Wachawi wanikosesha usingizi usiku wa leo

Wachawi wanikosesha usingizi usiku wa leo

simama kwenye Iman mkuu

Sent from my SM-A800F using JamiiForums mobile app
 
Huyo Mwakasege endeleeni tu kumsikiliza matokeo yake ndo hayo ya kutiana hofu zisizo za lazima.Anawapotosheni sana! Mara afundishe juu ya laana,mikosi mara "magundu"! Hivi Mungu wa kweli anaweza kumuumba kiumbe wake na kisha amtie mikosi na laana? Hivi makosa aliyofanya Baba,shangazi yanawezaje kuja kuwadhuru wajukuu au Vitukuu? Hebu waambieni hao wahubiri wenu uchwara watafute njia nyingine ya kuwanasa.Hii technique muda si mrefu nayo watu wataiona hainna mashiko na watawahama vile vile. Ya miujiza imekosa mashiko sasa wanabenderea hii ya uchawi,mikosi na magundu.Hivi huyo Mwakasege kasoma wapi Theology ya uhakika na katika Vyuo Vinavyotambulikana hadi umpe masikio kiasi hicho?
Kama Mungu wa kweli hawezi kumpa mtu laana, pia hawezi kumpa mtu kifo. Maana kifo ni kama laana kuu.

Tunaona kifo kipo.

Unakubali kwamba Mungu huyo hayupo?

Sent from my Kimulimuli
 
sisi watu ambao tumejiwekea urataribu wa kupiga chumba mbili au tatu za laga kila siku jioni tunalala vizuri sana....hayo maluweluwe hatuyaoti....au yanawafata watu wa dini tu?.
 
Hivyo vitu vipo ndani ya akili yako siyo rahisi mtu wa nje akaweza viona
Kutatua Changamoto hizo
1.Usiwe mkristo wa jumapili tu
2.Anza kufahamu asili yako maisha ya wazazi na babu ni nini kilichofanyika tangia wakati unazaliwa hadi hapo hupo
3.Elewa unapokuwa unaomba au unasikiliza Mahubiri yaani kama unayaamsha na moto mkali alafu yanajitokeza kukuzima ili usiendelee kaza spidi nunua bible
4.Anza kuwa mfungaji hata mara moja kwa wiki soma na tumia zaburi 35, 91
5.Ratiba nyingine ya mwakasege ni 107.5 Upendo Radio kuanzia saa 3 ucku...Jumamosi na Jumapili
6.Be commited to God Jitoe mzima mzima ukiwa unabipu una hatari kweli.

Hiyo historia ya Mababu zako toka Adamu na Hawa Mwakasege mdo anaifahamu vizuri? Yeye ndo anaweza kuzichambua vizuri historia za watu wote duniani? Yeye ya kwake nani alimchambulia? Baadhi ya Waafrika mulienda shule kukariri mambo au kung'azwa vichwa vyenu?
 
Dah! Iyo sehemu unayo ishi kama umepanga hama mara moja maana nyumb nyingine maybe ivo viumbe vinafugiwa hapo
 
Uja
Hiyo historia ya Mababu zako toka Adamu na Hawa Mwakasege mdo anaifahamu vizuri? Yeye ndo anaweza kuzichambua vizuri historia za watu wote duniani? Yeye ya kwake nani alimchambulia? Baadhi ya Waafrika mulienda shule kukariri mambo au kung'azwa vichwa vyenu?

Ujaelewa Boss.......Yaani yeye kama yeye aanze kujifahamu asili ya kwake kwa wale ambao wapo au apate mtu ambaye anawafahamu wao lada babu na bibi zake wazaa wazazi wake....ndivyo nilivyomaanisha Mkuu.
 
Wachawi wapo na wanatutesa sana sisi tuliozaliwa kwenye dini.hatujui cha mganga wala nini.

Kuna sehemu niliajiliwa nilikoma nilikuwa silali nachelewa kuamka nikamuuliza jirani akanambia kama sina kinga ya mwili nitateseka. akasema huku hutoweza kuishi.

Niliteseka nikataka kuacha kazi mama alinipa moyo nisaliii yaan nikisali kama ndo nawaita kwa Kasi

Nilienda kanisani nikachukua maji ya baraka na rozali nasaliiiiii mwisho wakapungu.

Nilitoka nilipokwenda chuo sikurudi. Sasa hivi ni mkubwa najua jinsi ya kusali ahasaaa ni maneno gani ya kusali ninapoishi kwa sasa mjini kuna wachawi huwezi amini. Wasomi wake za watu wabibi, na wanaume wachache.

Sijui nini kinanitokea kwa sasa yaan nina uwezo wa kusali na kumwona mchawi tangu mnaingia ndani. Hata niende kutembea sehemu kama kuna wachawi usiku naangaika sipati usingizi na mchawi akiingia ndani lazima nimuone.

Siku moja nimelala nilimwona Ness fulani akaja kanichezea kaniniga, asubuhi nikamwambia mwenye nyumba akasema huyo nesi ni mwalim wa wachawi. Nikakumbuka nilisali kizembe usiku nilikuwa nimechoka Ikabidi niende dukani kwake kununua dawa. Nikamwambia "shingo inauma usiku kuna mama alininiga ila akirudi kwangu hatotoka atabaki ndani hadi asubuhi." Akajisemesha wewe una uwezo gani nilimwambia nasali huwezi kuingia kwangu nisikujue.alianza kuja kupitia sura za watuwengine.ila maombi ndo kila kitu

Biblia yangu inalala kwenye mto na rozali, maji ya baraka hayakosi.nalala vizuri

La kufanya sali sana kabla hujalala kama unavaaga night dress ivae kwa kuigeuza.na kama utaweza weka maji kwenye jagi yaweke nyumbani mchawi hawezi kukugusa. Hizo njia mbili kwao ni mwiko.

Akikuta umegeuza nguo atarudi. Na akikuta maji wanasema anaona kama bahali. Mchawi akiguswa maji dawa zake uisha nguvu.so hawezi kuingia ndani
 
Kwahio kina Petro Yakobo na Mtume paulo walisona wapi thiolojia???

Hata mwisho wa amri kumi neno linasema "Nawapatiliza wana maovu ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukizao nami nawarehem maelfu wanipendao na kuzishika amri zangu"

Sasa hiyo hoja yako ya kusema eti haiwezekani mtu kurithi laana na Mikosi haina mashiko...

Alafu hoja hapa cyo Mwakasege cha muhimu ni kutoa ushauri kwa mleta mada...

We badala utoe ushauri unaanza kushambulia watu....

Sent from my A706s Infinity using JamiiForums mobile app

Kama umemsoma mleta mada vizuri huyo Mwakasege ndiye anayemjaza hayo mafundisho ya kichawi.Kuhusu hilo la Biblia kuongelea laana;una ufahamu gani juu ya Biblia? Hicho unachokisema juu ya kuandikwa kwenye Biblia umekisoma pia katika Lugha mama ya Kiyunani au Kigriki na kukuta maana hiyo hiyo ambayo imekusudiwa na tafsiri ya Kiswahili au Kiingereza? Soma kwanza Historia ya Uandishi wa Biblia kabla ya kujielekeza kufanya kazi ya tafsiri.Petro na Paulo hawakufanya kazi ya kutafsiri Maandiko Matakatifu kwa upotofu kama afanyavyo huyo Mwakasege.BTW, nyakati za Petro na Paulo hakukuwa bado na mkusanyiko wa Maandiko Matakatifu pamoja kama ilivyo hivi leo na wala hawakuwahi wao wenyewe kwa mafundisho ya mdomo au nyaraka zao kupotosha waamini kama anavyofanya huyo jamaa yenu.
 
Uja

Ujaelewa Boss.......Yaani yeye kama yeye aanze kujifahamu asili ya kwake kwa wale ambao wapo au apate mtu ambaye anawafahamu wao lada babu na bibi zake wazaa wazazi wake....ndivyo nilivyomaanisha Mkuu.

Akishakufahamu hiyo historia ya ukoo ndio inamsaidia nini sasa? Ninaelewa sana unachotaka kukieleza hapa.Una maanisha eti aufahamu mti wake wa ukoo na kisha auvunje na atupilie mbali maagano yake? Kama ndivyo, hayo mafundisho ni uongo! Nakuuliza swali: hivi wewe kaka yako akiwa na Mali nyingi asikugawie au kukupa mtaji wa biashara siku akifa na wala usipate sehemu ya urithi wake ina maana siku moja huko mbeleni watoto wako au wajukuu wako nao watatokea wawe matajiri sababu tu ya utajiri wa kakako huko nyuma?

Hivi leo kwa mfano: Manji, Malinzi,Rugemalila na wengineo wanaoshitakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi sasa hivi huko mbeleni watoto,wajukuu au ndugu zao wengineo wa koo hizo Mtawalia (respectively) nao watakuja kushitakiwa au kukutwa na hayo makosa ya uhujumu uchumi hata kama hawatakuwa wametenda makosa hayo?
 
Wachawi wapo na wanatutesa sana sisi tuliozaliwa kwenye dini.hatujui cha mganga wala nini.

Kuna sehemu niliajiliwa nilikoma nilikuwa silali nachelewa kuamka nikamuuliza jirani akanambia kama sina kinga ya mwili nitateseka. akasema huku hutoweza kuishi.

Niliteseka nikataka kuacha kazi mama alinipa moyo nisaliii yaan nikisali kama ndo nawaita kwa Kasi

Nilienda kanisani nikachukua maji ya baraka na rozali nasaliiiiii mwisho wakapungu.

Nilitoka nilipokwenda chuo sikurudi. Sasa hivi ni mkubwa najua jinsi ya kusali ahasaaa ni maneno gani ya kusali ninapoishi kwa sasa mjini kuna wachawi huwezi amini. Wasomi wake za watu wabibi, na wanaume wachache.

Sijui nini kinanitokea kwa sasa yaan nina uwezo wa kusali na kumwona mchawi tangu mnaingia ndani. Hata niende kutembea sehemu kama kuna wachawi usiku naangaika sipati usingizi na mchawi akiingia ndani lazima nimuone.

Siku moja nimelala nilimwona Ness fulani akaja kanichezea kaniniga, asubuhi nikamwambia mwenye nyumba akasema huyo nesi ni mwalim wa wachawi. Nikakumbuka nilisali kizembe usiku nilikuwa nimechoka Ikabidi niende dukani kwake kununua dawa. Nikamwambia "shingo inauma usiku kuna mama alininiga ila akirudi kwangu hatotoka atabaki ndani hadi asubuhi." Akajisemesha wewe una uwezo gani nilimwambia nasali huwezi kuingia kwangu nisikujue.alianza kuja kupitia sura za watuwengine.ila maombi ndo kila kitu

Biblia yangu inalala kwenye mto na rozali, maji ya baraka hayakosi.nalala vizuri

La kufanya sali sana kabla hujalala kama unavaaga night dress ivae kwa kuigeuza.na kama utaweza weka maji kwenye jagi yaweke nyumbani mchawi hawezi kukugusa. Hizo njia mbili kwao ni mwiko.

Akikuta umegeuza nguo atarudi. Na akikuta maji wanasema anaona kama bahali. Mchawi akiguswa maji dawa zake uisha nguvu.so hawezi kuingia ndani

Nenda kamuone daktari.Hata Yesu hakuwahi maisha yake yote hapa duniani kuonana au ku-deal na wachawi! Kwa hiyo jaribu kutafuta tiba ya kisaikolojia.
 
  • Thanks
Reactions: SIM
Akishakufahamu hiyo historia ya ukoo ndio inamsaidia nini sasa? Ninaelewa sana unachotaka kukieleza hapa.Una maanisha eti aufahamu mti wake wa ukoo na kisha auvunje na atupilie mbali maagano yake? Kama ndivyo, hayo mafundisho ni uongo! Nakuuliza swali: hivi wewe kaka yako akiwa na Mali nyingi asikugawie au kukupa mtaji wa biashara siku akifa na wala usipate sehemu ya urithi wake ina maana siku moja huko mbeleni watoto wako au wajukuu wako nao watatokea wawe matajiri sababu tu ya utajiri wa kakako huko nyuma?

Hivi leo kwa mfano: Manji, Malinzi,Rugemalila na wengineo wanaoshitakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi sasa hivi huko mbeleni watoto,wajukuu au ndugu zao wengineo wa koo hizo Mtawalia (respectively) nao watakuja kushitakiwa au kukutwa na hayo makosa ya uhujumu uchumi hata kama hawatakuwa wametenda makosa hayo?

Samahani sitaki jikuza kwa hili....mimi taaluma yangu ni mwanasaikolojia..sijataka sema hicho ulichokifikiria....to know your family background can solve even biological traits or genetic factor before to solve environment and nurture world......hivyo ni muhimu kutrace your origin.......ahsante Mkuu
 
Nyumba nyingine sijui zikoje, mi siku moja nmeona mavitu siyaelewi mchana wa jua kali nliamka nduki, nikabeba nguo za kazini nikahamia kwa ndugu nikaacha nyumba.....nlirudi baada ya miezi 3 kuijia vitu, shwain yule maza hausi
Ukimwaga chumvi au maji ya Baraka ndo umeyaamsha
 
kwanza nikupe pole, fuatilia hiyo habari uliyokuwa unaisikiliza kwa mwakasege then ielewe vizuri kwani inaujumbe wako, na hao jamaa hawataki usikilize ili usivuke.

Swala la imani lisikutishe, kwenye agano jipya hatuitaji imani kubwa sana ili kupata vitu toka kwa MUNGU, tunahitaji kuelewa tunachotaka na kukitafuta, tofauti na agano la kale walihitaji imani sanaaa, lakini kwenye agano jipya ukimkri kristo na kumfuata , Mungu anaachilia agano ndani yako hivyo imani inakuwa limejengwa ndani yako na inakuwa na wewe kila siku, ukishasikia kitu kikaingia ndani yako tiyari unayo imani yakutosha kuvuka hapo ulipo.

Pia achana na swala la maji ya baraka, agano jipya tumepewa DAMU ya YESU kama ndiyo tool ya agano ya kufanyia vitu, ukiweza sema tu NAWASHINDA KWA DAMU YA YESU KRISTO, utaona, then endelea kusoma na kujifunza DAMU ya YESU inafanyaje kazi ni inatumikaje, na utakapo kuwa unajifunza utakuwa unafungua maeneo mengine ya damu ya YESU ambaya ni mengi mno na unlimited.

matumizi ya vitu kama maji, sabuni, vitambaa, mafutaa, chumvi na nk, sio haswaa part ya agano jipya, ispokuwa ni mafunuo ya MUNGU kwa mtu, it cannot work to all equally, standard ni damu ya YESU, mafunuo huja kwa mtu specific na kutatua tatizo lake specific, hivyo sio jambo la kila mtu. Ukipata ufunuo juu ya jambo kama hilo sina shida MUNGU ndiye afanyae, lakini sio unapita mahali unakutana na mtu au mtumishi anakwambia chukua/nunua sabuni au maji ya baraka.

Usipoomba hawaji! sio kweli wanakuja ila hawapati resistance yoyote kwa sababu hakuna cha kuwazuia, ukiweka maji ya baraka hawaogopi kwa sababu sio sehemu ya agano jipya, hivyo ukiomba kwa damu ya YESU leo kesho omba tena, omba tena na tena, tena ,tena, wataacha kuja kabisa, lakini cha msingi omba ukiwa unajua unachofanya na unafahamu namna ya kutumia hiyo silaha unayoitumia.

Silaha tulizonazo ni kama ifuatavyo, ni nyingi sana nitataja mbili kwa kuanzia.
1.Damu ya Yesu,
-kazi yani kutusafisha na dhambi, unaomba msamaha na kujitasha kwa damu
-pia kutupatanisha na MUNGU
-Kufuta uovu wetu
-kuwashinda adui zetu wa rohoni
-Kuvunja nira za uovu
nk

2. Neno la MUNGU
-Kuthibitisha madai yetu
-kutekeleza ahadi ya MUNGU kwetu
-Kutuonyesha Mapenzi ya MUNGU juu yetu
-Kutupa nguvu ya kudai na kushindi
-Kutufundisha na kutuongoza
kwa mfano. MUngu amesema hutakuwa Mkia, ukiwa mkia unajua kabisa kunashida ila sitakiwi kuwa hivi
Mungu amesema umebarikiwa, kama hukuna baraka kuna shida tafuta ufumbuzi.

hiyo ndiyo kzi ya neno. kwa case ya kwako sasa, MUNGU ni mkuu sana na sisi tunatawala pamoja na MUNGU hivyo pepo hatakiwi kukutawala wewe, theni unajifunza kwanini natawaliwa, unatumia ahadi za MUNGU, na silaha zake kama neno na damu unajiweka sawa then unapambana unavuka. kirahisi tu utakuvuka, na kadili unvyojifunza ndivyo unajaa ufahamu na kazi inakuwa nyepesi, chukulia mafano mtu aliyesoea kilimo na aamua kulima, na yule ambaye hajasomea kilimo na akamua kulima pia, aliyesomea atakuwa na utawala mzuri na maarifa ya kilimo zaidi hivyo ni rahisi kufanya vizurii, na yule asiyesomea kwa kadiri anavyolima na kutafuta maarifa ndivyo atakuwa bora na kufanya vizuri zaidi( hapo sio swala la imani bali ni maarifa)

Kama unaye Kristu na bado unaamini kuna nguvu nyingine ya kukutemesha basi huyo yesu wako siyo tunayemjua wote.Atakuwa ni yesu ambaye hakukamilisha kazi yake sawa sawa! Hivi kweli Yesu aliyeshuka duniani akafa na kufufuka hakutosha kumdhibiti shetani kiasi kwamba shetani angali bado anatamba? Kasome vizuri Biblia upya.
 
Jini mkata kamba huyo alikua anakujia kwa madoido..

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Nyumba nyingine sijui zikoje, mi siku moja nmeona mavitu siyaelewi mchana wa jua kali nliamka nduki, nikabeba nguo za kazini nikahamia kwa ndugu nikaacha nyumba.....nlirudi baada ya miezi 3 kuijia vitu, shwain yule maza hausi
Ukimwaga chumvi au maji ya Baraka ndo umeyaamsha

Kama uliyaona kwa macho ungeyapiga picha ukaya-post Insta kwa Mange au FB na hivi leo ungekuwa ushahidi tosha.
 
Kama Mungu wa kweli hawezi kumpa mtu laana, pia hawezi kumpa mtu kifo. Maana kifo ni kama laana kuu.

Tunaona kifo kipo.

Unakubali kwamba Mungu huyo hayupo?

Sent from my Kimulimuli

Kwa uelewa wako kifo ni laana,siyo? Kwa hiyo kuzaliwa ni laana? Kuota matiti ni laana? Kuota mvi ni laana? Kutoka kutembea umenyooka na kisha kutembelea mkongojo uzeeni ni laana,siyo? Mwanamke kukoma kwenda hedhi ni laana ,siyo?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom