Wadada wa kazi (house maids) siku hizi ni pasua kichwa

Iko hivi mkuu,

Hao wadada wengi hawatoki mkoani kama unavyoaminishwa. Wanatoka hapo hapo Dar es Salaam.

Kinachofanyika unatuma nauli, inaliwa hafu anakuja hapo anajitia mshamba mshamba ila wanachora tu nyumba yako kama kuna kitu potential wanaweza kukuibia.

Ila wakikuta kuna usalama mkubwa CCTV chumba unafunga so hawawezi iba ndio wanawasiliana na yule dalali akupigie ajifanye kama anahitajika kwao.

Cha kukushauri, usitafute dalali wa house girl, kama unaweza wasiliana na ndugu yako aliopo mkoani au kijijini akutafutie binti anaemjua aje Dar mambo yaendelee.
 
Kabla haujamrudisha omba wamtumie nauli mtoto wao kistaarabu tu maana wewe ulituma ya kumleta.

Kama ulituma ya dalali pia dai wakishindwa kulipa sio mbaya heri watume hata nauli aende.

Na kabla hajaja utaambiwa anatolewa Dodoma labda lakini akija ukaongea naye atakujibu mimi nmetokea Ukonga na nina mwaka nipo Dar hapo ndio utachoka jinsì ulivyopigwa.
 
Ruyama

Mkuu

Soma alama za nyakati!

Nchi inaenda kwenye middle class state, nannies ndio mwisho!

Jibane ununue mashine za kutosha kuendeshe nyumba na kila kitu!

Watoto, wapeleke shule mwenyewe, na mama aache kazi arudi baada ya watoto kua wakubwa!

Watoto wasome shule zenye home care features, ambazo ni ghali kupita maelezo!

Otherwise mzee, tunafeli as a society!
 
Nannies bado wako hot sokoni maana hata duniani huko bdo wanahitajika kwa ksii na kwa mshahara mnono either kwa masaa au kwa week tofauti na sisi elfu50 mwezi ndo imezoeleka ukiachana na wale wa Masaki

Hii biashara ikiwa organized kama nchi zilizoendelea hakuna atakaeweza lipa!

Huku kwetu hii ni total slavery mpaka sasa!

Ni vizuri ina change!
 
HG wengi wanaletwa kukagua mazingira.

Mimi unakuja kwa nauli yangu ila ukiondoka ndani ya miezi mitatu nakata nauli yangu iliyokuleta. Itakayokupeleka ni yako mwenyewe.

Nasamehe wanao kaa miezi 6 na kuendelea, kitu ambacho hakijawahi tokea.

Hawa watoto hata uwafanyie nini hawanaga shukrani, sijui Wahindi wanawafanyaje?
 
Tunakoelekea tunakwenda kufungua kampuni ya kuajiri wadada wa kazi unalipa kampuni ila yeye atoe huduma. Akiiba akitoroka Cost ya kampuni hii pangine italeta adabu
Yaani unagharamika kutuma pesa ya nauli na ya kula njiani anakaa siku nne unapigiwa simu kwamba huyo binti tunamtaka kuna tiba anataka kupewa baada ya siku moja atarudi,akienda harudi ng'oo yaani tunapoelekea na hawa wadada sijuuii.
 
Nannies bado wako hot sokoni maana hata duniani huko bdo wanahitajika kwa ksii na kwa mshahara mnono either kwa masaa au kwa week tofauti na sisi elfu50 mwezi ndo imezoeleka ukiachana na wale wamasaki
Wale wa masaki sh.ngapi?
Nb:na mm natafuta kazi za ndani niajiri Hata hapo kwako
 
Kabla haujamrudisha omba wamtumie nauli mtt wao kistaarabu tu maana ww ulituma yakumleta.

Kama ulituma ya dalali pia dai wakishindwa kulipa sio mbaya heri watume hata nauli aende

Na kabla hajaja utaambiwa anatolewa dom labda lakn akija ukaongea nae atakujibu mm nmetokea ukonga na nna mwaka nipo dar hapo ndio utachoka jinsì ulivyopigwa
Uko sahihi, sema shida inakuja pale ukimng'ang'ania halafu akakuletea madhara hasa kwa kuwaletea madhara wanao.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom