Wadada mnisamehe kidogo!

Wadada mnisamehe kidogo!

Simwongelei mtu ni ujumbe kutoka kwa mdau wa masuala ya wanawake anaitwa
Lu-Patie!

Wanaume wengi hawajafikia ndoto zao, wanatamani kupata wanawake watakaowatia moyo kuwafikisha kwenye ndoto zao! Ukweli mchungu ni kwamba wanawake hawawataki wanaume ambao bado wako safarini kuelekea ndoto zao! Wanataka waliokwisha fika, na bahati mbaya zaidi waliokwisha fika wako 'occupied !! Linalotokea ni nini?! Wanawake wanadhani wana bahati mbaya ?!

Unaweza kuwa unalalamika kuwa una mkosi WA kuolewa yaani kila mwanaume anakuja na ahadi nzuri, baadae anakuacha! Lakin upande mwingine huenda maamuzi yako ndiyo maumivu yako.

Kweli huenda we ni mtoto WA kike mzuri wa sura umbo na hata kila kitu ila umenyimwa hekima!

Una mpaparikia kijana mtanashati kisa ana gari na kazii nzuri. Unamwona kijana anaeenda kumbi za usiku ndo mjanja..anae vaa suruali chini ya makalio ndo sahihi kwako lakini yule anaeenda ibada kila ijumaa au jumapili unamwona mruga ruga tu!

Una mpuuza Na kumdharau mtu 'A' kisa tu yeye ni kijana aliye soma ila hana ajira. Ama ni kijana ambae kipato chake hakizidi laki 2 kwa mwezi badala yake una mkumbatia mtu 'B' ambae ni baba fulani na ni mume WA Fulani kisa tu anapesa na shida zako zote anakutatulia...!!

SWALI!!
Utaolewa vipi ikiwa mpaka sasa unapenda toka na waume za watu au vijana wenye magari ya mikopo, au kijana yeyote ambaye unajua huna future naye? Au ndo unam'please ili asiache kukupa pesa!? Nani atakae KUOA wakati vijana wanaotafuta mke wewe una wasema vibaya kuwa hawana hadhi ya kutembea na wewe kisa hawana misuli ya uchumi kwa muda huo?

Funguo ya NDOA utaipata wapi wakati hapo ulipo una mnunia mke wa mtu kisa una toka na mume wake?

DADA maisha yanabadilika mwanaume mpiga debe wa Leo kesho unaweza mbadilisha akawa dereva kisha akamiliki gari lake...hakuna MTU aliye zaliwa kuwa masikini ndo maana juhudi zinahitajika...Mwanaume anae tumia pesa kukufanya uwe wake anafanya hivyo kwa wengi ila usijifanye hujui kisa unafaidika jua muda unaenda.

Weka malengo mbele lini unatamani uwe na ndoa na umri gani uzae kuliko anasa. Mwaka WA ngapi huu bado unatoka na wanaume ambao hawana malengo Na wewe, kazi ni pombe na wanawake?

Umegombana Mara ngapi na Huyo HB wako kisa usaliti na bado upo nae?? Wanaume wangapi wenye pesa mvuto na kila kitu ndani lakin wamekutumia na kukuacha? Lakini bado hujifunzi aina ya mwanaume wa kuwa nae?

Japo vyema acha kujidharau u mrembo onesha kwamba unajipenda kuanzia MAVAZI NA KAULI !
Marafiki zako wangapi waliolewa na wanaume WA kawaida lakin Leo wana mafanikio? Kwa nini usiige..weka uzuri pembeni simama imara kama MKE na MAMA bora WA kesho. Mtie moyo mmeo ajisifu kuwa Na wewe, si kila mara dharau Na kumbeza!!

Kifupi hakuna mwanamme anayependa mke asiyemtia moyo kwa kile kidogo anachofanikiwa kufanya !! Encouragement matters most kwa mwanamme yeyote mwenye akili timamu!
Utakuta mwanamke anafatwa na vijana wengi tuu anawakataa kisa hawana kipato, wewe mwanamke unayetaka wanaume waliofanikiwa jiandae kutendwa tuu hamna la zaidi. Unataka wanaume wenye magar wakati kwenu hamna hata baskel
 
Mawazo kama haya jana nimemwambia mchumba wangu kuwa kama ataendelea na tabia ya kunichit kila muda itafika pahara nisimsamehe tena na moyo wangu ukisha geuka haurudi nyuma. Mimi napenda msichana mwenye kutambua thamani yake na mwenye mawazo ya kimaendeleo hata kwa mtaji wa 10000. Sio kila mda ninunulie gauni lile mara nipeleke kwenye chips.
Mijiwanawake mingine hajielewi kabisa utakuta kutwa nzima anawaza kupiga mizinga tuu, mwanamke ambaye hawezi kutafuta hata elfu mbili ya kwake tupa kuleeeee
 
Asilimia kubwa ya wakaka mafanikio makubwa ni wadada waliwasaidia nyie hamna shukurani.
Wote ni binadamu bhana acha tu.
Sasa hivi ndoa nyingi ni mamario tu wamejaa basi.
So muache kulalamika.
Yaani wanasahu wao wanavyo waumiza wadada, mtu mpo maisha ya chini unavumilia siku katoka anamtupa aliyemvumilia
 
nililo likataa maishani mwangu ni leo kuwa na huyu kesho nipo na mwingine hiyo inakupunguzia heshima halafu kitu kingine hakuna mtu humu duniani asiyependa kupata heshima ya kuwa baba au mama katika familia.
Mwenzio kavumilia mafumanizi mara 3 halafu ni mchumba uvumilivu kiwango cha lami
 
Tatizo wenye navyo wachache au washaoa waliotafuta nao. Wachovu ndio tumejaa mnatukimbia.
Hahaha kwahiyo mmebaki wapweke ndoa karata 3 ukikosea tu umeliwa, na sio wote wameoana
 
Asilimia kubwa ya wakaka mafanikio makubwa ni wadada waliwasaidia nyie hamna shukurani.
Wote ni binadamu bhana acha tu.
Sasa hivi ndoa nyingi ni mamario tu wamejaa basi.
So muache kulalamika.
Ule msemo wa 'nyuma ya mwanaume aliefanikiwa kuna mwanamke' mnakosea kutafsiri.
Mwanamke huyo ni mama yake sio mpenzi.
 
sio kweli ..sio kweli kabisaaa"" kama hivyo usemavyo ni sahihi basiii Mandela angeshapoteza heshima yake baada ya kuamua kumuacha aliyekuwa mkewe winie Mandela "" Jamii itakuvunjia heshima endapo itaona kuwa unaachana na mke/mume kwa minajili ya kuendekeza umalaya( refer yaliyotokea kwa flora mbasha ""). na pia waweza kupoteza heshima ktika Jamii endapo mwenzako atakuwa anakufnyia usaliti na kutembea tembea na wanaume/wanawake hovyo .vitendo vyake viovu vitapelekea kukuvunjia heshima pia.hata familia yako inaweza ikakutenga..hapa ulipo waweza kuwa umeshapoteza heshima kwa watu kwasababu ya vitendo vya huyo gf wako ila kwakuwa huna desturi ya udadisi umeshndwa kulitambua hilo ...
so jiandae kusingiziwa mimba mkuu
Thanks broo for your oppinion
 
bab "" ndoa sio kama mahusiano ya bf/gf ""halafu sikatai kuwa sio kwamba hzo sio tabia za. baadhi ya wanawake lakini sio kwakiwango hcho ndugu ..mwanamke umemfuamania zaidi ya Mara 3 kisha wataka kumuoa ..jiandae kuletewa watoto ambao sio damu yako ..
jiandae kugongeawa na mdogo/kaka yako "" huyo inaonekana umalaya unazunguka kwenye misuli mishipa yake ya damu " kuhusu hilo laupataji pesa ...kupata pesa nijiuhudi zako tu na maarifa pamoja na mipango imara basiiiii" pesa huwa haipatijlkani kwa huo mtazamo maybe uwe umekwenda kwa MGanga then ukaambiwa uitumie nyota yake ...then kama hali ndio iko hivyo kama usemavyo means Siku akikuacha basiii uwe Tayari kujiaandaa kuishi ktk maisha ya dhiki
No kwa mganga me sijaenda but huwa unaamini baraka za mke au mchumba katika mahusiano. Tafuta wazee wenye busara zao wakuelezee hizo baraka. Kuna msichana unaweza ingia naye ktk uchumba ukawa kila siku unapata misala ya kuhatarisha maisha yako na mwingine ukawa unapata baraka tele wakati mwanzo kabla ulikuwa unaishi maisha ya kawaida. But kwa mawazo yako mengine nimejifunza kitu kutoka kwako Thanks
 
1. Ukimpata handsome kichwani ni empty
2. Ukimpata kwenye mapenzi ya dhat walet ina 0.6%
3. Ukimpata msomi busy mapenzi hakuna anawaza in come
Namnukuu MC Pilipili baadae nitakuja andika zipo kama 10
 
1. Ukimpata handsome kichwani ni empty
2. Ukimpata kwenye mapenzi ya dhat walet ina 0.6%
3. Ukimpata msomi busy mapenzi hakuna anawaza in come
Namnukuu MC Pilipili baadae nitakuja andika zipo kama 10
Hujakosea no.2 siku akizipata tu anatafuta mwingine
 
Back
Top Bottom