Wadau: Dowans imechimbia kaburi CCM

Hii inanikumbusha kauli ya Dr. Kitila alipokuwa akisisitiza jambo (siku ya Kongamano la Wanafunzi - MAbibo) na kutamka neno 'zuzu'

Sikutarajia mtu mwenye hadhi ya Mtikila kuamini CCM na taasisi zake wanaweza kuongea jambo mtu mwenye akili sawasawa akaliamini.

Ni zuzu tu anaweza kuwaamini CCM na kauli zao
 
Chadema wamtiwisha JK deni la Dowans
Sunday, 23 January 2011 09:50

dk%20willbrodslaa1.jpg

Claud Mshana
KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa, amesema wanaopaswa kulipa deni la Dowans ni Rais Jakaya Kikwete na Kamati kuu ya CCM.Dk Slaa imetoa kauli hiyo siku moja baada ya Kikao cha Kamati Kuu ya CCM kubariki Dowans ilipwe Sh 94 bilioni kufuatia kampuni hiyo kushinda kesi katika Mahakama ya Biashara ya Kimataifa (ICC), dhidi ya serikali ya Tanzania.

Akihutubia katika Kongamano lililoandaliwa na Baraza la Vijana wa Chadema na kuwashirikisha vijana wa chama hicho walioko vyuo vikuu jijini Dar es Salaam jana, Dk Slaa alisema amepata taarifa kuwa wajumbe wa Kamati Kuu wakiongozwa na Rais Kikwete walikubali Dowans ilipwe na Serikali.

"Ni uzembe umefanyika katika suala hilo, mimi nasema alipe Rais Kikwete na Kamati Kuu ya CCM," alisema Dk Slaa huku akishangiliwa na mamia ya wanafunzi na wafuasi wa chama hicho waliofurika Viwanja vya Mabibo External.

Kuhusu hukumu hiyo, Dk Slaa alisema kuna mambo mengi ambayo yako kinyume na sheria lakini hakuna mtu anayejali kuyashughulikia.

Alitoa mfano wa taarifa zilizopo kuwa kesi hiyo haijawasilishwa mahakama kuu ya biashara kama inavyohitajika kisheria ili malipo yafanyike na kwamba kilichopelekwa ni viambatanisho vya kesi.

"Kuna utata mkubwa sana katika kesi hii, kwanza kesi yenyewe haijasajiliwa katika Mahakama Kuu kama inavyotakiwa, kilichowasilishwa huko ni Indices (Viambatanisho) za kesi, tunataka Mwanasheria Mkuu atupe maelezo," alisema Dk Slaa.

Alifafanua kuwa Kampuni ya uwakili ya Rex Attorney iliyokuwa mshauri wa Serikali wakati wa kuvunja mkataba huo, inapaswa itoe maelezo wakati huu Dowans inatakiwa kulipwa.
"Rex Attorney ni nani, aliishauri nini Serikali kuhusu kuvunja mkataba na anaishauri nini kuhusu kuilipa Dowans?" alihoji.

Hali ya Siasa
Akizungumzia hali ya siasa nchini, Dk Slaa alisema hadi sasa, nchi imechanganyikiwa na kusisitiza kauli yake kuwa nchi hii haitawaliki.

Huku akikatizwa na kelele za mara kwa mara kutoka kwa wanafunzi waliofurika katika viwanja hivyo, Dk Slaa alisema anashangazwa na jinsi serikali inavyozuia watu kuzungumzia masuala ya siasa.

"Ukitaka watu wasiongee siasa unataka nini, hii ni kasumba ya viongozi wasiopenda kufikiri, wanaolichanganya taifa na kusababisha migogoro mikubwa," alisema na kuongeza:
"Viongozi wa dini wanapokemea watu wanaotenda maovu katika siasa wanasemwa kuwa wanaingilia siasa, lakini Rais Kikwete alipowaita viongozi hao Kunduchi kuwaomba kura walikuwa hawaongei siasa?," alihoji.

Udini
Dk Slaa pia alitumi nafasi hiyo kuwaonya viongozi wanaoeneza maneno kuwa kuna udini nchini.

Alisema dhana hiyo inachochewa na viongozi dhaifu wanaotafuta hoja itakayomeza hoja za msingi za maendeleo ya taifa.

Dk Slaa ambaye alishika nafasi ya pili katika matokeo kura z urais kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita alisema anashangazwa na kauli za Rais Kikwete kuwa kuna harufi ya udini wakati hachukui hatua yoyote na wakati udini ni kosa la jinai kwa vile ni sawa na ubaguzi.

"Kama rais analalamika kuwa kuna udini na hachukui hatua, nani achukue hatua, hatujaona mtu yeyote aliyekamatwa kwa kuhubiri udini, Watanzania bado tunaishi kama ndugu tena kwa amani," alisema Dk Slaa.

Alitoa mifano ya mwaka 1987 kulipoibuka vuguvugu kubwa la udini, lakini aliyekuwa rais kipindi hicho, Mzee Ali Hassani Mwinyi, alichukua hatua za kuunda kamati kutoka madhehebu yote iliyoshughulikia kiina cha tatizo hilo na kulimaliza.

Alisema hakuwahi kusikia Rais mstaafu Mwinyi akikemea udini majukwaani na kushangaa kauli za Rais Kikwete juu ya kuwepo kwa udini ambao hakuna hata mmoja aliyechukuliwa hatua za kisheria.

Vyuo vikuu na Siasa
Akizungumzia vyuo vikuu kujihusisha na siasa, Dk Slaa alisema ni jambo la ajabu kwa wanafunzi kuzuiwa kushiriki siasa wakati vyuo vinawafundisha siasa.

"Mwalimu Julius Nyerere alianza harakati za ukombozi akiwa chuoni, kwenye vyuo ndiko kunakopikwa watu wanaofikiria, ndio kituo cha mawazo na hoja za maendeleo, tunataka viongozi makini na si viongozi wa propaganda," alisema Dk Slaa na kuongeza:
"Nchi isiyotaka kuchukua changamoto kutoka kwa vijana itakuwa imepotea. Wakati umefika vyuo viwe ni msaada kwa nchi na wanafunzi wanatakiwa wawe huru".

Kiongozi huyo wa Chadema aliituhumu Bodi ya Mikopo kuwa imejaa upendelea na kuongeza na kwamba alishawahi kutoa mapendekezo ivunjwe na kuundwa mpya.

Akizungumzia viongozi wa nchi kupewa shahada za heshima, Dk Slaa alisema inasikitisha kuona kuwa chuo ambacho hata hakina program ya Shahada Uzamili, kinakuwa na sifa ya kutoa shahada ya heshima.

"Degree (shahada ya kwanza) hazigawanywi kama karanga, haya ni matokeo ya kupendeleana, chuo chenyewe kina matatizo chungu nzima, wakuu wake wanatoa ‘degree' hizo ili waendelee kunufaika," alisema huku akishangiliwa na wanafunzi hao waliokuwa wakitamka "UDOM...UDOM....UDOM...." wakimaanisha chuo Kikuu cha Dodoma.

Mabere Marando
Kwa upande wake, Wakili wa Kujitegemea na mwanachama wa Chadema, Mabere Marando, alisema suala la katiba mpya kwa sasa halina mjadala tena.

"Katiba mpya, tupende tusipene, Kikwete apende asipende, CCM ipende isipende, lazima iandikwe upya hilo si suala la mjadala tena," alisisitiza Marando a kuongeza:
"Hoja iliyopo ni je viongozi walio madarakani wanasoma alama za nyakati au wapo tu kama kisiki wanasubiri wafagiwe na upepo".

Marando pia aliponda hali ya kupingana iliyojitokeza kwa mawaziri, baraza la vijana wa CCM kupingana na wazee kuwa ni ishara kuwa chama hicho kinaelekea kufa.

"Chama chochote cha siasa kinazaliwa, kinakua, kinazeeka na kinakufa, CCM sasa inakufa. Hebu kisaidieni kife bila ya sisi kupata madhara," alisema Marando ambaye ni mmoja wa waasisi wa mageuzi nchini.

Kuhusu mabadiliko ya katiba, Marando alitoa mfano wa katiba mpya ya Kenya kuwa ina vipengele ambavyo ni lazima katiba yetu iwe navyo.

Alitoa mifano ya Ibara ya 71 ya Katiba ya Kenya kuwa masuala ya madini lazima yaidhinishwe na Bunge kabla ya serikali kutia saini mkataba wowote ule.

Alisema pia Ibara ya 152 ya katiba hiyo kuwa inamtaka Rais kuchagua baraza la mawaziri nje ya bunge na wabunge watakuwa na kazi ya kukubali au kukataa uteuzi wake.


John Mnyika
Naye Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika, alionya kuwa iwapo viongozi walioingia madarakani kwa hila hawatabadilika, nchi inaweza kugeuka na kuwa kama Tunisia.

Joseph Mbilinyi (Sugu)
Kwa upande wake Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu Sugu aliyekuwa kivutia kikubwa katika kongamano hilo, aliwataka wanafunzi wa vyuo vikuu kusoma kwa bidii na kuja kuikombia nchi.

Sugu ambaye alilazimishwa na wanachuo hao kuongoza kuimba wimbo wa taifa wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo, alisema amekuwa mstari wa mbele katika kupigia kelele matatizo yanayowakabili wanafunzi vyuoni na kuwasisitiza kusoma ili watumie elimu yao katika siasa za kweli na si propaganda.


Kutoka Dodoma, Israel Mgussi na Masoud Masasi wanaripoti kuwa,
Chadema mkoani Dodoma kimefanya maandamano ya amani kuunga mkono maandamano yaliyofanywa na chama hicho mkoani Arusha Januari 5, mwaka huu kupinga mchakato wa uchaguzi na matokeo ya Meya wa Jiji la Arusha.


Katika maandamano ya jana ambayo mamia ya wafuasi wa chama hicho walijitokeza Chadema ilitoa tamko la kulaani Jeshi la Polisi kwa madia kuwa linaendelea kuwakumbatia waovu wanaoitafuna nchi kwa kuwatisha na kuwaua raia wasiokuwa na hatia.


Mkurugenzi wa Oganizesheni na Mafunzo wa chama hicho taifa, Benson Singo Kigaila ambaye ndiye alipokea maandamano hayo katika Viwanja vya Barafu mjini hapa alisema Tanzania na nchi tajiri lakini inashindwa kuendelea kutokana kushamiri kwa ufisadi.


Alisema hata askari polisi ambao wamekuwa wakitumiwa na baadhi ya watu wasioitakia mema nchi, wamekuwa wakifanya hivyo kutokana na kutotambua umhimu wa ustawi wa taifa lao.


"Ndugu zangu, nchi hii mali yetu, hatujaikodisha,hatuwezi kuvumilia maovu yanayoendelea,uchaguzi wa Arusha lazima urejewe upya,l azima wananchi tuwe tayari kupigania uhuru wetu, tunafahamu hata maauaji yaliyotokea kule Arusha haikuwa bahati mbaya,"alisema Singo.


Katika maandamano hayo ambayo yalianzia ofisi za chama hicho mkoa kupitia Soko Kuu la Majengo,Hospitali ya Mkoa, Barabara ya Morogoro na kuishia Viwanja vya Barafu yaliongozwa na askari polisi waliokuwa wakilinda usalama.


 
Hii inanikumbusha kauli ya Dr. Kitila alipokuwa akisisitiza jambo (siku ya Kongamano la Wanafunzi - MAbibo) na kutamka neno 'zuzu'

Sikutarajia mtu mwenye hadhi ya Mtikila kuamini CCM na taasisi zake wanaweza kuongea jambo mtu mwenye akili sawasawa akaliamini.

Ni zuzu tu anaweza kuwaamini CCM na kauli zao

Na kweli kwa mtu ambaye anaweza kusikiliza kauli za CCM tunaweza kusema ni zuzu maana hakuna jambo ambalo CCM unaweza kuwaamini siku hizi
 
Mtikila hapo amechemsha.......kwa sababu hawa UVCCM bado hawajatambua ya kuwa kiini cha DOWANS ni ufisadi ambao JK anauendesha pale Ikulu..........................................kwa hiyo kauli yao inaficha maovu na kamwe haiwezi kuisafisha serikali wakati JK anendeleza kuigeuza Ikulu kuwa ni pango la mafisadi........................................

Majawabu ya ufisadi ambao JK anauendesha pale Ikulu ni raia wote kuingia mtaani kwa maandamano yasiyo na kikomo kama yale ya Tunisia kushinikiza JK aachie ngazi na asipofanya hivyo................................kulishinikiza Bunge limshtaki, limchunguze na hatimaye kumfukuza kazi..................................

Vinginevyo tutaendelea kutwangfa maji kwenye kinu tu.........................................na hata ukiwatoa akina Ngeleja na wengineo bado mzizi wa ufisadi ambao ni Jk mwenywe utaendelea kuzalisha wafanikishaji wengine wa ufisadi tu...........................na wala siyo vinginevyo.......................

Ng'oa mizizi kwanza
 
Pia kuna hukumu iliyo tolewa na mahakama kuu miaka mingi ya nyuma kuhusu mhindi mmoja kwa jina la la vallambhia (nadhani) ambaye alitoa huduma ya ununuzi wa vifaa kwa ajili ya jwtz. Hadi leo serikali imekaidi kutekeleza hukumu hiyo (nadhani sasa vallambhia ni marehemu). Hukumu nyingine ambayo ilitolewa na mahakama kuu ni kuhusu malipo halali ya wafanyakazi wa Benki Kuu walioachishwa kazi isivyo halali. Serikali/Benki kuu imepuuzia hukumu hiyo na watumishi hao wanazidi kuzeeka katika umasikini. Dowans hadi chama cha....... kinasisitiza malipo yafanyike. Kweli bongo/duniani kuna haki.
 
Hii inanikumbusha kauli ya Dr. Kitila alipokuwa akisisitiza jambo (siku ya Kongamano la Wanafunzi - MAbibo) na kutamka neno 'zuzu'

Sikutarajia mtu mwenye hadhi ya Mtikila kuamini CCM na taasisi zake wanaweza kuongea jambo mtu mwenye akili sawasawa akaliamini.

Ni zuzu tu anaweza kuwaamini CCM na kauli zao

Mtikila sasa amechoka...............................Hana mchango zaidi ya ile misemo yake ya ma********* kuwalaumu wahindi kwa ufisadi ambao viongozi wetu kama JK wanaupika....................................tena wanaupika kwenye madhabahu iliyopo pale Ikulu ambako Nyrere alisema ni patakatifu................................
 
mtikila is the real deal....the man...the mzalendo wa kweli.....ANAPONGEZA PANAPOSTAHILI NA ANAKOSOA PANAPOSTAHILI......si mda wote kukosoa bila sababu na si muda wote kupongeza bila sababu.....ASTAHILIYE TUZO APEWE TUZO NA ASTAHILIYE ADHABU APEWE ADHABU and not vice versa
bravo kiboko ya ma.GA.BA.CHO.LI....I REMEMBERE YOU IN EARLY AND MID 1990's MA.GA.BA.CHO.LI. WALILALA MBELE
 
Hii inanikumbusha kauli ya Dr. Kitila alipokuwa akisisitiza jambo (siku ya Kongamano la Wanafunzi - MAbibo) na kutamka neno 'zuzu'

Sikutarajia mtu mwenye hadhi ya Mtikila kuamini CCM na taasisi zake wanaweza kuongea jambo mtu mwenye akili sawasawa akaliamini.

Ni zuzu tu anaweza kuwaamini CCM na kauli zao

Mkuu mimi naona tutakuwa tunafanya makosa kumpuuza mtikila,alichokifanya ni kitendo cha ujasili na anapaswa kupongezwa.Hata UVCCM pia wanapaswa kupongezwa kwa kitendo chao cha ujasili,katika kujenga hoja zetu siku zote tunapaswa kuwa objective,biasness haitotufikisha popote.Kweli CCM ni tatizo na kikwazo cha maendeleo ya nchi hii,lakini anapojitokeza mmoja mmoja ama ndani chama hicho au njee ya chama hicho ambaye anapinga uovu hadharani,sisi kama wapiganaji wa kweli ni lazima tuwapongeze!!
 
Alichokifanya Mtikila ni kuwagonganisha ccm na uvccm, ka kamwe haamini hata yeye kuwa uvccm wanamanisha kweli kupinga malipo Dowans. Ndiyo maana anaihusisha Dowans na mafisadi yenye kiini kwa JK, ambapo uvccm wanamuona kama asiye husika na ufisadi (contrast). Kauli ya Mtikila ni ya "kifalsafa" kuchimba undani wa uvccm na baba yao ccm juu ya mstakabari wa Dowans ili waje wale matapishi yao wenyewe mbele ya umma wa watanzania baadae.
 
Kama kuna kikundi kinachotakiwa kulipwa haraka na sisi walipakodi tunaafiki kwa kauli moja, ni hawa wazee waliotumikia miaka mingi huko nyuma kutujengea hili taifa zuri la Tanzania na Arika Mashariki kwa ujumla enzi hizo, kwa mazingira magumu sana na bila kula kufanyia taifa hili UFISADI wowote kama Dowans leo hii.
 
UVCCM baba yao mmoja mama yao mmoja hapa mtikila kachemka

Watoto wa baba mmoja na mama mmoja si lazima wafanane tabia,UVCCM wametoa tamko la maana sana ingawa waliniuzi kile kipengele cha kumtukana Dr Slaa!!
 
MI NADHANI KATIKA MALIO YA MADAI HAYA ITUMIKE FOMULA YA ...FIFO.....na sio LIFO bravo UVCCM NAUNGA MKONO HOJA YA UVCCM
 
UVCCM wataka wayumbisha chama washughulikiwe


na Ghisa Abby, Morogoro


amka2.gif
JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Morogoro, wamemuomba Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, kuwawajibisha na kuwachukulia hatua wale wote wanaohusika na kukiyumbisha chama kwa maslahi yao binafsi. Tamko hilo lilitolewa jana na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Morogoro, Jonas Nkya, baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza la vijana mkoa ambapo pia jumuiya hiyo iliunga mkono tamko la kamati ya utekelezaji ya UVCCM Taifa la kukataa kampuni ya Dowans kulipwa mabilioni ya fedha.
Nkya alisema wao kama vijana wanaunga mkono tamko la wenzao, lakini wanamuomba Rais Jakaya Kikwete kuhakikisha anawachukulia hatua wanachama wenye kukiharibu chama na kutokitakia mema.
Alisema Chama cha Mapinduzi kwa sasa kina matatizo na ni kutokana na watu wachache wenye uelewa mdogo, wivu, tamaa pamoja na chuki binafsi zinazokipeleka chama kuonekana kibaya hususan kwa vijana wengi na hata wasomi.
"Sisi kama vijana wa taifa hili tunaendelea kukemea kwa nguvu zote makundi ya viongozi wa juu yasiyomalizika ndani ya chama na yanayotupeleka pabaya na hata wakati mwingine kuwahusisha vijana wenzetu kwa maslahi yao. Tunachoomba ikiwezekana CCM iwaweke kando wale wote wanaohusika kwa njia moja ama nyingine," alisema Nkya.
Aidha, mwenyekiti huyo alisema vijana wa Morogoro wanaomba suala la Richmond na Dowans lirudishwe bungeni ili wabunge waweze kutoa maamuzi zaidi.
 
Nkya alisema wao kama vijana wanaunga mkono tamko la wenzao, lakini wanamuomba Rais Jakaya Kikwete kuhakikisha anawachukulia hatua wanachama wenye kukiharibu chama na kutokitakia mema.
Alisema Chama cha Mapinduzi kwa sasa kina matatizo na ni kutokana na watu wachache wenye uelewa mdogo, wivu, tamaa pamoja na chuki binafsi zinazokipeleka chama kuonekana kibaya hususan kwa vijana wengi na hata wasomi.

Hawa UVCCM ni bomu sana hadi leo hawajaui ya kuwa JK ndiye fisadi nambari one sasa kwa kutolielewa hilo wanarudi kwa fisadi nyangumi aweondolee mafisadi.................................hawa UVCCM kweli ni sikio la kufa ambalo kamwe haliwezi kusikia dawa.................
 
Ingekuwa vyema kama wanajamvi wangesoma kwanza kauli ya UVCCM ndo wangejua kwamba hoja ya Mtikila ni uzuzu mtupu kupongeza UVCCM maana kauli zao zote zilikuwa zimeoza na siamini kama hao ndo vijana ambao wanalilia kuliongoza taifa hili. UVCCM walisema kwamba Dowans isilipwe maana hawajui marithishano kati yake na Richmond. Kwamba kamati ya Mwakyembe imelidanganya bunge na kusababisha uvunjwaji wa mkataba huo uliosababisha Dowans wadai fidia so wasilipwe. Kwamba Mwakyembe na Sitta wawajibishwe kwa kauli zao juu ya Dowans kutokulipwa na ikumbukwe kwambo mwisho walisema Dowans isilipwe sawa na kina Sitta na Mwakyembe. Sasa inapotokea mtu akasifia UVCCM nitamshangaa sana kwa kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom