Wadada wa kazi (house maids) siku hizi ni pasua kichwa

HG wengi wanaletwa kukagua mazingira.
Mimi unakuja kwa nauli yangu ila ukiondoka ndani ya miezi mitatu nakata nauli yangu iliyokuleta. Itakayokupeleka ni yako mwenyewe....

Nasamehe wanao kaa miezi 6 na kuendelea, kitu ambacho hakijawahi tokea.

Hawa watoto hata uwafanyie nini hawanaga shukrani sijui wahindi wanawafanyaje
Wahindi wanawaweza hawa kwa njia hii huwapa kazi bila kuchekanao au kumbembeleza usijaribu kula nae meza moja ukiwa na family yako au upo pekee yako ukila nae anajiona mtoto wa nyumbani sio mfanyakazi akivunja glass mkate pesa zake hapo sasa atakaa na wewe vizuri.lakini sisi tunajifanya wema sana kwao ndio maana hata baba nyumbani yeye haoni tabu kumpa penzi
 
Yaani unagharamika kutuma pesa ya nauli na ya kula njiani anakaa siku nne unapigiwa simu kwamba huyo binti tunamtaka kuna tiba anataka kupewa baada ya siku moja atarudi, akienda harudi ng'oo, yaani tunapoelekea na hawa wadada sijui.
Na nyie mmezidi kuwatesa kila kitu dadaaa dadaaa
 
Kampun ipo, ukitaka unaletewa HG aliefundishwa kaz vizuri, akiiba akiharibu kitu kampuni italipa, mshahara utalipa kampuni ila yeye atalipwa na kampuni, na mkataba unasaini
 
  • Thanks
Reactions: ram
HG wengi wanaletwa kukagua mazingira.
Mimi unakuja kwa nauli yangu ila ukiondoka ndani ya miezi mitatu nakata nauli yangu iliyokuleta. Itakayokupeleka ni yako mwenyewe...

Nasamehe wanao kaa miezi 6 na kuendelea, kitu ambacho hakijawahi tokea.

Hawa watoto hata uwafanyie nini hawanaga shukrani, sijui Wahindi wanawafanyaje?
Wahindi wana waroga


Mbombo ngafu
 
Kampun ipo, ukitaka unaletewa HG aliefundishwa kaz vizuri, akiiba akiharibu kitu kampuni italipa, mshahara utalipa kampuni ila yeye atalipwa na kampuni, na mkataba unasaini
Hebu samahani tueleweshe kwahyo kampuni inakuambia laki3 halafu wao wanamlipa laki na nusu
 
Nimesha mpandisha gari,nimefata ushauri wenu pesa yake ndio nimemlipia nauli the remaining amount nimempa asepe kwao Gairo

Nimemwona kashukia Mbezi, asharudi mjini jiandae kupigwa tukio hapo ndani.... vile anajua funguo unapoweka na majirani hujawajulisha kuwa umemrudisha kwao.
 
Nenda shule kasome uchumi hela housegirl anayolipwa hapa Tanzania shilling elfu hamsini kwa mwezi ni sawa na 500$ kwa marekani. Kusema hatutaweza kumlipa house girls ni ujinga. Kwa uchumi wa Tanzania shilling 120k ni sawa na 1200$ kwa lugha nyepesi ukimlipa 120k ni sawa na akiwa anafanya kazi USA na kulipwa 2.4M za kitanzania.

Kwa lugha ingine mwajiriwa anayelipwa 1.2m hapa Tanzania ni sawa na mwajiriwa anaelipwa 25m kwa mwezi akiwa anafanya kazi U.K.
Hii biashara ikiwa organized kama nchi zilizoendelea hakuna atakaeweza lipa!

Huku kwetu hii ni total slavery mpaka sasa!

Ni vizuri ina change!
 
Kinachonikera ni siku anakuja unaenda kumpokea ubungo then baada ya mwezi au miezi miwili ukampandishe tena basi ubungo arudi kwao
Mimi hua nawarudisha kwa kuwapandisha bus mwenyewe ubungo sasa akashuke mbezi atajua mwenyewe ila nauli simpi mkononi
 
Yaani unagharamika kutuma pesa ya nauli na ya kula njiani anakaa siku nne unapigiwa simu kwamba huyo binti tunamtaka kuna tiba anataka kupewa baada ya siku moja atarudi, akienda harudi ng'oo, yaani tunapoelekea na hawa wadada sijui.
Kabla hajaja nampa masharti yangu

Akiondoka kabla ya miezi 3 ajigharamie nauli

Siku hizi nimekua na roho ngumu baada ya kuona naendeshwa sana.

Unamtoa mtu katavi hivko baada ya wiki anataka kurudi kwao.....simple maliza mweI mshahara wako ndio nauli yako.....ila kama una haraka sana wakutumie nauli au ujigharamie

ANGALIZO

BINTI AKISHASEMAGA HIVI SIMUACHI MWENYEWW NYUMBANI......LAZIMA KUNA MTU WA KARIBU KWA AJILI YA KUANGALIA NYUMBA NITAMWEKA KWA USALAMA
 
  • Thanks
Reactions: nao
Iko hivi mkuu,

Hao wadada wengi hawatoki mkoani kama unavyoaminishwa. Wanatoka hapo hapo Dar es Salaam.

Kinachofanyika unatuma nauli, inaliwa hafu anakuja hapo anajitia mshamba mshamba ila wanachora tu nyumba yako kama kuna kitu potential wanaweza kukuibia.

Ila wakikuta kuna usalama mkubwa CCTV chumba unafunga so hawawezi iba ndio wanawasiliana na yule dalali akupigie ajifanye kama anahitajika kwao.

Cha kukushauri, usitafute dalali wa house girl, kama unaweza wasiliana na ndugu yako aliopo mkoani au kijijini akutafutie binti anaemjua aje Dar mambo yaendelee.
Nilipata mmoja niliambiwa anatoka tanga

Baada ya kuchunguza nikagundua anatok gongo la mboto

Ila huyu alikaa wiki 2 mazingira hayakuwa rafiki kwake akatoroka mwenyewe...hasara niliyopata ni hela ya dalali

Toka hapo situmii madalali...kwanza ni risk imagine akiumwa itakuwaje???
 
HG wengi wanaletwa kukagua mazingira.

Mimi unakuja kwa nauli yangu ila ukiondoka ndani ya miezi mitatu nakata nauli yangu iliyokuleta. Itakayokupeleka ni yako mwenyewe.

Nasamehe wanao kaa miezi 6 na kuendelea, kitu ambacho hakijawahi tokea.

Hawa watoto hata uwafanyie nini hawanaga shukrani, sijui Wahindi wanawafanyaje?
Aisee yaani hawa wahindi hata mimi sielewagi wanawalisha nini hawa wafanyakazi. Yaani wanalipwa mshahara mdogo,wanateswa lakini hawaindoki wengine wanazeekea hapo hapo
 
Back
Top Bottom