Ndugu zanguni
Jana wote hapa tuliona taarifa ya mauaji yaliyotokea huko mwanza ya aliekuwa mwenyekiti wa ccm.
Ninajua kila binadamu ana mapungufu yake na ikitokea hasira kwa mwanadamu anaweza fanya lolote na inaweza kuwa hasira zimesababishwa na upande wowote kati ya marehemu au wananchi.
Nguvu ya umma ni kuuana ?
Tuache masuala ya upelelezi kwa polisi na ninawasihi ndugu zangu huko tunakoelekea ni kubaya, hata kama una chuki na mtu ni vyema ukakaa kimya kuliko kuandika maneno ambayo hayatajenga hapa zaidi ya kubomoa
MODS, NAOMBA MUWE MNAPIGA BAN MTU ANAYETOA COMMENTS ZENYE UCHOCHEZI KWA JAMII
JITAMBUE!