cocastic
JF-Expert Member
- Nov 30, 2019
- 122,266
- 201,312
Nipoo udugu. [emoji23][emoji23][emoji23]Udugu upo?? [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Nipoo udugu. [emoji23][emoji23][emoji23]Udugu upo?? [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Vizuri kama unafahamu na kulitii hili.Nafahamu mkuu lakini naona kama nguvu kubwa inatumika kukumbusha wajibu wa wanawake kuliko wa wanaume wakati dunia ya leo jinsia zote zimepwaya, mwisho wa siku tafsiri yake inaonekana kwamba wanawake tu ndio wenye makosa na ndio wanaotakiwa kubadilika, huku wanaume wakionekana wako sawa kwa wanayoyafanya hivyo wao waendelee tu jambo ambalo linawaumiza wanawake na hawawezi kukubali hasa wa kizazi hiki kwahiyo inatupasa tuchague moja
Magazeti ni matokeo ya maelezo marefu kukuelezea wewe ambaye unamix mambo. Shida yako ni unalinganisha umuhimu wa Ndoa kwa mwanamke na mwanaume kuwa sawa wakati sote tunajua mahitaji ya mwanaume ni tofauti na ya mwanaume sasa wanakuwaje na uhitaji sawa?Mkuu yani magazeti yote haya uliyoshusha nikajua labda utakuwa umeelewa hoja yangu in deep ila badala yake naona lawama malalamiko na kunilisha na kuniwekea maneno, maybe let me put this right unajua tofauti yangu na wewe ni kwamba mimi nasema ndoa ina umuhimu kwa wote ila wewe unasema ndoa ina umuhimu kwa mwanamke tu na siyo kwa mwanaume, mimi nilichokuwa nafanya ni kukuonesha umuhimu wa ndoa na kwa mwanaume pia na nimekuwa nikisema wanaume ndio wanahitaji zaidi ndoa kuliko wanawake lakini hakuna mahali niliposema wanawake hawahitaji ndoa kabisa na kama papo nioneshe ili tuweke mizani sawa
By the way kitendo kinachohusisha jinsia mbili kinakuwaje muhimu kwa jinsia moja halafu kisiwe muhimu kwa jinsia nyingine ndipo mnapofeli hapo ninyi wanaume mnaosema kwamba ndoa ina umuhimu kwa wanawake ila siyo kwa wanaume, inatakiwa either iwe na umuhimu kwa wote au isiwe na umuhimu kwa wote and that depends on how one defends their points huwezi kusema ndoa ina umuhimu kwa wanawake na siyo wanaume, kana kwamba wanawake wanaoana na viumbe wengine na wanaume wanaoana na viumbe wengine wakati ni hizi jinsia mbili zilizopo ndio zinaoana
Yani confidently kabisa unasema kuwa umuhimu wa ndoa kwa mwanamke ni financial support kwahiyo leo hii ndio mnakubali na mnaona sawa mwanamke kuingia kwenye ndoa kwa lengo la kutafuta financial support, siyo ninyi mnaoanzisha mada kila siku za kulalamika kwamba siku hizi wanawake hawana mapenzi ya dhati wanaingia kwenye ndoa kwa sababu ya pesa na mali wamekuwa ombaomba na matapeli, sasa kama mnajua kwamba wanawake hawana kingine cha kufuata kwenye ndoa zaidi ya financial support kwanini sasa mnalalamika wanapoingia kwenye ndoa kwa lengo hilo mlitaka waingie kwa lengo gani ambalo ni tofauti na hilo
Mimi nilitegemea utaniambia umuhimu wa ndoa ambao ni general na universal ambao kila mwanamke bila kujali utaifa, dini, kabila wala hali ya kiuchumi atauona lakini badala yake unaniletea habari za wazungu mara waarabu mara sijui mimi nina pesa na financial support (kana kwamba unafahamu niliyopitia) sijui kuna watu hawana pesa wana maisha magumu na blah blah, asee mbona unarukaruka kama bisi ni umuhimu gani huo ambao unachagua aina ya watu yani ni kwanini mpaka mwanamke awe masikini au awe ameshatendwa ndio aone umuhimu wa ndoa dont you feel that something is wrong somewhere au ni mimi peke yangu ndio nahisi hivi, kwahiyo ina maana leo hii nchi zote masikini nazo zikiendelea na wanawake wote wakaweza kujitafutia pesa na kujisimamia kiuchumi kama kwenye nchi zilizoendelea maana yake ndoa ndio basi tena au unajaribu kusemaje
Hata hivyo nafurahi hujapinga ule umuhimu wa ndoa kwa mwanaume ambao ni wa kisaikolojia and the good thing about pyschology is that it is a general and a universal thing, mwanaume yeyote yule haijalishi ni tajiri au masikini katendwa au hajatendwa ni lazima ahitaji ndoa tena uhitaji wa ndoa kwa wanaume siyo ule wa kushurutishwa na jamii kwa sababu za kimaumbile au kiuchumi kama ilivyo kwa wanawake bali uhitaji wenu ni natural, na kama nilivyokuambia wanaohitaji zaidi hizo mommy care na romantic gestures ni wanaume hizo daddy care ulizonitajia wewe naona ziko financially zaidi kuliko psychologically, and yet uko hapa unasema eti mwanaume anaoa ili tu kutimiza wajibu aliopewa na mungu ingekuwa hiyo ndio sababu yenu pekee ya kuoa basi kwa tabia hizi za wanawake wa kizazi hiki mngekuwa mmeshaacha kuoa kitambo sana, ila ndio kwanza ndoa zinazidi kufungwa kila siku na malalamiko kwenye ndoa kutoka upande wa wanaume yanazidi kuongezeka kila siku
Lawama ni matokeo ya kile kilichofanyika tofauti na matarajio huku chanzo ukiwa ni wewe! Ili usilaumiwe basi hakikisha kila wakati unatenda sawasawa na matarajio japo hilo haliwezekani maana wewe sio malaika! Kulaumiwa ni sehemu ya kuwajibika kwa ulilofanya!Huu ugonjwa sina. Na ukijikoroga kuniambia katika SMS like uko kimya sana hunitafuti na bla bla.. my dia hiyo text utajijibu mwenyewe maana me hapo ndio nakuwa nimemalizana na wewe.
Nachukia lawama 😂😂
Ukitaka kunivuruga, we nilaumu tu
Unajua aidha unapenda kubishana au unachukulia vitu simple sababu haujui kinachoendelea uraiani.Mkuu mimi nafahamu ndoa ni muhimu kwa kila jinsia ila ninaopingana nao ni hawa wanaosema eti ndoa ni muhimu kwa wanawake na siyo kwa wanaume, na huku hawana hoja za maana wanazotoa zaidi ya ujinga na upotoshaji waliolishwa na mfumo dume tu na toka enzi za wazee wetu watu wamekuwa wanadanganywa na wanaamini hivyo, ila sasa meza zimegeuka ndio tumeanza kuona hali halisi kwamba ndoa ni muhimu kwa wote ila wanaume wengi wanajifanya hawataki kukubali hili
@Jadda anahisi hapa ninabishana nae. Anachokizungumza ni nadharia ya usawa kati ya mwanaume na mwanamke eneo la ndoa akiamini wote wanataka ndoa kwasababu za kufanana.mkuu unadili na saikopathi kama mada husika
Wapo ambao hawana kabisa hata moja sababu wapo makini na tabia hizi chafu. Hizi ni tabia mbaya na kuna mabinti anabeba zote hizi na ndio hawa wanaliwa na kutupwa.Hivi yupo mwanamke ambaye Hana sifa hata Moja Kati ya hizo zilizotajwa na mleta mada?
Kama yupo mnifahamishe tafadhali.
Wanaume wanastyle yao ya kuwanyoosha wanawake ili kuwakumbusha wajibu wao. Sasa kosa mnalofanya wanawake ni kujibu mashambulizi kwa tit for tat. Kosa kubwa.Nafahamu mkuu lakini naona kama nguvu kubwa inatumika kukumbusha wajibu wa wanawake kuliko wa wanaume wakati dunia ya leo jinsia zote zimepwaya, mwisho wa siku tafsiri yake inaonekana kwamba wanawake tu ndio wenye makosa na ndio wanaotakiwa kubadilika, huku wanaume wakionekana wako sawa kwa wanayoyafanya hivyo wao waendelee tu jambo ambalo linawaumiza wanawake na hawawezi kukubali hasa wa kizazi hiki kwahiyo inatupasa tuchague moja
11. Mwanamke ambaye anaanza anakulaumu kuwa hujajibu sms yake na ukimuambia hujaiona anaituma muda huohuo. Na sms yenyewe anakuomba pesa au kitu fulani.Sociopath ni mwendawazimu au mtu asiye na utimamu wa akili yake kufanya kazi sawa sawa kutokana na kuathiriwa na changamoto za kimaisha kama stress, ugumu wa Maisha, madeni, malezi mabovu na kadhalika.
Kuna hawa wadada eneo la mahusiano wanatabia zifuatazo mimi huwa nawaona kama sio timamu kichwani na nikiona hizi tabia huwa najiweka mbali nao maana najua huyu sio mzima kichwani so hakuna la maana tutaweza kufanya pamoja ukitoa kupelekeana moto.
1. Mwanamke ambaye anakwambia yeye muda wote anawaza pesa. Utasikia "yaani nisipokuwa na pesa natamani kupiga kelele nachanganyikiwa, mimi napenda sana pesa". Nikiona tu hizi kauli najua hapa hazijatimia huyu anaweza lala hata na baba yako au rafiki yako kupata anachotaka.
2. Mwanamke ambaye analalamika kuwa haumtafuti ila cha ajabu yeye pia hakutafuti. Mtu ambaye analalamika kufanyiwa kile ambacho anamfanyia mwenzake tafsiri yake ni kuwa amekosa uwezo wa kujitathimini so utendaji wa akili yake haupo kamili.
3. Kuna wale wanawake ukikaa nae muda wote yeye ni kukuonyesha kuwa hana amani anatakiwa kufanyiwa jambo ili ajisikie vizuri kama kutolewa out, kununuliwa zawadi na mbaya zaidi anachotaka yeye ni material things bora hata atake labda kukumbatiwa au kupelekewa moto ila sivyo.
4. Mwanamke ambaye akikasirika au mkipishana hatazami kauli zake sawa sawa. Anaropoka muda mwingine kauli ambazo baadae ukimuuliza kwann ulisema hiki anasema ilikuwa ni hasira sikumaanisha. Huyu sio mzima kichwani.
5. Mwanamke ambaye mkipishana kidogo anakublock au anapenda kususa au hapendi kujadili anawahi kukatisha mjadala huku akijua wazi mna misunderstanding. Mfano umetumiwa sms yenye utata au kuna mdada amekuona nae au simu ilizima chaji usiku akakutafuta asikupate then ukataka kujielezea kumpa ufafanuzi yeye anakukatisha huku kafura na kukuonyesha anachokiamini ndicho ukweli sio unachotaka mwambia. Na akikaa na rafiki yake, au ndugu zake au mama yake anarudia kile kile anachokijua badala ya kusikiliza upande wako ili kubalance story. Mimi kwangu huyu ni mwendawazimu hayupo timamu.
6. Mwanamke ambaye hampo pamoja kinyumba, mkipishana akaenda kulala bila kuhakikisha amekubembeleza au kukutuliza moyo kwa kauli ili kuonyesha anakujali na hataki ulale ukiwa unasononeka au umekwazika au unahasira. Huyu mwanamke muombee hata ugumba maana si shetani kama wewe mume wake mtarajiwa hajui kujali hisia zako huyu hana utu watoto atawapa vipi upendo wa mama? Care ya mama inaanza kwa mume, then watoto ndio itazidi, ni kama baba ambaye ameshindwa mtunza mke ataweza tunza familia ya mama na watoto wake?
7. Mwanamke ambaye anaweza soma sms yako halafu akapiga kimya ila ukimtumia ujumbe kumuonyesha kuna zawadi au pesa au kitu unataka mpa anarespond bila kupoteza sekunde, huyu anaweza kuwa hata ameshatoa mimba ya miezi 4, sababu mtu timamu hawezi mkalia kimya mtu anayesubiria kujibiwa sms upande wa pili, huyu ni sociopath.
8. Mwanamke ambaye kutoa mimba na ujauzito kwa visingizio kama iliingia bahati mbaya, kumkomoa mwanaume, kulinda ndoa, na sababu yoyote ile, mtu anaye amua kuua kiumbe ambacho kimejiumba ndani ya mji wake wa uzazi yaani damu yake, huyu anaweza kuja kukuua siku akitaka kitu kwako kama mali au akiwekewa dau la kukuua apewe pesa hashindwi. Huyu ni sociopath na mkalie mbali.
9. Mwanamke ambaye kila ukiongea nae anakuletea story za shida na unaona kabisa huyu anazitengeza muda mwingine ila anachofanya ni maintain aina ya mawasiliano ambayo ukiongea nae iwe ni kama baba anaongea na binti yake ili amwambie shida zake tu na sio kuongea mambo ya msingi. Yaani yeye hajali unacho au hauna ila ni mkiwasiliana tu anaanza kukuelezea matatizo mara anaumwa, mara simu mbovu, mara mama anaumwa, mara nadaiwa. Yaani hawezi hata kukujulia hali na kutaka kufahamu kama upo salama au unachangamoto gani ni yeye na shida zake kwanza na ukimtatulia anapiga kimya hakuna shukrani wala nini. Huyu ni mwendawazimu.
10. Mwanamke ambaye haogopi kuonekana au kushobokewa na wanaume wengine mbele ya mwanaume wake. Anafurahia kushobokewa na hapati ile sympathy au remorse kuwa mpenzi wangu ataumia au atajiskia dhaifu au ataniona kama sijamuweka juu ya wanaume wote. Huyu sio mzima kichwani ana matatizo ya akili.
11. Mwanamke ambaye mwanaume wake akiwa na changamoto za kiuchumi ila huwa siku zote anampa sapoti yeye ila siku kadhaa za kukwama mwanamke anasimamia msimamo kuwa mwanaume anatakiwa apambane na hampi ile comfort na care ya kumpa nguvu mpya ile feeling ya "i got you boo, don't worry mommy is here for you, you will get back when you are strong". Ukiona mwanamke hana hii anakuchenjia ukiwa vibaya kwa kisingizio kuwa wewe ni kidume, haraka sana sogea mbali huyu sio mzima ni mwendawazimu.
12. Mwanamke ambaye analingana na yule wa namba 10 pale ila afikie hadi hatua ya kuwa na sexual intercourse na wanaume kwa usiri huku akimuenjoy mwanaume aliyenae bila kuwazia nini kitatokea siku akigundua. Huyu ni sociopath tena anaweza kuwa ni zaidi ya sociopath anaweza kuwa ni psychopath.
Tabia ni nyingi ila nimeweka hizi chache for the sake of noticing them na najua wanaume wengi hawa mshakutana nao au kuna wadada wanajua wapo na hizi tabia. Go and seek therapy.
Kabeeeesa lo
Magazeti ni matokeo ya maelezo marefu kukuelezea wewe ambaye unamix mambo. Shida yako ni unalinganisha umuhimu wa Ndoa kwa mwanamke na mwanaume kuwa sawa wakati sote tunajua mahitaji ya mwanaume ni tofauti na ya mwanaume sasa wanakuwaje na uhitaji sawa?
Kama ni sawa unajua wanaume huwa wanataka mke zaidi ya m'moja je, why wanawake huwa hawapo tayari kwa hilo?
Umuhimu wa kitu huwa unapimwa na nani ana benefits nyingi kumsinda mwenzake. Mfano ni kama mtumwa na bwana wake enzi za utumwa nani alifaidika zaidi ya mwenzake.
Au tutolee mfano wa eneo la ajira, wewe unapoajiriwa kwenye kampuni wanayokulipa mshahara laki 6 huku gharama zako kwa mwezi ni laki 5 ila unaitengenezea kampuni mamilioni kila mwezi , utasema hapo ni wewe unafaidika au ni kampuni ndio inafaidika kupitia wewe hata kama kuna pesa unapata kama mshahara?
Huo ndio ukweli kwamba ulimwengu wa maisha ya kisasa security anayoweza kuprovide mwanaume kwa mwanamke wake ni kupitia financial support, sababu everything is paid through money, ataprovide vipi sehemu ya kuishi, chakula, mavazi, afya, entertainment, kulea watoto bila kuwa na financial support kwa mwanamke, ARE YOU THAT NAIVE AND IGNORANT?
Nani kalalamika kuhusu mwanamke kupewa financial support cha zaidi wanaume hulalamika gold digging habits kutaka kuexploit mwanaume au kumtapeli kwa kutumia ulaghai wa mapenzi. Hiyo hata kaka yako hautapenda afanyiwe mbona unajitoa ufahamu wewe?
Mahitaji ya wanawake yanatofautiana kulingana na mazingira tofauti. Mfano mwanamke wa kiarabu hawezi kuomba wigi ila wa kiafrika ataomba pesa ya wigi. Mwanamke wa kibrazil hawezi omba abaya sababu hana huo utamaduni wa kuvaa abaya ila wa kituruki ataomba abaya maana ni sehemu ya culture.
Mwanamke wa kiafrika hawezi omba mashine ya kufulia nguo sababu afrika hatuna huo utamaduni tunafua na mikono ila wakizungu hiyo ndio culture yao. Hivyo basi mahitaji wa wanawake katika kuwaprovide na wanachohitaji yanatofautiana across different cultures.
Bado hoja yangu umeshindwa kuielewa kwasababu kama nilivyosema you sound young and without experience eneo la mahusiano. Kama ungejua mengi basi usingeongea haya unayoongea. Na ninakuonea huruma sababu you think hii ni debate kama ya "education is better than money" ndio maana unasoma kujibu sio kuelewa.
Umeshawahi kujiuliza mwanaume akitafuta utulivu nje ya ule anaotafuta kwenye ndoa huwa anafanya vitu gani? Ukiweza kunijibu then tutaweza kuelewana nani anahitaji ndoa zaidi kati ya mwanamke au mwanaume?
Unajua aidha unapenda kubishana au unachukulia vitu simple sababu haujui kinachoendelea uraiani.
Shida yako unaforce kuwa mahitaji ya ndoa kwa mwanaume ni sawa sawa kama kwa mwanamke jambo ambalo si kweli na sababu zipo.
Mwanamke ndoa kwake ni source ya Maisha mwanaume kwake ndoa ni purpose ya Maisha meaning nje ya Ndoa mwanaume atapata shida kuwa na purpose ya kuishi fulfilling life na mwanamke nje ya ndoa atastruggle kuwa na maisha stable na ya amani.
Nimekupa mifano kule juu umesema ni blah blah jambo ambalo linadhihirisha kuwa hakuna unachoelewa juu ya Maisha ya ndoa zaidi ya story za inspiration za mafeminist ulizojazwa.
Nimekuuliza huku mtaani unajua kuna wadada wanateseka na kausha damu, unadhani wanapenda kuchukua hizo kausha damu? Ni kwasababu hawana ile financial support ambayo ndio mwanaume analeta katika maisha ya mwanamke (kitu ambacho unaonekana hupendi sababu wewe Jadda ni chronic feminist). Sasa unabisha je uhalisia ni upi kwani wewe haujui toka enzi na enzi kuwa wanawake wanaishi na wanaume kwaajiri ya mahitaji gani kama sio security na affection, sasa why uje useme hapa kuwa tulingana sawa sawa kimahitaji kwenye ndoa?
Mfano wewe unaweza kuishi na mwanaume wako wa ndoa mkazaa watoto watano, na tokea mtoto wa kwanza usimamie show kwa 100% bila mwanaume kutoa hata mia, halafu uweze kuwa na haiba ya kike kwa mume wako bila kukizana nae wala kumwambia umechoka yaani apate mahaba yako ile ya 100% kwa miaka hata kumi, je unaweza hii?
Kama hauwezi then why sasa unabisha kuwa mwanamke anahitaji ndoa kumshinda mwanaume?
Hivi ni kwanini unalazimisha kunilisha na kuniwekea maneno hebu nioneshe ni wapi niliposema mahitaji ya ndoa kwa mwanaume na mwanamke ni sawa, hivi kati ya mimi na wewe ni nani anayebishana kwa mihemko bila logic au wewe ndio umeamua kupinga bila sababu ili upate hoja mpya baada ya kuona umeshindwa zilizopo mezani, hadi sasa umeshanisingizia mambo mengi mara nimesema ndoa haina umuhimu kwa wanawake, mara nimesema mahitaji ya ndoa kwa wanawake na wanaume ni sawa, mara mimi naandika hivi kwa sababu sijafika umri fulani, mara mimi nina financial support, yani sioni hoja yako zaidi ya ad hominem attacks tu, kwenye mijadala kama hii jitahidi kuepuka personal attacks ni ishara kwamba umeshindwa hoja, mbona mimi hakuna mahali nimekuattack wewe kwamba unaandika hivi kwa sababu una hiki na kile au uko hivi na vile@Jadda anahisi hapa ninabishana nae. Anachokizungumza ni nadharia ya usawa kati ya mwanaume na mwanamke eneo la ndoa akiamini wote wanataka ndoa kwasababu za kufanana.
Mimi namwambia kuwa ndoa inamfaidisha zaidi mwanamke na ndio maana ni yeye anayeitaka. Anasema nimpe mifano nampa mifano ya madada wanaokwenda kwa akina mwamposa, kwa akina mama lwakatale na kwa wachungaji wengine kwenda kuombewa wapate ndoa, wapi ameona wanaume wanaenda kuombewa wapate ndoa?
Anasema jamii inampa pressure mtoto wa kike kuolewa na kumyooshea vidole asipoolewa, swali ni nani ana time hapa mjini ya kujudge mtu asiyeolewa cha zaidi si ni wanawake wenyewe ndio wanaitafuta ndoa na wasipoipata wananyoosheana vidole sababu wanajua faida za kuwamo kwenye ndoa?
Akina zari wanapesa wale, akina jide, akina wema, jackline wolper hao ni maarufu tuachane nao tuje hata kwa ambao si maarufu hivi kuna mtu anawaforce kutafuta ndoa ila si unaona wanavyohangaika.
Sasa huyu binti me nahisi bado hajaingia 3rd floor ambapo ndipo kwenye ukweli wa ndoa ni kitu gani.
Nimeshakutana na wadada wa miaka 36 hawana watoto wala hawakuwahi vishwa pete,angekaa nao ndio angejua ndoa ni kwaajiri ya mwanamke kwa asilimia kubwa sababu anachokitafuta katika maisha kipo humo.
Ila ngoja tumpe muda, ana mengi ya kujifunza kwenye maisha naona kwa sasa kachagua kuwa mbishi.
Dooh yani wanaume sijui kwanini mnapenda kufanya makosa kwa makusudi ili mradi tu wanawake wajishushe yani imagine eti unatengeneza tatizo ili mradi tu mkeo akubembeleze mbona kama huo ni utoto sana, kwanza kabisa unapomkataza mkeo kutoka weekend je unakuwa na sababu ya msingi ya kufanya hivyo au ndio basi tu ili mradi utumie mamlaka yako kiubabe hata pasipostahili hivi kwanini mnapenda kuwapima na kuwajaribu wanawake, na je wewe unapotoka na kumuambia mkeo asitoke ni kwamba hujui kuwa ukimuacha atabaki mpweke kiasi cha kuona kwamba hadi hilo nalo ni jambo la kukumbushwa tena kwa unyenyekevu kwanini wewe usijiongeze tu kwamba ukitoka ukamuacha mkeo lazima tu atabaki mpweke hivyo ni either utoke naye au mbaki wote nyumbaniWanaume wanastyle yao ya kuwanyoosha wanawake ili kuwakumbusha wajibu wao. Sasa kosa mnalofanya wanawake ni kujibu mashambulizi kwa tit for tat. Kosa kubwa.
Mwanaume akikwambia sitaki kukuona unatoka out weekend unatakiwa kujibu kwa kumwambia sawa mume wangu sitotoka basi naomba uwe unatumia muda wako wa weekend karibu yangu natoka sababu nakuwa mpweke ukiwa haupo na mimi.
Sasa Jadda atajibu "Bwanaaaaa eeeeeeeeeh kama wewe unatoka kwann mimi nikae ndani pekee yangu kama utumbo, ukitoka na mimi natoka ama sivyo sote tubaki nyumbani mimi sikai pekee yangu ndani"
Umeona tofauti ya hizi responses mbili, moja unamuonyesha mwanaume kuwa upo submissive na yeye ni kiongozi wako na unamtii na kufuata maelekezo yake halafu ya pili ni response ya mwanamke anayetaka kuonyesha yeye pia ni mwanaume na ana ubavu na hapo ndani hakuna aliye juu ya mwenzake.
Mwa
Mkuu mimi mbona hakuna mahali niliposema kwamba wanawake hawahitaji ndoa mimi nafahamu ndoa ni muhimu kwa jinsia zote mbili hasa for the sake of maadili na ustawi wa jamii, mimi ninaopingana nao ni hawa wanaosema kwamba mwanamke ndiye anayehitaji ndoa na siyo mwanaume ilihali hawana logic zaidi ya kutumia mihemko tu, yani eti tendo linalohusisha jinsia mbili liwe muhimu kwa jinsia moja halafu lisiwe muhimu kwa jinsia nyingine hivi inaingia akilini kweli hiyo mkuuVizuri kama unafahamu na kulitii hili.
Seems una uelewa na ufahamu mpana. kwa hoja zako naona kabisa unaweza jena hoja X ni alama ya kuzidisha na sio herufi na watu wakashawishika. Sasa tusaidie jambo...
Waambie wanawake kuwa ni kweli sisi wanaume tunahitaji ndoa, lakini pia wao wanahitaji directives katika ili kuepuka divergent ending. Naelewa hata wewe hapa unaweza question lakini tunaongelea divine rule (Nature).
Sasa tukubali kuvumiliana, nikupe upendo, unipe namna au nikuwezeshe kufikia kule unakotamani.
Dada umeandika ukweli mtupuMkuu hiyo daddy care siku hizi mbona ni kama wanawake wameshaikatia tamaa maana wameshaaminishwa kwamba hayo ni mapenzi ya kihindi na kikorea, na kwamba africa watasubiri sana kupata wanaume wa kuwapa hiyo care hasa hawa vijana wa rika lao, wenyewe huwa mnadai haiwezekani mwanaume akutafutie pesa akuhudumie na bado awe romantic na akupe care
So wanawake ni kama wameamua kutafuta furaha kwa watu wengine mfano watoto, wazazi, ndugu au jamaa na vitu vingine mfano kazi au biashara lakini wanaume bado furaha yenu iko centred around women, yani mnategemea muipate toka kwa wanawake tu unaweza kuta mwanaume ana kazi au biashara nzuri ana marafiki na washkaji wengi tu ila hana furaha kwa sababu tu anaona kama mke wake hamtreat vizuri, ninyi ndio huwa mnapenda zaidi zile kauli kama "pole na uchovu wa kazi mume wangu" au "karibu chakula mpenzi wangu" na romantic gestures kama hizo
Tena wenyewe huwa mnakiri kwamba hivyo vitu vidogo vidogo ndio vinamkeep mwanaume asipovipata ni either atakusaliti au atakuacha, ambapo bado ataenda kuvitafuta kwa kiumbe yule yule mwanamke lakini jiulize ni wanawake wangapi wanasaliti au wanaacha waume zao eti kisa hawapewi hiyo care, kinachowafanya wanawake wahitaji ndoa ni ile mentality waliyojengewa na jamii kwamba mwanamke asipoolewa anaonekana malaya, kwahiyo huwa wanaogopa tu wasipoolewa jamii itawaonaje ila tukija kisaikolojia wanaume ndio wanahitaji zaidi ndoa, kwa sababu ya kupenda sana care kama hizo ambazo ni ngumu kuzipata kwa kununua tu malaya bila kuwa na stable relationship or marriage
Huu ni uongo..wote mli compromise mkavumiliana makosa/mapungufu yenu..na sio kwamba ulimpata mtu alive kuweka priority..hakuna mwanamke anayekuweka priority asiwe na hayo makosa mengine uliyotaja...bro kama his ndio mindset yako you have to change or you will die lonely... YAANI I CAN PREDICT KABISAAA HUNA MAHUSIANO AU HUJAWAHI KUWA NA MAHUSIANO YA KUDUMU/ MUDA MREFU..KAKA MCHAWI NI WEWE MWENYEWE.Unajua sio kwamba wale tunaoendana nao ni watu ambao wapo perfect au hawakuwa na shida za kitabia, ila kinachotokea wanatuweka sisi priority na kukubali kubadilika ili kuweza kuwa na sisi kwenye maisha.
So everyone is crazy until they meet someone who can make them feel safe to feel sane again.
Nani ana hitaji zaidi ndoa au mahusiano kati ya mwanamke au mwanaume kwa wewe akili yako unavyo ona ?!Dude, nafikiri mpaka hapa utakuwa umeshaelewa kati ya mwanaume na mwanamke ni nani anayehitaji zaidi ndoa au mahusiano kuliko mwenzie, sasa wanaume endeleeni kushindana na hawa wanawake wa leo mkidhani mnawakomoa kumbe ni ninyi wenyewe ndio mnaoumia
Huku mtu yoyote anaweza kusema lolote...ngumu sana kuamini kama wewe mtu ushawahi kuwa na mahusiano ya kudumu .....utatudanganya tu hapa to prove your point lakini ukweli ni kuwa umepitia series za broken relationships.....na unaendelea kuwa na rocky relationships sababu mtu unayemtafuta hayupo! ...hata huyo ulie nae alikuwa na baadhi ya tabia hizo...it means ni nature kumkuta mtu na hizi tabia, kusema amebadilika sasa hivi hanazo ndio uongo wenyewe ili tuamini....kama wewe sio Muongo zitaje hizo tabia alizokuwepo nazo awali ambazo sasa hivi hana tukukamate vizuri....umekubaliana na udhaifu wake mnaenda sambamba halafu unasema amebadilika?!....hujiulizi kwa nini baada ya kuwa na mahusiano mengi yaliyovunjika huyo uliyempata nae hakuwa tofauti na wa zamani , na yeye alifall kwenye hizo tabia..???... ndio ujue ulichokiandika ni upuuzi na kinaonyesha wewe ndio una udhaifu wa kuwa perfectionist na unapingana na nature sijui kwa faida ya nani..tuambie wanawake wa nchi gani ambao Havana hixo tabia kwanza..?Sasa dada aliyekwambia mimi sipo kwenye mahusiano ni nani au unataka nikualike uje uone maisha yangu tushinde hata siku moja halafu utazame kama mwenzako anateseka kama unavyodhania.
Mimi hapa naweka bayana haya mambo sababu nilishakutana nayo sana kwenye mahusiano na hata huyu nilie nae alishakuwa na dalili ya kuwa na baadhi ila alikubali kurekebika na ndio maana tunaenda sambamba.
No one is perfect ila inaanza na kukubali kwanza kuwa tunashida somewhere.
Wewe umesoma hapo badala ya kujitathimini unaanza kuprove my point kuwa kuna watu wana haya matatizo.
Kama hiyo list ya tabia umeona imekuumiza kichwa it means that's not something new kwako na ulishasikia mtu anakusema una hizi tabia so ni muda sasa kujitathimini na kuchukua hatua.
Na kama hauna hizi shida then why hautaki wenzako warekebike tabia.