Sijakulazimisha wala kukulisha maneno hata kidogo ninachofanya ni kukutafsiria kile unachokiongea kwa lugha ya kike (emotional) nakiweka kwenye lugha ya kiume (logical) ili uweze kupata kuelewa kuwa unachokisema haujakitazama vema.
Ninachofanya sio personal attack najaribu kukuonyesha kuwa unaongea not from personal experience bali unatumia a very narrow but partially perspective ya maisha. Kwa kifupi una kwenda kitheory badala ya uhalisia. Mfano ni watu waseme maisha ni magumu sababu serikali haitoi ajira halafu atokee mtoto wa kitajiri aseme ni wavivu kwann hawajajiarii (anasahau kuwa mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe na mtaji wa tajiri ni mali zake). So that's not personal at all nimekushtua tu kuwa unaongea usichokifahamu sababu haupitii maisha kama ya mabinti wenzako na umri pia pengine haujafika 3rd floor ndio maana haujaanza elewa pressure huwa inaanzia wapi.
_________________[emoji1540]
Umekuja vizuri sana kwa kusema kile ninachosema kuwa mwanamke anaingia for financial support (emotional needs and fulfilment). Tunapoanza ugomvi ni wewe kuanza kusema mwanaume pia anaingia for PSYCHOLOGICAL PURPOSE which also translates into emotional needs, sijui unaelewa wewe binti mimi na wewe ngumi zinaanzia wapi? Kwann unakwepa the fact kwamba wanaume hatuprocess mahusiano emotionally rather tunaprocess mahusiano logically?
Nimekufafanulia kule juu kwamba mwanaume anachofanya ni kama askari anaye jitoa kwa taifa lake sio kwasababu anagain chochote material bali its more of a self logical purpose in life. Yaani hafanyi jambo sababu linambenefit rather anatafuta sababu za kumfanya ahisi jambo linambenefit ili apate sababu za msingi za kulifanya kutimiza moral conduct and moral social responsibility ya kuprotect mwanamke na watoto wake kitu ambacho wewe unakosea kutafsiri ukidhani mwanaume anashida ya ndoa au bila ndoa kuna kitu anakosa (unasema anakosa care na romantic gestures) hivi hizi romantic gestures na care huwa unadhani wanaume hatujui kuwa ni wizi tu tunafanyiwa ili tulipe bills na kutunza familia, na tunajua wazi tukishazeeka na kuishiwa nguvu huwa hivi vitu hatutapewa tena na ndio maana wanaume hufa mapema kuliko wanawake mara tu umri ukianza kwenda sababu maigizo ya wanaume hufa ila mwanaume hatoacha asili yake ya kutunza mwanamke na watoto hata kwa hela yake ya kustaafu.
Again, unachanganya vitu, hivi haukunisoma vema kule juu niliposema FINANCIAL SUPPORT ni neno linalobeba maana ya kitu kinaitwa SECURITY PROVISION kwa mwanamke kutoka kwa mwanaume? So kwa mwanamke anayepata financial sources anaweza kwa muda fulani kuhisi hana shida ya mwanaume but as time goes on, umri unaenda na guarantee ya kuendelea kujipa hiyo support plus kukosa emotional support na kutokuwa na companion wa kumpa Financial support (ambapo humu ndani nilikuonyesha kuwa kuna contents za both physical and emotional needs anapewa mwanamke) then ndio maana hofu hurudi tena. Unaona wakina Jennifer Lopez, akina Halle berry, akina Tony Braxton, na wadada wengi sana wa huko majuu wenye pesa nyingi sana, kwann wanaendelea kutafuta wanaume na ndoa katika umri wa miaka 50+? Ila tazama wanaume wangapi wakisha divorce at the same age unaona wanatafuta ndoa tena? Tazama Dr Dre, Billgates, Jeff bezos, Michael Jordan, 50cent, tazama hawa wote wanapesa ila maisha yao ya kimahusiano unaona wanahangaika na Ndoa au wanachumbia wanawake at that age? Why? Si unasema mwanaume anahitaji ndoa kumshinda mwanamke?
___________[emoji1540]
Kosa unalorudia kwenye kila paragraph ni kusema mwanaume yupo clingy kwenye ndoa sababu ndoa ndani yake ina kitu ambacho mwanaume hawezi pata nje ya ndoa. Mimi nakukatalia na nakupa na melekezo kwenye kila paragraph ila kama kawaida yenu wanawake ukiona hoja inakubananisha na uhalisia huwa mnashift goal posts na kutwist reality ili unachosema kiweze kuonekana ni ukweli kumbe ni kinyume chake, okay ngoja nikujibu lakini maana nimedhamiria kukufunza.
Umeuliza kuwa ukitoa ndoa ni sehemu gani nje ya ndoa mwanaume atapata utulivu (me naita purpose for life wewe umetumia neno utulivu so tuelewane hapo kuwa tunaongelea kitu kimoja ni sawa na wewe useme mwanaume anataka soda mimi niseme anapendelea Pepsi). Mwanaume nje ya ndoa anakuwa ni kiumbe unpredictable na hii inaweza kuwa na faida au madhara kwenye jamii. Mwanaume akituliza kichwa akabakia yeye na MUNGU wake na kutaka kuwa positive ndio tunapata watu kama akina Tesla, Newton, Albert Einstein, etc ambao wanatenga muda na kuwa inventors na founders wa mambo mengi ya kimaendeleo (this is purpose). Ila pia mwanaume akiamua sasa kuwa kinyume chake ndipo unapata sasa shida kama akina Bokoharam, ISIS, wabakaji, wauwaji, wezi, incels, na hawa ambao wanazalisha mabinti na kutoka nduki hawatoi Financial support kwa mwanamke.[emoji362]Kumbuka financial support ndani yake inabeba nini na inamaanisha nini kwa mwanamke kutoka kwa mwanaume nakukumbusha hapa.[emoji362]
Ndio maana wazee waliokuwa na busara wakamtrick mwanaume kuamini anahitaji ndoa kumshinda mwanamke na purpose yake au sababu yake ya kuwa mwanaume kamili na kuja duniani ipo ndani ya ndoa ila huu si uhalisia wa mambo katika eneo la asili (nature) ila katika context ya jamii tuliyokuzwa story inawekwa kama wewe unavyojaribu au unavyolazimisha kuwa mwanaume pia kama mwanamke ana njaa ya ndoa na akikosa hana maisha nje ya ndoa kama mwanamke, jambo ambalo si kweli. Nenda kajifunze zaidi kuhusu ndoa. Ndoa imebidi kuwepo ili kuchannel purpose ya mwanaume kwenye maisha ilenge katika kuprotect interest za mwanamke na mtoto, wazee na wahitaji wengine ndio maana kwenye ndoa mwanamke hawezi kuwa bread winner wa kulea mume , watoto wake, halafu alee na ukoo wa mume wake pamoja na wakwake bado alee na ndugu jamaa na marafiki wa pande zote mbili hii kazi mwanamke hawezi ni mwanaume ndio anafanya miaka yote, how does that benefit him for whatever reason?
Kukukujibu mwanaume anaweza kupata nini kama akiwa nje ya ndoa. Kama ni mfuatiliaji mzuri utagundua sasa hivi kuna ongezeko kubwa la single mother sababu ni wanaume hawaishi kwa ile channelled purpose ya kuprotect mwanamke na watoto na other weak members of the society sababu tayari hakuna trainings za kushape na kuprogram akili ya mwanaume wa kisasa logic wise kuihitaji ndoa na hiki ndicho usichokifahamu na ndicho nakazana kukwambia hapa tokea kule juu.
Wanaume wa kisasa wanahitaji ngono ambayo anaipata kwa njia ambazo ni haramu mfano, kwa mashoga kwa kufanya nao kinyume na maumbile, kubaka wanawake na watoto, kununua makahaba, kupiga punyeto. Hivi vitu vyote wazee walijua wakamset mwanaume kuhitaji ndoa ili aamini mtu pekee wa kumpa utamu ni mkewe na kutafuta utamu nje kwa namna yoyote ni dhambi na kosa kimaadili. Jiulize nani ana athirika na hii life style ya mwanaume wa kisasa mwanamke au mwanaume? Wewe kama mwanamke jamii yako ikazungukwa na wanaume wanaotaka kuwangilia watoto wako wa kiume, kurubuni na kulala na watoto wako wa kike, wewe tu uwe katika risk ya kubakwa, hiyo imekaaje kwako, usijibu hapa kama mtoto wa kishua ambaye haujawahi experience haya mambo, tuliza kichwa chako vaa viatu vya mwanamke wa maisha ya kawaida sana ambaye hana mtu wa kumtegemea wala hana mtetezi, yaani akibakwa ni imeisha hiyo, mtoto wake akipewa mimba katika umri wa miaka 15 imeisha, mtoto wake wa kiume akilawitiwa imeisha no body wa kumtetea wala kumlinda. Hii ni eneo moja tu la mahitaji ya ngono ambapo mwanaume akikosa ndoani anapata nje kwa namna ambazo hugeuka na kuwa haramu ila madhara na hatari humrudia tena mwanamke na kumuweka hatarini kimaisha.
Ndoa hutumika kuzima hormones kali za kiume ambazo humpa hasira, jazba, mfadhaiko na kadhalika. Mwanamke ana namna ya kumfanya mwanaume kutulia na kufocus kama mama anavyobembeleza mtoto. Ila si kwamba mwanaume anashida na huo utulivu, mwanaume akiwa katika wildness state yake anakuwa kama Hulk and trust me ni nzuri kwake ila mbaya kwa mwanamke. Akiwa katika hali yake ya asili ndipo hupenda vita, ugomvi, atapigana kila dakika hizi chaos zinamuweka mwanamke na watoto hatarini. Kama haukubaliani na mimi nitakuuliza kama unafuatilia kinachotokea katika black communities huko marekani umeona nature ya mtoto wa kiume ambaye hajawa programmed kuishi kwenye ndoa anavyokuwa, ugomvi kila saa, kuuwana, kubaka, kutukana, gangs, kuuza madawa, silaha etc, trust me hutaki kumuona mwanaume akiwa nje ya purpose za ndoa.
So unavyosema mwanaume anahitaji ndoa ili kupata mtu wa kumliwaza sababu anahitaji na akikosa atapata msongo wa mawazo hayo ni matokeo ya kuwa programmed kuamini ndoa ndio inampa utulivu na sababu ya kuishi ila kaa chini utafakari mwisho wa siku nani huwa anabeba mzigo na kuwa manipulated kuamini anafanya kwa faida yake? Nimekufafanulia kwann anatulizwa sababu akiamua kuishi nje ya ndoa anajituliza kwa namna ambazo zinaanza kuleta hatari kwenye jamii.
___________[emoji1540]
Again, unakosea tena kulazimisha kuwa mwanamke anaitafuta ndoa sababu ya mitazamo ya jamii, hebu futa hii kitu kichwani wewe acha kuwa mbishi. Nenda marekani na ulaya kule hebu tazama wanawake vitu wanavyofanya na kule hakuna shinikizo wala kunyoosheana vidole. Wanawake wa ulaya wanafunga ndoa na wazee, wanaoa wanawake wenzao, wanaoa hadi mbwa, ng'ombe, nguruwe, miti, magari, na wengine wanajioa wenyewe, unataka kunaambiwa sisi waafrika tunafosi wanawake zetu kwenye ndoa? [emoji848][emoji848] Hivi kuna watu wanaojua kujiamulia kuwashinda wazungu hata kama ni swala la kipumbavu wao huwa wanakomaa ila mbona kwenye ndoa wamechemka. Huko majuu kuna wanaume wa miaka 50+ au 60+ hawajawahi kuoa wala kuwa na familia na wanaishi wenyewe kwenye bachelor pads, ana drive gari ya bei kali, nyumba ya single au vyumba viwili but very expensive, ana salio la kutosha bank na hana time, akitaka kula ni restaurant, au ataita mpishi ampikie au ata order fast food. Akitaka sex kuna wanawake kibao wa kulala nae ila wasichoweza ni commitment sababu wamestukia sheria za ndoa zinalinda na kuwabeba wanawake wao zinawafilisi tu na kuwapa stress. Sasa kwa akili kama zako ipo siku tutaelekea huko kama tukipata viongozi wanaofikiria kama wewe kuwa mwanaume anashida ya ndoa kumliko mwanamke.
Of course kuhusu kuwananga masingle mother nitaendelea na sitoacha sababu ni kirusi kibaya sana kwenye jamii yetu. Na usikosee kufikiria kuwa wanawake wanaingia kwenye ndoa sababu tunawasema na usingle mother sijui hapana. Wanawake mnaviburi vya hasara sana hilo hata kwenye Bible utaliona sehemu nyingi na ndio chanzo cha uharibifu duniani so tusipowakemea huwa mnatabia ya kufanya mambo ya kipuuzi sana na kuharibu jamii, mfano ni hili la usingle mother ni maamuzi yenu binafsi msitusingizie wanaume. Wanawake hawapanic na ndoa kwasababu sisi tunawasema ingekuwa hivyo basi wangekuwa wanapanic mabinti wa umri wa ndoa yaani 25 kushuka chini ila huwezi nambia mwanamke wa miaka 30+ anapanic sababu wanaume na jamii wanamnyooshea vidole na kumsema, anapanic sababu anaanza kuona uhalisia wa maisha na kuona uzito na faida ya ndoa wakati muda wa kujiandaa umefika, ni kama mwanafunzi wa form 4 au 6 ambaye ni mvivu kusoma, ikifika wiki ya mtihani wa taifa anakosa usingizi sio kwasababu kuna mtu anamsema au kuzungumzia juu ya uvivu wake bali anapanic sababu sasa anaanza kuelewa uzembe wake unakwenda unamgharimu na anakwenda kufeli sababu kapoteza miaka yake yote ya masomo.
_______________[emoji1540]
Nimekujibu pale juu, wanawake umri ukienda wanajua madhara ya kupoteza muda na sasa wanaona umuhimu wa ndoa na hasara ya kutowekeza kwenye mahusiano ya ndoa ndio sababu wanapanic, mabinti wadogo hawawezi panic sababu wapo katika prime hawajapata ile pressure uhalisia wa maisha bado,zamani walikuwa wanafunzwa impact umya umri kwenda bila ndoa wanaelewa siku hizi jamii imewaachia mkalie kuti kavu mjifunze kwa matendo yenu wenyewe na kwa muda wenu wenyewe something which is very bad, kama wewe hapo bado makaa ya moto ya 3rd floor hayajakuwakia endelea tu kurelax usiwe na time na mahusiano sababu ndoa inamfaidisha mwanaume wewe hauna shida nayo, uone balaa ukifika ghorofa ya tatu. [emoji23][emoji23] Huko ukifika vyumba vyote vinawapangaji na lift inaenda juu tu kuelekea 4th na 5th floor huko haishuki chini tena kwenye 2nd na 1st floor, huko juu kuanzia 4th na 5th floor ni penthouses tu hakuna nafasi ya wapangaji, all apartments are taken and paid for in full ni aidha uombe kushare nyumba au ukae koridoni maisha yako yote au mpangaji atoke wewe uingie[emoji23][emoji23][emoji23]
_________________[emoji1540]
Wanawake naoolewa na ndoa zao kudumu ni wale wanokwenda na misingi ya jamii kwa namna kila siku tunavyoelekeza hapa. Wanaume wanaendelea kutimiza wajibu wao ndio maana idadi ya wanaume wazuri wanao oa wanawake wasiojilewa na ndio zikavunjika ni wengi kuliko wanawake wazuri wao olewa na wanaume vilaza wasio na kaliba ya ndoa. Kumbuka ndoa ni mwanamke akiwa amefundwa vema itadumu ila kwa ambaye anapenda ligi kama wewe itategemea na haiba ya mwanaume, kama amekuzwa vema ataweza kukazania akunyooshe huku anavumilia ila mwanaume wa wastani lazima atakukataa na kutafuta mji mwingine.
______________[emoji1540]
Kwenye hii aya ya mwisho naona unaweza kuona kuwa umejijibu sasa swali lako mwenyewe bila kutambua kuwa unajibu kitu gani. Umesema vema sana kuwa mwanamke hawezi fanya kile ambacho mwanaume anafanya sasa nikuulize swali, kumbe unajua kuwa kwa mwanamke haina faida kufanya majukumu ya mwanaume sababu gharama ni kubwa sana kwake compared to yale anayofanya mwanamke kwa mwanaume reward kwake ni kubwa sana.
Ukitaka jua nani anapata nini tazama mwisho wa maisha. Unaiskia kila siku wanaume ndio huwa kufa kuliko wanawake shida unadhani ni nini? Shida ni gharama ya kumtunza mwanamke na watoto huwa ni kubwa kuliko return yake. Vyovyote unavyotafuta ni kwaajiri ya mke na watoto ila kama mwanaume unaweza amua kuwa na vyako mwenyewe ila guess what? Hatujawa programed kuishi hivyo especially jamij hii ya Dunia ya tatu sababu tukifanya hivyo tutatesa wanawake na watoto na wataumia sana.
Mwanaume akisema afanye anachofanya mwanamke then mwanamke ataumia. Imagine mimi nimekuoa wewe Jadda halafu unafanya kazi ya mshahara mzuri, say milioni 3.5. Mimi naamua kuwa stay home Dad na trophy husband. Nakuwa run home affairs, unaniwekea house girl asaidie shughuli za nyumbani hata tukipelekea moto hautajua sababu itakuwa ni siri yangu na yeye, then ukienda kazini ukirudi nataka tupelekeane moto round tatu kwa siku, ukibeba ujauzito mimi nakuwapo around kukusapoti na naweza piga mishe mbili tatu kusapoti expenses kipindi ukiwa mjamzito, then ukishajifungua tu unarejea kwenye kazi mimi nalea mtoto na house girl. Hii ndio iwe style yetu hadi ufike umri wa kustaafu. Assets na mali zote ziwe kwa jina langu na watoto?
Hiyo imekaaje kwako, unaweza kusacrifice hivyo,kama haiwezekani, unaweza nambia kwann? [emoji848]
__________________[emoji1540]
Kosa gani sasa mtu anakwambia hataki mkewe utoke nje sababu ya usalama wako na ulinzi wa ndoa wewe unabishana nae ili kuprove nini?
Naweza kutoka nje nikapigwa nisikupigie simu kama mke wangu na nikamaliza kila kitu huko nje nikarejea home salama salimini. Ila wewe unaweza toka nje huko ukakabwa, ukapigwa, ukadhurika na chochote simu ya kwanza nitapigiwa mimi, hata kama utapiga kwa baba na mama yako au kama yako au dada yako kuwa umepatwa matatizo, wao watanipigia mimi kuniuliza kulikoni binti yetu mtoto wetu anapatwa na shida wewe haupo eneo la tukio. Hiyo ndio sababu kwann nawajibika kucontrol unapokwenda na unakuwa na nani na unatoka saa ngapi.
Usiulize kwann but that's the way it is and the way it will always be.
Utoto ndio sasa wewe unavyomwita mtu baby ilidhani baby ni ugali au mfuko wa rambo?
Shida ufosi sana usawa as if nature inajali hisia zako na inatakiwa kujielekeza upande wako kukupa kile utakacho, well am sorry ma'am, the world doesn't evolve around what you feel or want, nature is nature.
Ndio ndoa ni muhimu kwa jinsia zote mbili sababu kuna vitu tunapata ila katika hizo jinsia, mojawapo inapata zaidi, na jinsia hiyo si ya kiume ni ya kike.
Ulimwenguni hapa hakunaga fair gain, huwa kuna manipulations and exploitation, upande m'moja hupata zaidi ya mwingine kwasababu tofauti.
Mfugaji anaefuga kuku au ng'ombe kwaajiri ya nyama huwa anamhangaikia kumlisha na kumpatia matunzo ili aongezeke kilo na kuwa mkubwa anone kwaajiri ya kuchinja nyama.
Sasa imagine wewe uje na observation kwamba mchungaji na ng'ombe au kuku wake wote wanabenefit sawa sawa katika uhusiano wao huu, hivi hiyo imekaa sawa? Yaani ng'ombe anafugwa ili hatima yake ni kuuliwa aliwe wewe unasema anafaidika yaani analishwa vizuri na kupewa matibabu na matunzo ili anone kisha aliwe wewe unasema anafaidika na yeye ndie anashida sana ya huo uhusiano uliopo kati yake yeye ng'ombe na mfugaji.
Kwa kifupi, mwanaume anaoa na kuwa na mwanamke sababu jamii imeshaweka program maalumu za kulinda jamii yenyewe kupitia mwanaume sababu ndie kiumbe imara zaidi. Hivyo basi wameona watengeneze structure itakayompa mwanamke guarantee ya usalama ili aweze lea watoto( offsprings) bila shida sababu kinyume chake ndio hivi tunapata masingle mother,watoto wao by 90% huwa wanakuwa na tabia za hovyo. Nenda kajifunze madhara ya nyumba bila baba imara au baba bora utaelewa naongelea nini.
Hata wanyama wanajua hapa kuwa huyu ni wmanaume huyu ni mwanamke na wanatii zaidi na kuogopa mwanaume kushinda mwanamke.
Hivi wewe huoni aibu kushusha haya magazeti yote ili mradi tu kutetea uongo na mawazo yako binafsi yani sitaki kuamini kwamba unataka kunilazimisha tujadili assumptions zako na siyo reality like seriously, wewe unasema mimi naforce mambo as if nature inajali hisia zangu hivi hata kwa kuangalia tu kwa akili ya kawaida katika huu mjadala ni nani ambaye anajadili kwa kudhani dunia ina revolve around kile anachohisi na anachotaka, au labda niongee kiujumla tu hivi kati ya wanaume na wanawake ni kina nani ambao wanadhani dunia ina revolve around what they feel and want huku wakiisingizia nature
Yani hakuna jinsia ambayo inapenda kuisingizia nature hata kwenye mawazo yao binafsi kama wanaume mfano hata kwenye suala la mwanaume mmoja kuwa na wanawake wengi na huku kwa wanawake hairuhusiwi, miaka yote mmekuwa mkiisingizia nature na kuwadanganya wanawake kwamba wako wengi kuliko wanaume na kuitumia hiyo kama justification, lakini ukiangalia demographic stats za dunia zinaonesha wanaume ni wengi kuliko wanawake na hata ukichukua hizo factors zinazosemwa kama ushoga, hukumu, magonjwa, vifo nk (ambazo hata wanawake zinawakuta) bado utakuta kwamba population hairuhusu kila mwanaume kuwa na wanawake hata wawili tu achilia mbali hao wengi, maana mkilazimisha basi na wanawake nao watajikuta wanakuwa na wanaume zaidi ya mmoja vile vile
Hapo nilikuwa najaribu kukuonesha jinsi gani wanaume mnajua kutumia ile self serving reverse psychology trick kuwamanipulate wanawake wakubali kufanya vitu kwa manufaa yenu huku mkiwadanganya kwamba ni kwa manufaa yao, sababu mnajua bila kufanya hivyo hawatakubali kirahisi hivyo mtajikuta mnatumia nguvu kubwa kuwabembeleza ili wakubali kitu ambacho wanaume wengi hamtaki sababu ya mfumo dume hivyo ndio maana mkaamua kutumia hiyo mbinu, yani imagine kuna wanaume wanasema eti mwanaume anapooa wanawake wengi anakuwa anawasitiri wale ambao wangekosa waume sababu ya idadi yao kuwa kubwa kuliko ya wanaume kitu ambacho ni uongo, na wengine wanaenda mbali zaidi na kusema eti wanawake hawapendani kisa hawataki kushare waume ili na wenzao nao waolewe kitu ambacho ni uongo pia kwa sababu ubinafsi na kutokupenda kushare ni hulka ya kila kiumbe, hata wanaume hampendi kushare wanawake lakini hutasikia mkisemana kuwa hampendani eti kwa sababu hampendi kushare wanawake
Lakini tukija kwenye hali halisi sababu kubwa (ambayo iko wazi kabisa wala haihitaji uwe psychologist kuielewa) ya wanaume kuoa wake wengi ni kwa tamaa zao na manufaa yao ya kingono tu wala si kwa faida ya wanawake, ila hii sababu wameamua kuiweka pembeni na kuifanya kama vile ni minor reason tu sababu wanajua wangewapa wanawake hiyo sababu basi wanawake wasingekubali kirahisi kuingia kwenye ndoa za wake wengi, hivyo wakaona waje na propaganda na porojo za wanawake ni wengi kuliko wanaume hivyo wanajaribu kuwasitiri wanawake waliokosa waume, na hiyo hiyo mbinu ya manipulation ndio walioitumia wazee wetu kwenye kuwaaminisha wanawake kuwa ndoa ni muhimu zaidi kwa mwanamke kuliko mwanaume kiasi kwamba wanaume bado mnatembea kwenye huo uongo hadi leo, pamoja na kwamba yanayoendelea dunia ya leo yameshadhihirisha ni jinsia gani inahitaji zaidi ndoa ambayo ni yenu
Kwenye comments zangu za mwanzo kuna mahali nilikuambia zamani enzi za babu na bibi zetu kwenye jamii nyingi za kiafrika wanawake walikuwa wanafanya majukumu mengi kuliko wanaume, yani wanawake walikuwa wanafanya kazi za nyumbani, wanalea watoto, wanaenda shamba nk huku wanaume kazi yao ilikuwa kuenda vilabuni, kunywa, kupiga soga yani wanaume jukumu lao lilikuwa kutawala himaya tu na kuleta mamlaka na ubabe kwa wanawake na watoto, lakini pamoja na hayo walikuwa wanaaminishwa kwamba ndoa ni muhimu kwa mwanamke na siyo mwanaume sasa unaweza ukaniambia huo umuhimu wa ndoa kwa mwanamke ulikuwa ni upi katika mazingira kama hayo
Okay unasema kwamba mwanaume asipopata utulivu wa kwenye ndoa basi anafanya mambo ya ajabu ili apate utulivu sasa huoni hadi hapo tu hiyo ni sababu tosha ya kuonesha umuhimu wa ndoa kwa mwanaume, yani kwanini upate utulivu kwa kufanya maovu je mwanamke akikosa ndoa anaweza akafanya mambo ya ajabu kama hayo, by the way inawezekana vipi mtu akapata utulivu kwa kufanya mambo ya ajabu kama ushoga, ujambazi, ubakaji na uhuni mwingine hii ni saikolojia ya wapi hivi unafahamu kweli saikolojia ya mwanadamu inavyofanya kazi au umeamua kwa makusudi tu kujitoa ufahamu, ni binadamu gani anayeweza kujisikia vizuri na kupata utulivu kwa kufanya maovu wewe huoni kama hayo ni matatizo ya akili yatokanayo na trauma na depression ambazo mara nyingi husababishwa na kukosa upendo, au husikii watu kila siku wanajuta na wengine kujiua kabisa kwa sababu ya kushindwa kuishi na ile guilt ya kuwatendea maovu wenzao
Sasa mimi sioni kama eti mwanamke kuwa victim wa hayo maovu ya mwanaume ndio kunafanya ndoa iwe muhimu zaidi kwa mwanamke, kwa sababu ulivyoandika umeassume kama vile hayo maovu mwanaume akishayafanya basi yeye ndio atakuwa okay tu na ataendelea na maisha mengine kama kawaida yani kana kwamba akili na nafsi yake vitapata utulivu, hivi nikuulize kitu kati ya wanaume na wanawake ni kina nani wanaoongoza kwa kuwa na depression na post traumatic stress disorders, hivi unafahamu kwamba wanawake wana njia nyingi za kuondoa stress ambazo ninyi huwa mnaona ni za kike au za kitoto na mwanaume hatakiwi kuzifanya, matokeo yake zinawasaidia wanawake huku ninyi mkistruggle kutafuta utulivu mfano mzuri tu mwanamke anaweza maliza stress zake kwa kupiga umbea na hii ni kwa wanawake wote duniani, ila kwa wenzetu walioendelea stress wanajitafutia wenyewe sababu ya kuukataa mfumo wa kijamaa na kuishi mfumo wa kibepari, ambao wenyewe hauna mambo ya kutembeleana mara kwa mara au kuenda sijui kwa mama nani kupiga story na kuombana chumvi na mkaa kila siku
Unaniambia eti wanaume wanaoa kwa sababu wamekuwa programmed kujitoa kwa ajili ya wanawake na watoto, na kwanini unaassume kwamba ni wanaume tu ndio ambao wamekuwa programmed, ila wanawake hawajawa programmed kufanya vitu fulani kwa ajili ya kuwaridhisha na kuwafurahisha wanaume, labda nikuulize hivi unadhani kati ya mwanamke na mwanaume nani anaenjoy sex, kama jibu ni wote kwanini wanaume ndio ambao wanahangaikia sana sex wengi wanahonga pesa na mali walizozitafuta kwa jasho mradi tu wapate sex lakini uliona wapi mwanamke anahangaikia sex kiasi hicho, je hii maana yake ni kwamba wanawake hawaenjoy na sex siyo muhimu kwao kama ilivyo kwa wanaume ndio maana wao hawaihangaikii sana, je na wanawake nao wakiamua kusema kwamba hawaenjoy sex ila wanafanya tu ili kuwafurahisha na kuwaridhisha wanaume (ndio maana wanaweza kukaa muda mrefu bila sex) je watakuwa sahihi
Na labda nikuulize je unahisi mwanamke kuwa financially dependant kwa mwanaume ni nature yani ni kitu natural, au nao wamekuwa programmed tu kuwa hivyo kama ambavyo wanaume wamekuwa programmed kuprotect familia, yani kwanini uhisi kama wanaume kufanya vitu fulani ndio wamekuwa programmed na siyo nature ila wanawake kufanya vitu fulani ni nature tu ila hawajawa programmed, we unahisi wanawake hawawezi kujitafutia pesa na kujisimamia kiuchumi kama wanaume, kwani huoni sasa hivi ambapo ulimwengu uko kwenye 50 50 jinsi wanawake walivyoanza kushika uchumi kwenye sekta mbalimbali na wanafanya vizuri kama wanaume tu, ila kinachowahold back ni yale majukumu yao ya asili tu ambayo hata kama wanatafuta pesa na kusaidia kuhudumia familia bado wanatakiwa waendelee kutimiza majukumu yao, ambayo wanaume wengi hasa wa kifrika hawataki kuyafanya na hadi leo wanayaona ni ya wanawake na wewe ukiwa mmoja wapo
Kuhusu mwanamke kushindwa kutekeleza majukumu ya mwanaume nafikiri unashindwa kuelewa kitu kimoja au labda unaelewa ila unajitoa ufahamu, ni hivi mwanamke jukumu ambalo halitaki ni kumhudumia mwanaume tu na si kuhudumia nyumba au watoto hilo mbona wanawake wengi wanalifanya sana siku hizi, wewe unaishi kwenye jamii gani hiyo ambayo wanawake wanatafuta pesa na hawachangii chochote kwenye pato la familia hizi nazo ni propaganda kama propaganda nyingine tu, mwanamke kama anatafuta pesa kwa asilimia fulani ni lazima tu atahudumia nyumba au watoto ila mnacholalamikia wanaume ni kwamba hawawahudumii ninyi, na hilo jibu nimeshakupa ni kwa sababu nanyi hamuwezi kufanya majukumu yao wala kuwapa ile heshima na utii wanayowapa ninyi, huo mfano uliotoa kwamba ikitokea wameswitch majukumu je mwanamke ataweza siyo mfano hai, kwa sababu hakuna mwanaume ambaye atakubali kufanya majukumu ya mwanamke (ukitoa yale ya kimaumbile) kikamilifu halafu eti mke akatafute pesa tu ahudumie nyumba
Hawa hawa wanaume ambao wakiachiwa nyumba mwezi tu unakuta kila kitu kiko shaghalabaghala nyumba chafu vyombo havijaoshwa vina siku tatu, ukimuachia watoto ukirudi ndio kabisa utatamani kulia halafu leo hii mje mseme mnaweza kuswitch majukumu na wanawake, ilihali mwanamke yeye anaweza akatelekezwa na watoto kwa miaka mingi na bado akaendeleza gurudumu la malezi huku akihangaika kuwatafutia, hata kama siyo kwa kiasi kile kile kama mwanaume lakini that shows women are more capable of multitasking compared to men, kuna makala mbalimbali nilisoma kwamba mwanaume naturally hawezi kufanya majukumu mengi kwa wakati mmoja hasa majukumu ya kifamilia na akilazimisha atavurunda baadhi hivyo anahitaji msaidizi, akili yake imeundwa kufanya kitu kimoja kwa wakati mmoja ila atakifanya kwa ufanisi tofauti na mwanamke ambaye anaweza kuhandle kufanya majukumu mengi kwa wakati mmoja, kwahiyo katika hali kama hiyo kuswitch majukumu itakuwa ni kama tu kumtegea mwanamke halafu mwisho wa siku useme hawezi
Kuhusu kumkataza mkeo asitoke weekend sijaona sababu yenye mantiki hapo kwahiyo ina maana huyo mkeo hatafuti pesa ni mama wa nyumbani, na kama ni hivyo maana yake maisha yake yote yeye anashinda ndani tu hata sokoni haendi, na kama anatafuta pesa kwanini sasa kwenye shughuli za kutafuta kusiwe na shida yoyote kuenda ila weekend tu ndio uhofie kwamba anaweza akapatwa na matatizo, kwahiyo hayo matatizo yanachagua siku za kumpata mkeo kwamba akienda kwenye shughuli fulani hayawezi kumpata ila akienda kwenye shughuli nyingine yanaweza kumpata, hivi kwanza hata katika hali ya kawaida tu kati ya wanaume na wanawake ni kina nani wanaoongoza kupatwa na matatizo kwenye mishe zao za kila siku na ni wangapi wanachomoka kirahisi kama wewe ulivyojaribu kuandika hapa, asee hizi ndoa kweli wanawake wanapitia mengi yani kisa kuhudumiwa tu ndio mtu upangiwe masharti hivyo kama mnyama anayefugwa asiye na utashi, hapana asee ninyi ndio chanzo cha wanawake leo hii kutafuta pesa kwa nguvu sana ili walau nao wawe na sauti na maamuzi ndani ya nyumba
Yani ungenifahamu mimi wala usingeandika yote haya kunihusu ila kwa taarifa yako mimi siyo wa kishua wala sijui hata maisha ya kishua yanafananaje, na wala siko under 30 tayari nilishaingia third floor kitambo sana na wala siyo single mother, si kila kitu ninachojadili humu basi ni either nimekipitia au eti sijakipitia kumbuka kuna watu wanaotuzunguka ambao wanapitia haya na tunaona na mengine yako mitandaoni tunasoma, hii dunia siku hizi ni kama kijiji mzee taarifa ziko kila mahali haina haja ya kusubiri mambo yakutokee au uyaexperience eti ndio ujue dunia inavyoenda, mimi kwenye hii mijadala huwa napenda kuwa general kuliko kuwa individual yani hata kwenye mijadala mingine mfano ya kisiasa, huwa sipendi kumsifia kiongozi fulani eti kisa tu nilinufaika kwenye utawala wake au kumponda kiongozi fulani eti kisa tu sikunufaika kwenye utawala wake kama wengi wanavyofanya, mimi huwa naangalia na nasikiliza malalamiko ya wengi sijiconsider mimi kwahiyo wewe ukianza kujudge sifa zangu au maisha yangu kwa kuangalia jinsi ninavyowasilisha hoja humu basi utafeli na ndio utazidi kujiweka mbali na kuufahamu uhalisia wangu, ndio maana mimi hutanikuta namletea mtu personal attacks kwenye mijadala kama hii sababu siwezi kujua anatoa mitazamo yake kutokea upande gani mimi ninachoangalia tu je anachoandika ni uhalisia au ni mawazo yake mwenyewe