hivyo kupata rangi huwa ngumu na ndio maana kuna mitambo maalumu ya color separation ili kuweza kuwa na kiwango kinachotakiwa. Hata hivyo kwa siku za leo kazi nzuri ni ile ambayo kuna full color, ukiwa na jarida la rangi moja usishangae kushinda unapangusa vumbi tu bila kununuliwa, watu wanafuata kinachovutia macho.

NB kwa mwanzaji si lazima kuwe na idara zote hizi zinazojitegemea, unaweza kuunganisha baadhi ya idara ikafanya mbili mfano idara ya costing/estimation inaweza kuunganishwa na hii ya marketing. Editorial ikawa pamoja na publishing, nk.

Hivyo basi unapokusudia kufanya biashara hii, jambo la msingi fikiria haya niliyoeleza hapo juu, kisha kwa kutumia dondoo hizo andaa business plan yako ambayo kwa vyo vyote kama mwandaaji ni mzoefu na mjuaji atagusa kila kipengele na kufanya tathmini ya mapato na matumizi kwa kila nakala hali kadhalika matarajio ya nusu mwaka na mwaka mmoja. Tathmini hiyo itakupa picha kama ufanye biashara hiyo au la, maana gharama za maandalizi kwa shughuli hii ina cost material sana, hivyo muhimu kufanya tathmini ya kutosha.

CC;
Roga Roga
 
Attachments

 • images.jpg
  File size
  5.3 KB
  Views
  128
 • images (1).jpg
  File size
  9.4 KB
  Views
  452
 • images (2).jpg
  File size
  12.1 KB
  Views
  127

kassamali

JF-Expert Member
Jan 11, 2010
215
195
Maelezo marefu ya mdau kassamali ni zaidi nadharia kuliko kupata maelezo kwa watendaji wa kazi yenyewe. Wengi hutumia zaidi ya darasani wakati ukiingia kwenye utendaji utakutana na hali ambayo ya darasani yanaenda kusini wakati ya utendaji yanaelekea kaskazini. Hata hivyo umejitahidi kuleta ufafanuzi.

Kwa uzoefu wangu ni kama ifuatavyo:

Idara ya costing/estimation
Awe ni mwenye uwezo wa kujua hatua zote za mwanzo hadi umaliziaji wa kazi, kujua gharama za material, labor work, office expenses, salary, transportation, Revenue, fidia ya gharama za dharura, na gharama nyinginezo. Huyu ni mtu muhimu lazima awe na upeo, ujuzi, ubunifu, werevu, mvuto kwa wateja na kabisa awe ni mchumi na anayejua mambo ya procurement.

View attachment 128616
Ujipange kuwa na editorial board
Unahitaji jopo la wahariri wawe ni full time, au part time na wengine just writers na pengine reporters. Hiyo ndiyo source muhimu ya kukusanya news. Ukifanya peke yako kitakuwa kitu kama blog hivi kitu ambacho hakina hadhi kwa public media. Unahitaji watu wenye maono mbalimbali na tofautitofauti ambao watajenga kitu kikamilike. Hali kadhalika fani hii haitakiwi mwenye kuleta au kuandika habari aihariri, la hasha, lazima kuwa na mwingine anayehariri ndipo anaweza kuona zaidi makosa na lugha ambayo haistahili kwa public media isahihishwe.

View attachment 128615
Advertising
Matangazo ni muhimu na ndiyo yenye kulipa zaidi gharama za uendeshaji wa jarida lako. Kutegemea mauzo tu ya jarida ni kidogo sana na pengine utakuja kushtukia hata gharama za uendeshaji tu zinafikia kufuani tu badala ya kufikia kimo cha mtu mzima hadi utosini. Hiyo nayo ni idara muhimu na ndiyo yenye kulipa zaidi na pengine hata kukuletea faida zaidi katika biashara ya jarida lako.

View attachment 128607 Mtambo wa plate making, hiyo inaonekana na picha ni plate tayari kuchapisha nakala mtamboni
Publishing - Pre Press production
Hii ni hatua muhimu ambayo kazi za wahariri na idara ya matangazo zinapokusanywa na kuwekwa pamoja kwa utaratibu wa kutengeneza kurasa. Mratibu wa hatua hii ni mhariri mtengenezaji wa kurasa ambaye anatakiwa awe na ujuzi wa publishing. Jambo la msingi kuwa na ujuzi wa layout and design, paste up, graphic design, page format, input and output for films, paper or metal plates. Kwa kawaida metal plated hufanyizwa kwa mtambo wa plate making machine kwa kutumia mitambo mojawapo uitwao repromaster dublication machine. Sina muda wa kuelezea zaidi nafasi haitoshi. Kuna baadhi ya makampuni na hasa waanzaji hupenda kutumia mfumo wa zamani wa pre-press kwa kutumia vitendea kazi vya camera, projeters na processing liquids. Kama unaweza kufanya hatua hii wewe mwenyewe utakuwa umepunguza gharama kubwa za printing, maana huko wakianzia hatua hii watakunyofoa pesa nyingi.

Printing
Iwapo hatua ya pre-press umeifanya tayari kama nilivyoainisha hapo juu, basi utakachohitaji ni kupeleka kwenye mitambo ya uchapaji (printing).
Inategemea printing utakayo tumia, maana kuna aina mbalimbali za printing.

View attachment 128605 View attachment 128606 Letter press printing mashines
Letter press pringint ni wa zamani ambao hutumia muda mwingi katika kupanga herufi au kuzitengeneza kisha kufanya composing ili kukamilisha kazi.
View attachment 128608 View attachment 128604 Kushoto 6 color unit machine na kulia webpress for newspaper (offset)
Offset printing ni mtindo wa kisasa ambao katika uchapishaji lazima kuwe na maji yanayoenda sambamba na wino, kitaalamu kuna water dump rollers na ink rollers. Jambo gumu kwa wasio wataalamu na wazoefu katika masuala ya uchapishaji, kwa bahati mbaya sina nafasi ya kutosha kuleta maelezo namna inavyofanya kazi. Kifupi ni kwamba ni mfumo kama wa lugha ya computer kama ilivyo off -set, yaani yes or no. Kwa maana kwenye no basi maji yatapita, na kwenye yes maji yatakataa na wino utapita ndivyo inavyotokea taswira kwenye plate na kisha kuwa transfered kwenye karatasi. Wino utumikao katika uchapaji wa aina hii ni oil base ndio maana kwenye maji unakataa, na maji kwenye wino huo hukataa.

View attachment 128613 Flexo Printing unit with flexo plate mounted to the press cylinder
Flexo Plate Printing, huu ni mtindo wa uchapati kama wa Offset lakini hautumii maji bali ni wino tu ambao ni water base ink. Plate zake ni za plastic na watumiaji wengi wa mtindo huu ni wachapishaji wa majarida na magazeti kwa vile hudumu muda zaidi kuliko metal plate taswira husha upesi. paper plate nayo ndio mbaya zaidi inahitaji nakala chache sana.

View attachment 128612 View attachment 128611
Sehemu ya mtambo wa engrave printing unit sehemu ya kwanza na sehemu ya pili inayokusanya na kufunga bundle pesa zinapochapishwa
Engrave printing hii ni giant printing ambayo hutoa nakala za mamilioni, kwa afrika bado hatuna sababu ya kuwa na mitambo aina hii kwa vile ni ghali na inahitaji sana kutumika kwa nakala nyingi malaki na zaidi ni mamilioni. Pre press huhamishia taswira kwenye cylinder mchuma uliokuwa composite na material mengine, mcylinder huyo hufungwa kwenye mtambo. Kawaida aina hii ya uchapaji haitumii wino kidogo, bali kuna visima kama ilivyo gas station hivyo wino husafiri kwenda kwenye mtambo na unaobaki hurudi kwenye matanki. Uchapaji aina hii mitambo mingi huendeswa automatic na mingi ni robotical interface system. Nisingependa kuelezea zaidi hiyo kwa vile kwa mazingira ya Afrika to earlly kwa vile production haijafikia kiwango cha kuwa na mitambo ghali hivi. Mtambo huu huenda kasi sana na kama ni majarida au vitabu ndani ya 24 hour huzalisha nakala pengine zaidi ya milioni, ndio maana finishing huhitajika robot kukusanya vitabu kwa vile kasi yake kwa binadamu ni vigumu, na kwa kawaida kuna conveyor ambayo husafirisha printed material hadi unit ya binding.

View attachment 128609 Mtambo wa digital printing
Digital printing, huu ni mpango mzima wa kisasa wa kuchapisha ambao operator hutumia zaidi touch screen monitor. One heading press ni mamilioni ya $, kama ni full color ambapo inahitajika four heads hapo ni makampuni makubwa yenye uwezo nazo na ni very complicated. Mara nyingi kuna online service na kama kuna tatizo manufacture hufanya service online. Kwa mazingira yetu bado kidogo hatua hii, ni ghali inahitaji wataalamu waliobobea kwa kizazi hiki cha digital.

View attachment 128619 View attachment 128620
Copy printing machine
Kuna baadhi ya kazi zinazoweza kuchapwa kwa njia hii, lakini njia hii si nzuri na huwa taswira haidumu muda mrefu. Sababu kwa njia hii mashine hazitumii wino bali toner ambayo ni ungaunga usioweza kudumu muda mrefu na pengine unaweza kufuta tu ukifanya jitihada, wino haufutiki kwa vile unaingia kwenye pours za karatasi lakini toner huwa imetapakaa juu tu. Iwapo uchapishaji ukifanyika kwenye karatasi yenye fine texture basi hapo madhara ni makubwa. Kwa jarida uchapishaji aina hii haufai, hii ni kwa shughuli za msimu mfupi tu.

View attachment 128614
Marketing/distribution
Idara hii ni muhimu pia kwa vile production baada ya kukamilika unahitaji idara hii kutafuta soko na kusambaza. Hali kadhalika ndo ni idara ya kushughulikia matangazo ujuavyo ulimwengu wa leo wa biashara ni matangazo.

View attachment 128617 View attachment 128618
Full color printing
Katika mada yako umeongela kuwa unapendelea jarida lako liwe full color kwa lugha ya kitaalamu, yaani kama kuna picha basi ziwe za rangi badala ya rangi moja kama tulivyozoea kuita black and while. Kumbuka kuwa kuchapisha rangi ni ghali zaidi, na kwamba gharama huwa zaidi katika material kwa sababu rangi moja unahitaji unit moja ya printing, lakini full color lazima uwe na 4 printing unites. Full color kuna cyan color (blue), magenta (nyekundu), yellow na nyeusi. Hivyo kila rangi lazima iwe na unit yake pekee inayojitegemea na karatasi lazima lipitie unit zote ili kuwa na picha ya full color. Pia kuna utaalam wa color separation kwa mpangilio wa half tone dots na kila color kuna angle yake. Bila hivyo kupata rangi huwa ngumu na ndio maana kuna mitambo maalumu ya color separation ili kuweza kuwa na kiwango kinachotakiwa. Hata hivyo kwa siku za leo kazi nzuri ni ile ambayo kuna full color, ukiwa na jarida la rangi moja usishangae kushinda unapangusa vumbi tu bila kununuliwa, watu wanafuata kinachovutia macho.

NB kwa mwanzaji si lazima kuwe na idara zote hizi zinazojitegemea, unaweza kuunganisha baadhi ya idara ikafanya mbili mfano idara ya costing/estimation inaweza kuunganishwa na hii ya marketing. Editorial ikawa pamoja na publishing, nk.

Hivyo basi unapokusudia kufanya biashara hii, jambo la msingi fikiria haya niliyoeleza hapo juu, kisha kwa kutumia dondoo hizo andaa business plan yako ambayo kwa vyo vyote kama mwandaaji ni mzoefu na mjuaji atagusa kila kipengele na kufanya tathmini ya mapato na matumizi kwa kila nakala hali kadhalika matarajio ya nusu mwaka na mwaka mmoja. Tathmini hiyo itakupa picha kama ufanye biashara hiyo au la, maana gharama za maandalizi kwa shughuli hii ina cost material sana, hivyo muhimu kufanya tathmini ya kutosha.

CC;
Roga Roga

Mkuu nakubaliana na wewe unachokisema sahii lakini mimi nipo zaidi kwenye printing zaidi ya miaka mitano unaweza kuangalia kampuni yetu hapa Главная - peroprinters.com data nilizotoa nikutokana na uzoefu lakini lazima ujue kazi yangu mimi ni kuhakikisha jarida lenye quality ya juu lipo mikononi mwako suala la uuzaji linategemea na mteja na jinsi alivyojidhatiti kuingia sokon ofcourse matangazo ni muhimu.

Kama Roga Roga yupo tayari nitumie info kwenye email nitakupa full calculation ya kila kitu

info@peroprinters.com
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,879
1,250
Mkuu nakubaliana na wewe unachokisema sahii lakini mimi nipo zaidi kwenye printing zaidi ya miaka mitano unaweza kuangalia kampuni yetu hapa Ð"лавная - peroprinters.com data nilizotoa nikutokana na uzoefu lakini lazima ujue kazi yangu mimi ni kuhakikisha jarida lenye quality ya juu lipo mikononi mwako suala la uuzaji linategemea na mteja na jinsi alivyojidhatiti kuingia sokon ofcourse matangazo ni muhimu.

Kama Roga Roga yupo tayari nitumie info kwenye email nitakupa full calculation ya kila kitu

info@peroprinters.com

Haina maana nimeona uliyoeleza si mazuri, umeongelea kitaaluma zaidi na ni vema. Nilichokifanya nadhani unaweza kutambua kwamba katika uwanja huu nina marefu na mapana ndio maana nimejaribu kudadafula na kuonyesha njia mbalimbali zinazotumiwa katika uchapishaji huo hivyo ajue ni mtambo aina gani utatumika katika kuchapisha maana maandalizi ya pre press lazima kujua aina ya mtambo utakaochapisha, hali kadhalika kama ni kuandaa plates kujua pia kuachia nafasi kiasi gani cha clippers za mashine kushika plate ili taswira isipotee kwenye clippers. Ukubwa wa machine ya uchapaji maana plates na karatasi ziendane na mtambo huo. Kuna mengi tu ambayo ni muhimu ambayo katika business plan husaidia kuyaweka wazi. Vinginevyo kuandaa kazi kiswahili swahili au kibongobongo matoke unashtukia umepoteza pesa na muda kwa maandalizi yasiyoendana na mitambo itakayotumika kuchapisha nakala zako.

Jambo la msingi anachotakiwa kufanya ni business plan kuiandaa, maelezo yangu niliyoeleza hapo kwenye bandiko #5 ni kumsaidia kufuata mfululizo wa kuandaa business plan. Biashara za siku hizi ni muhimu kufanya hilo na hasa kujua mapana na marefu, makisio na matarajio kwa siku zijazo inafikia wapi ndivyo business plan yake itakavyokuwa.

Unaweza kumsaidia kuandaa hiyo calculation utakuwa umemsaidia, mimi sina nia kufanya hivyo, lakini si mradi jarida lichapishwe mradi calculation imefanyika, business plan ni muhimu maana itamsaidia kujua nafasi ya biashara yake, mauzo, eneo la mauzo, walengwa wa mauzo, gharama za uendeshaji, mishahara, labor charges, revenue, office expenses, matangazo, usafiri na mengineyo. Akishayaweka sawa hayo kwenye business plan yake kwa mpango huo huendana pia na kuainisha calculation ya mradi mzima hapo anakuwa amepata kitu kamili na kujua future development ya mradi wake. Lakini hii ya calculation peke yake nadhani kuna kitu fulani kitakuwa kimekosekana ndio wengi utakuwa wanaanza mradi na kushtukia yanajitokeza magumu kumbe business plan ingeandaliwa kitaalam utakutana nayo yote kwa vile katika uandaaje wake kuna viashiria vinavyotumika kuandaa.

Bahati nzuri mimi ni mzoefu katika uwanja huu nchini Tanzania na nchi hizo zilizopaa kimaendeleo. Mitambo niliyoelezea hapo juu yote nimeitumia hadi robot katika utendaji wa kazi hizi. Ninachojaribu kufafanua ni uzoefu wangu licha ya elimu yangu katika uwanja huu najaribu zaidi kutoa ufafanuzi kiutendaji kwa vile ndio mang'amuzi ya kazi yangu. Kwa vile nimecheza zaidi na pre press na kiasi fulani uendeshaji wa mitambo hiyo hapo juu nadhani uzoefu wangu wa maelezo utamsaidia pia katika kufanya tathmini ya biashara yake kabla ya kuanza ili kujipanga vizuri.

Katika bandiko litakalofuata baada ya hili nitajaribu kuambatanisha tamplates za fomula za kuandaa business plan.
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,879
1,250
The business plan

OBJECTIVE: The business plan is the key ingredient for a successful business and is often ignored. This session shows you how to create an individualized business plan, and provides the tools to make it easy.Ukitaka kupata dondoo nyingi za business plan na uandaaji waji wake tembelea website ifuatayo hapo chini itakusaida kupata mengi na namna ya kuandaa business plan yako.

SAMPLE BUSINESS PLAN TEMPLATE

www.inis.gov.ie/.../Sample%20Business%20Plan%20Template.../Sample...‎​
This section should not be completed until the business plan is written. .... Profile of key players (company size, turnover, profitability etc) and their market share ...
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,879
1,250
kassamali
Nimeangalia website yenu, you have some experience so far, haba na haba atajaza kibaba, ni mautundu yake kutumia madodo tunayomwaga hapa mwingine analeta ugali, mwingine ubwabwa na mwingine anakamilisha kwa kumwaga mboga na mapochopocho wakati wapita njia wanaongezea viungo na vikolezo kazi itakamilika tu ni kwake mhusika kufungua macho na masikio kisha aachie ubongo wake ufanya kazi yake.
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,879
1,250
Wadau wa Jf naombeni mnisaidie nataka nianzishe jarida maalum la burudani na mziki. Wapi naweza kupata huduma ya gharama nafuu ya kuprint jarida hilo. Nategeme kutoa nakala 5000 awamu ya kwanza. Jarida nataka liwe coloured na liwe na page 30. Naombeni msaada wenu.

Ukikutana na wafanya tathmini wa kurasa za majarida au vitabu na namna binding itakavyofanyika watakuelewesha vizuri, inabidi kujua aina ya binding kama itahitaji single paper au folding paper. Kwa idadi ya page unazosema nadhani kutumia stitching ni bora na ni gharama nafuu zaidi.

Hivyo basi kama binding itafanyika kwa stitching, means stepple stitching, basi jarida lako litakuwa na kurasa 32. Inategemea na ukubwa wa jarida lako na mikunjo. Inawezakana ikachapwa katika karatasi mbili au nne.
Mkunjo mmoja kurasa
4
Mikunjo miwili kurasa
8
Mikunjo mitatu kurasa
16
Mikunjo minne kurasa
32

Karatasi
1 yenye mikunjo 4 utapata kurasa 32
Karatasi
2 zenye mkunjo 3 kila moja itakuwa na kurasa 16 x 2 = 32
Karatasi
4 zenye mikunjo 2 kila moja itakuwa na kurasa 8 x 4 = 32

Mpango huu wa binding ni kwa kutumia stepple machine kwa stitching na ni gharama nafuu ya binding, na huo ndio mchanganua wa kujua mpangilio wa kurasa.

Ukiwasilaina na wataalamu wa publishing kuna fomula za kutengeneza kurasa, ndio unaona wakati mwingine kitabu kinakuwa na kurasa tupu (blank pages) si kwa kukusudia, ila kutokana na mfumo wa utengenzaji hasa kwa mpangilio wa mikunjo.
 
Roga Roga

JF-Expert Member
Dec 20, 2013
645
500
Jamani wadau nashukuru kwa wote mliochangia katika mada hii, nitafanyia kazi mawazo yenu na pia address zote mlizonipa nitawasiliana nazo ili nipate pakuanzia.
 
bagain

JF-Expert Member
Jul 21, 2011
365
250
Ukikutana na wafanya tathmini wa kurasa za majarida au vitabu na namna binding itakavyofanyika watakuelewesha vizuri, inabidi kujua aina ya binding kama itahitaji single paper au folding paper. Kwa idadi ya page unazosema nadhani kutumia stitching ni bora na ni gharama nafuu zaidi.

Hivyo basi kama binding itafanyika kwa stitching, means stepple stitching, basi jarida lako litakuwa na kurasa 32. Inategemea na ukubwa wa jarida lako na mikunjo. Inawezakana ikachapwa katika karatasi mbili au nne.
Mkunjo mmoja kurasa
4
Mikunjo miwili kurasa
8
Mikunjo mitatu kurasa
16
Mikunjo minne kurasa
32

Karatasi
1 yenye mikunjo 4 utapata kurasa 32
Karatasi
2 zenye mkunjo 3 kila moja itakuwa na kurasa 16 x 2 = 32
Karatasi
4 zenye mikunjo 2 kila moja itakuwa na kurasa 8 x 4 = 32

Mpango huu wa binding ni kwa kutumia stepple machine kwa stitching na ni gharama nafuu ya binding, na huo ndio mchanganua wa kujua mpangilio wa kurasa.

Ukiwasilaina na wataalamu wa publishing kuna fomula za kutengeneza kurasa, ndio unaona wakati mwingine kitabu kinakuwa na kurasa tupu (blank pages) si kwa kukusudia, ila kutokana na mfumo wa utengenzaji hasa kwa mpangilio wa mikunjo.Nami nimejifunza mengi. natamani kuadvance kutoka stationery ya kawaida inayotumia canon IR series kwa printing and copying hadi kuanza kutumia machine ndogo za digital printing kama Konica minolta, Ricoh, Xerox.

Je, unaweza nishauri ni machine gani kati ya hizo inafaa?
 
chabusalu

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
7,803
2,000
kwa uzoefu wangu kwa vile unaprint nyingi inaweza kuwa kwenye 5,000 000 ( million 5 )
wewe utauza kwa 3,000 hivo utapata 15,000,000
ukiweka za kulipwa kutokana na matangazo unaweza pata 18,000,000
Duh! Biashara hii sio ya kuingia kichwa kichwa , na haiko hivi unavyoieleza. Ni ugonjwa wa moyo kama una hela ya mawazo si mahali salama pa kuwekeza!
 
Inaguresheni

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
294
250
Duh! Biashara hii sio ya kuingia kichwa kichwa , na haiko hivi unavyoieleza. Ni ugonjwa wa moyo kama una hela ya mawazo si mahali salama pa kuwekeza!
Umesema kweli mkuu.
Anaweza kufaidika hivi. Kwanza huwezi kupata jarida la kurasa 30. Either 28 au 32. Kitu cha Pili Inatakiwa uwe bega kwa bega na dizaina anayejua jinsi ya kuandaa kazi za offset machine. Usije ukaandalia jarida lako Photoshop. Program za vector ndio nzuri kufanyia kazi. Baada ya dizain Inatakiwa kutoa demo na kazi ya demo NI kuangalia mvuto Wa kazi, mpangilio wa kurasa, rangi zinamatch vipi, na muhimu kuliko vyote inaitwa proof reading. Soma taratibu usahihishe lugha, maneno vituo na vyote vifananavyo na hivyo.

Ushauri : Jarida lako NI jipya halijulikani hivyo usianze na kopi nyingi. Anza na 2000 kwanza mkuu ili upate guideline ya taste za watu.

Wazo zuri nakuunga mkono.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom