Wachina wakutwa na hatia ya kuwatupa wazamiaji wawili wa Tanzania baharini

Je hao vijana wetu wa bongo ktk hiyo faini watapewa chochote ingalao wajiliwaze??
Wachina wanatuona watu weusi kama nyani.
Wabaguzi saana vijana chunga kuweni makini??
 
Hawa wana bahati sana, nakumbuka kuna movie inahusu mambo Kama haya sema wale jamaa, walipigwa nyundo na wagiriki mmoja baada ya mwingine ila mmoja ndiye aliyepona.

NB: sikumbuki kama ile movie ni true story.

Alafu waTZ🇹🇿 tujikaze tupambane hapahapa, ukifanikiwa mbona huko ni karibu tu kama unaenda mikoani,
Kama hapa umeshindwa huko utaanzia wapi rafiki yangu mTZ. mpaka mugeuzwe chakula cha papa na familia yake.
 
Kuna nchi moja ya wazungu uko magharibi ya mbali ilishamfanya Mtu mweusi kuwa Rais huku population kubwa in terms of race ni watu weupe. Serikalini na sehemu nyingi nyeti za serikali wamejaa watu weusi kwenye nchi Hiyo.

Pia kwenye nchi Hiyo Ni Bora ukutwe umeiba kuliko kumbagua mtu mweusi. Ni kosa na utatengwa.

Hiyo jamii ipo mkuu.
Tatizo lao ni kukataa kuvaa mask tu,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna nchi moja ya wazungu uko magharibi ya mbali ilishamfanya Mtu mweusi kuwa Rais huku population kubwa in terms of race ni watu weupe. Serikalini na sehemu nyingi nyeti za serikali wamejaa watu weusi kwenye nchi Hiyo.

Pia kwenye nchi Hiyo Ni Bora ukutwe umeiba kuliko kumbagua mtu mweusi. Ni kosa na utatengwa.

Hiyo jamii ipo mkuu.
Mkuu si ungeitaja kabisa tuijue
 
Hawa wana bahati sana, nakumbuka kuna movie inahusu mambo Kama haya sema wale jamaa, walipigwa nyundo na wagiriki mmoja baada ya mwingine ila mmoja ndiye aliyepona.

NB: sikumbuki kama ile movie ni true story.

Alafu waTZ🇹🇿 tujikaze tupambane hapahapa, ukifanikiwa mbona huko ni karibu tu kama unaenda mikoani,
Kama hapa umeshindwa huko utaanzia wapi rafiki yangu mTZ. mpaka mugeuzwe chakula cha papa na familia yake.
DEADLY VOYAGE ya OMAR EPPS.

1587530038646.png
 
Uzamiaji upo duniani kote hata Ulaya,Asia na America kuna watu wanazamia meli kutoka eneo moja kwenda jingine.

Hao wachina wamefanya kosa, na mahakama imetoa hukumu ya faini.
Maisha popote waacheni watu wakapambane.

Wale wote wa kujilipua melini nitawaandikia "SEA ESCAPE PLAN" itakuwa na sheria zinazohusu uzamiaji, haki zako na kuijua meli kuanzia nje mpaka ndani.
 
Heshima yako Chief Engineer,
Ngoja niongezee kidogo hapa kuhusu suala la uzamiaji.

Meli kabla haijatoka bandarini inakaguliwa kila sehemu ili kukagua wazamiaji au kitu cha hatari, hao walifanikiwa kupenya salama kosa walilofanya ni kutaka kuambiwa mwisho wa safari ya meli.

Kitendo cha kuzamia meli hii shambulio la hatari kwa meli, baada ya matukio mengi ya uzamiaji mnamo mwaka 2004 ikaanzishwa sheria ya mambo ya usalama kwenye meli na bandari International Ship and Port facility Security Code (ISPS Code).

Mtu akizamia kwenye meli ni lazima ahudumiwe vizuri kwa chakula na kulala, mfanyakazi yeyote melini aruhusiwi kumfanyia kitendo chochote kibaya Hata kumpiga kofi.

Kwenye ISPS Code kuna vifungu vinavyomlinda mzamiaji na yeye kama mwanadamu. Maana miaka ya nyuma vilitokea vitendo vya kutupwa majini,kupigwa ,udhalilishaji wa kijinsia na matumizi ya silaha za moto melini. Hivyo saizi meli za biashara zinabeba silaha kwa kibali.

Mzamiaji akipatikana kwenye meli analindwa na kutunzwa ili baya lolote lisimkute, maana ikitokea baya adhabu itaenda kuanza na nahodha mpaka wafanyakazi wengine.Faini kubwa itatozwa kwa wahusika na kampuni.

Mzamiaji wakimkuta ilitakiwa wawabebe au wapige simu Port State ya Africa kusini maana meli bado ilikuwa kwenye nchi yao,pia walikuwa wanauwezo wa kwenda kuwashusha bandari inayofata. Baada ya kushuka bandari inayofata wangekabidhiwa kwenye Port State Control ya hapo kisha wapelekwe kwenye balozi yao ili warejeshwe nchini mwao na huko kinachofata watamalizana kwao.
Mkuu nakubaliana na procedures pindi mabaharia wa meli husika wanapogundua kuwa kuna stowaway.
Kuna wakati hao stowaway wanaweza kuwa ni watu waarifu yaani bandits wako tiyari kudhuru mabahari,meli na mizigo yake.
Nakumbuka kisa kimmoja ambapo tuligundua stowaway amejificha pump room kwenye meli iliokuwa imebeba petroli.
Huyu mtu mara baada ya kugundulika alikimbilia deck huku ameshikilia kiberiti akitishia kuwasha moto na kuutumbukiza kwenye matank ya mafuta!!!
Ilituchukuwa muda wa masaa karibu 5 kumbembeleza hajisalimishe akakataa katakata.
Lakini Nahodha alibadirisha njia, bahari ikachafuka sana,bahari ilivyozidi kuchafuka kwa mawmbi mazito alilewa bahari akalegea tukamkamata.
Mkuu hawa vijana wakitanzania wako wengi wenye mawazo ya kupanda meli kwa kuzamia.Hakuna ajira kwa wazamiaji kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.Sana sana ataishia jela au akikutana na wachina watupu sio tu watamtosa bali watamfunga chuma kizito asielee,wanakimbia gharama za kumsafirisha hadi makwao.
 
Nahodha na mabaharia wa Meli ya wachina wawatupa Watanzania baharini kwa hofu ya kuambukizwa Corona

Nahodha na mabaharia wa Meli ya Wachina wamekiri kosa la jaribio la mauaji kwa kuwatupa watanzania wawili baharini kutoka kwenye meli ya mizigo iliyokuwa inaelekea katika bandari ya Durban, Afrika Kusini kwa hofu ya Watanzania hao kuwaambukiza virusi vya Corona.

Wakipewa chupa mbili za maji kila mmoja na jaketi la kusaidia kutozama kwenye maji, Amiri Salamu (20), na Hassani Rajabu (30) waliambiwa kuwa wapige mbizi hadi wafike nchi kavu kwa kutumia mikono yao kama makafi.

Kwa siku tatu, hawakula na walibahatika kusafirishwa na mawimbi hadi katika ufukwe wa Zinkwazi, karibu na Durban, linasema gazeti la Daily Mail la nchini Uingereza.

Mara baada ya kupokea taarifa hizo, The African Maritime Safety Agency ilikamata meli hiyo ya MV Top Grace ilivyotia nanga katika bandari ya Richards Bay na nahodha alikamatwa mara moja.

Nahodha huyo Cui Rongli, pamoja na mabaharia wake Lin Xinyong, Zou Yongxian, Tan Yian, Xie Wenbin, Xu Kun na Mu Yong wote walikiri kosa la jaribio la mauaji katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Durban siku ya Ijumaa.

Nahodha Rongli alipigwa faini ya dola 5000 huku mabaharia wakipigwa faini ya dola 2500 kila mmoja ili kumaliza shauri.

Msemaji wa Jeshi la Polisi la Afrika Kusini, Natasha Cara aliliambia gazeti la Daily Mail kuwa ‘’watuhumiwa waliwapa wahanga majaketi ya uokozi na mabaharia wakawatishia na kuwarusha baharini. Meli ikaondoka na kuwaacha wakiwa baharini. Watuhumiwa wamekiri kuwa kitendo walichofanya kingeweza kusababisha majeraha makubwa na hata kifo’’, alisema

Wakili wa Utetezi, Willie Lombard akiwatetea wateja wake alisema ‘’hatua muhimu za kiusalama zilichukuliwa, na ikiwa mabaharia walikuwa na nia ya kuwa wakatili wangewatupa watu hao mbali kabisa na nchi kavu tena bila jaketi ya uokozi’’

Watanzania hao wamechukuliwa na kupatikwa matibabu na mamlaka za Afrika Kusini na hivi sasa wanaendelea vizuri. Wakati wanaokolewa, walikutwa na hali mbaya ya kiafya inayotokana na baridi na ukosefu wa chakula.

Hivi karibuni, kumeibuka wimbi la malalamiko kwa Waafrika kubaguliwa na raia wa China hasa wale waliopo nchini China. Katika taarifa zilizochapishwa na vyombo vya habari vya kimataifa, inaonesha waafrika wengi wakiwa wametengewa katika maeneo ya umma na hata kufukuzwa katika nyumba wanazoishi na kulazimika kulala nje mitaani kwa madai kuwa wana maambukizi ya Virusi vya Corona.

Hata hivyo, Serikali ya China kupitia msemaji wake ilisema kuwa si sera ya taifa hilo kuwabagua wageni na kwamba ubaguzi wa rangi hauvumiliki.

Chanzo Taarifa:

Daily Mail Newspaper
serengetipost.co.tz

MY TAKE:

Kinachonisitikisha na Kuniuma sana kama si mno GENTAMYCINE ni Kuona Sisi Watanzania ( hasa kupitia Viongozi au Watawala wetu ) wakiwa ' Wanajipendekeza ' kwa Wachina na Serikali yao huku Wachina hao hao pamoja na Kujifanya wanatupenda Watanzania na wanatusaidia kwa Misaada mbalimbali lakini ndiyo hao hao ambao wanatuumiza kama hivi walivyowafanyia Watanzania wenzetu.
Hao viongozi wanaojipendekeza kwa Wachina ni hawa mashetani ya CCM yaliyotukuka ambayo wewe ndo unayapenda au ni viongozi wa Chadema?
Naomba Jibu Tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nakubaliana na procedures pindi mabaharia wa meli husika wanapogundua kuwa kuna stowaway.
Kuna wakati hao stowaway wanaweza kuwa ni watu waarifu yaani bandits wako tiyari kudhuru mabahari,meli na mizigo yake.
Nakumbuka kisa kimmoja ambapo tuligundua stowaway amejificha pump room kwenye meli iliokuwa imebeba petroli.
Huyu mtu mara baada ya kugundulika alikimbilia deck huku ameshikilia kiberiti akitishia kuwasha moto na kuutumbukiza kwenye matank ya mafuta!!!
Ilituchukuwa muda wa masaa karibu 5 kumbembeleza hajisalimishe akakataa katakata.
Lakini Nahodha alibadirisha njia, bahari ikachafuka sana,bahari ilivyozidi kuchafuka kwa mawmbi mazito alilewa bahari akalegea tukamkamata.
Mkuu hawa vijana wakitanzania wako wengi wenye mawazo ya kupanda meli kwa kuzamia.Hakuna ajira kwa wazamiaji kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.Sana sana ataishia jela au akikutana na wachina watupu sio tu watamtosa bali watamfunga chuma kizito asielee,wanakimbia gharama za kumsafirisha hadi makwao.
Kweli mkuu kuna maeneo wazamiaji huwa na lengo la kufanya uporaji au nia ovu.

Mtu akizamia sio tiketi ya kupata kazi, siku hizi mtu mpaka uwe umesoma na kuwa na vigezo.Hao wachina ni tia maji waliona bora wawatupe majini maana wangeingia gharama za kuwarudisha kwao.

Wazamiaji saizi itabidi waangalie meli za kuzamia wakiona meli iliyosajiliwa Panama,Hong Kong,Liberia na nchi zote zenye usajili wa wazi(Open registry) wasithubutu kuzamia maana ni jehanamu ndogo. Wafanya kazi wenyewe wanalipwa pesa kiduchu, malazi mabovu na meli hazina ubora. Stress walizo nazo wafanyakazi wakimkuta mzamiaji hasira wanammalizia kama hao wachina. Mara mia uzamie meli ya mgiriki kwa sasa.
 
Mkuu lete iyo sea escaping plan,ukileta unitag,I like adventure
Uzamiaji upo duniani kote hata Ulaya,Asia na America kuna watu wanazamia meli kutoka eneo moja kwenda jingine.

Hao wachina wamefanya kosa, na mahakama imetoa hukumu ya faini.
Maisha popote waacheni watu wakapambane.

Wale wote wa kujilipua melini nitawaandikia "SEA ESCAPE PLAN" itakuwa na sheria zinazohusu uzamiaji, haki zako na kuijua meli kuanzia nje mpaka ndani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli mkuu kuna maeneo wazamiaji huwa na lengo la kufanya uporaji au nia ovu.

Mtu akizamia sio tiketi ya kupata kazi, siku hizi mtu mpaka uwe umesoma na kuwa na vigezo.Hao wachina ni tia maji waliona bora wawatupe majini maana wangeingia gharama za kuwarudisha kwao.

Wazamiaji saizi itabidi waangalie meli za kuzamia wakiona meli iliyosajiliwa Panama,Hong Kong,Liberia na nchi zote zenye usajili wa wazi(Open registry) wasithubutu kuzamia maana ni jehanamu ndogo. Wafanya kazi wenyewe wanalipwa pesa kiduchu, malazi mabovu na meli hazina ubora. Stress walizo nazo wafanyakazi wakimkuta mzamiaji hasira wanammalizia kama hao wachina. Mara mia uzamie meli ya mgiriki kwa sasa.
Mkuu kuzamia hakulipi ni kuhatarisha maisha.
Ni kosa kuajiri mtu yeyote kuwa BAHARIA bila kukidhi vigezo.
Vijana wenye nia wafuate utaratibu kuepuka madhara ya kuuwawa,kutosawa,Kunajisiwa,kupigwa,kunyimwa chakula, kufungwa lock up baharini, kufanyishwa kazi bila malipo n.k
Sio lazima ufanye kazi ya meli,zipo kazi nyingine nyingi tu.
 
Siku zote ninasema hapa Wachina ni wanyama wanamuona mwafrika kama Covid -19 tu hivi.
 
Jameni yamefika huku, ndugu zetu Watanzania mbona msitulie ndani tu badala ya hizi aibu za njaa, mnaletea hili bara aibu sana, mnapozamia tena kwa kutumia meli za Wachina msitegemee huruma mkikamatwa, Wachina wakatili sana wale, wametosa Watanzania wawili kwenye bahari maeneo ya papa, kwa bahati hawakuliwa, waliokolewa na wanavijiji.
Hivi mnapata wapi ujasiri wa kuzamia kipindi kama hiki, mnakwenda kwenye nchi ya nani ambayo ni nafuu.
Kwa hali ilivyo sasa hivi kila mtu abaki kwao, mskilizie viongozi wenu wanaelekeza vipi, wakishauri kufukiza, basi inakua mwendo wa maji moto kwa kila mtu.
=============================

A Chinese captain of a cargo ship and his crew have pled guilty to attempted murder after throwing two terrified Tanzanian stowaways into a shark-infested ocean over fears of catching the coronavirus from them.

The crew assembled a raft out of plywood, plastic drums and rope, and set the pair of stowaways overboard near South Africa, all with the skipper, Cui Rongli, watching, according to the Daily Mail.

WIth two bottles of water each and a life jacket, the stowaways, Amiri Salamu, 20 and Hassani Rajabu, 30, were instructed to make their way to land using their hands as paddles.

The two men were given no food on the flimsy raft, which was dumped near the mouth of the Tugela River where great whites, hammerheads, tiger and bull sharks are known to hunt, but mercifully washed up on the Zinkwazi Beach near Durban three days later.

The pair were found by horrified locals and were sent to the hospital after suffering from hypothermia, thirst and hunger.

The African Maritime Safety Agency impounded the MV Top Grace when it docked at Richards Bay and the captain was arrested.

Rongli, along with crewmembers Lin Xinyong, Zou Yongxian, Tan Yian, Xie Wenbin, Xu Kun and Mu Yong all pled guilty to attempted murder at Durban Magistrates Court on Friday.

Rongli was fined over $5,000 and crew members were fined $2,500 in a plea bargain.

“The accused … provided the men with life jackets and the crew acted in a threatening manner banging the vessel’s decks as they descended into the raft,” National Police Authority spokesperson Natasha Cara told the paper.

“The ship pulled away leaving them once they were aboard the raft. The accused admitted that their actions could have resulted in serious injury and even the loss of life.”

Defense lawyer Willie Lombard countered, “There were many mitigating factors and if the crew had wanted to be cruel they could have dropped them in the high seas much further out without life jackets.”

Captain pleads guilty to throwing stowaways into shark-infested waters
 
Back
Top Bottom