Wachawi wapo na wanatutesa sana sisi tuliozaliwa kwenye dini.hatujui cha mganga wala nini.
Kuna sehemu niliajiliwa nilikoma nilikuwa silali nachelewa kuamka nikamuuliza jirani akanambia kama sina kinga ya mwili nitateseka. akasema huku hutoweza kuishi.
Niliteseka nikataka kuacha kazi mama alinipa moyo nisaliii yaan nikisali kama ndo nawaita kwa Kasi
Nilienda kanisani nikachukua maji ya baraka na rozali nasaliiiiii mwisho wakapungu.
Nilitoka nilipokwenda chuo sikurudi. Sasa hivi ni mkubwa najua jinsi ya kusali ahasaaa ni maneno gani ya kusali ninapoishi kwa sasa mjini kuna wachawi huwezi amini. Wasomi wake za watu wabibi, na wanaume wachache.
Sijui nini kinanitokea kwa sasa yaan nina uwezo wa kusali na kumwona mchawi tangu mnaingia ndani. Hata niende kutembea sehemu kama kuna wachawi usiku naangaika sipati usingizi na mchawi akiingia ndani lazima nimuone.
Siku moja nimelala nilimwona Ness fulani akaja kanichezea kaniniga, asubuhi nikamwambia mwenye nyumba akasema huyo nesi ni mwalim wa wachawi. Nikakumbuka nilisali kizembe usiku nilikuwa nimechoka Ikabidi niende dukani kwake kununua dawa. Nikamwambia "shingo inauma usiku kuna mama alininiga ila akirudi kwangu hatotoka atabaki ndani hadi asubuhi." Akajisemesha wewe una uwezo gani nilimwambia nasali huwezi kuingia kwangu nisikujue.alianza kuja kupitia sura za watuwengine.ila maombi ndo kila kitu
Biblia yangu inalala kwenye mto na rozali, maji ya baraka hayakosi.nalala vizuri
La kufanya sali sana kabla hujalala kama unavaaga night dress ivae kwa kuigeuza.na kama utaweza weka maji kwenye jagi yaweke nyumbani mchawi hawezi kukugusa. Hizo njia mbili kwao ni mwiko.
Akikuta umegeuza nguo atarudi. Na akikuta maji wanasema anaona kama bahali. Mchawi akiguswa maji dawa zake uisha nguvu.so hawezi kuingia ndani