Wachawi wanikosesha usingizi usiku wa leo

simama kwenye Iman mkuu

Sent from my SM-A800F using JamiiForums mobile app
 
Kama Mungu wa kweli hawezi kumpa mtu laana, pia hawezi kumpa mtu kifo. Maana kifo ni kama laana kuu.

Tunaona kifo kipo.

Unakubali kwamba Mungu huyo hayupo?

Sent from my Kimulimuli
 
sisi watu ambao tumejiwekea urataribu wa kupiga chumba mbili au tatu za laga kila siku jioni tunalala vizuri sana....hayo maluweluwe hatuyaoti....au yanawafata watu wa dini tu?.
 


Hiyo historia ya Mababu zako toka Adamu na Hawa Mwakasege mdo anaifahamu vizuri? Yeye ndo anaweza kuzichambua vizuri historia za watu wote duniani? Yeye ya kwake nani alimchambulia? Baadhi ya Waafrika mulienda shule kukariri mambo au kung'azwa vichwa vyenu?
 
Dah! Iyo sehemu unayo ishi kama umepanga hama mara moja maana nyumb nyingine maybe ivo viumbe vinafugiwa hapo
 
Uja

Ujaelewa Boss.......Yaani yeye kama yeye aanze kujifahamu asili ya kwake kwa wale ambao wapo au apate mtu ambaye anawafahamu wao lada babu na bibi zake wazaa wazazi wake....ndivyo nilivyomaanisha Mkuu.
 
Wachawi wapo na wanatutesa sana sisi tuliozaliwa kwenye dini.hatujui cha mganga wala nini.

Kuna sehemu niliajiliwa nilikoma nilikuwa silali nachelewa kuamka nikamuuliza jirani akanambia kama sina kinga ya mwili nitateseka. akasema huku hutoweza kuishi.

Niliteseka nikataka kuacha kazi mama alinipa moyo nisaliii yaan nikisali kama ndo nawaita kwa Kasi

Nilienda kanisani nikachukua maji ya baraka na rozali nasaliiiiii mwisho wakapungu.

Nilitoka nilipokwenda chuo sikurudi. Sasa hivi ni mkubwa najua jinsi ya kusali ahasaaa ni maneno gani ya kusali ninapoishi kwa sasa mjini kuna wachawi huwezi amini. Wasomi wake za watu wabibi, na wanaume wachache.

Sijui nini kinanitokea kwa sasa yaan nina uwezo wa kusali na kumwona mchawi tangu mnaingia ndani. Hata niende kutembea sehemu kama kuna wachawi usiku naangaika sipati usingizi na mchawi akiingia ndani lazima nimuone.

Siku moja nimelala nilimwona Ness fulani akaja kanichezea kaniniga, asubuhi nikamwambia mwenye nyumba akasema huyo nesi ni mwalim wa wachawi. Nikakumbuka nilisali kizembe usiku nilikuwa nimechoka Ikabidi niende dukani kwake kununua dawa. Nikamwambia "shingo inauma usiku kuna mama alininiga ila akirudi kwangu hatotoka atabaki ndani hadi asubuhi." Akajisemesha wewe una uwezo gani nilimwambia nasali huwezi kuingia kwangu nisikujue.alianza kuja kupitia sura za watuwengine.ila maombi ndo kila kitu

Biblia yangu inalala kwenye mto na rozali, maji ya baraka hayakosi.nalala vizuri

La kufanya sali sana kabla hujalala kama unavaaga night dress ivae kwa kuigeuza.na kama utaweza weka maji kwenye jagi yaweke nyumbani mchawi hawezi kukugusa. Hizo njia mbili kwao ni mwiko.

Akikuta umegeuza nguo atarudi. Na akikuta maji wanasema anaona kama bahali. Mchawi akiguswa maji dawa zake uisha nguvu.so hawezi kuingia ndani
 

Kama umemsoma mleta mada vizuri huyo Mwakasege ndiye anayemjaza hayo mafundisho ya kichawi.Kuhusu hilo la Biblia kuongelea laana;una ufahamu gani juu ya Biblia? Hicho unachokisema juu ya kuandikwa kwenye Biblia umekisoma pia katika Lugha mama ya Kiyunani au Kigriki na kukuta maana hiyo hiyo ambayo imekusudiwa na tafsiri ya Kiswahili au Kiingereza? Soma kwanza Historia ya Uandishi wa Biblia kabla ya kujielekeza kufanya kazi ya tafsiri.Petro na Paulo hawakufanya kazi ya kutafsiri Maandiko Matakatifu kwa upotofu kama afanyavyo huyo Mwakasege.BTW, nyakati za Petro na Paulo hakukuwa bado na mkusanyiko wa Maandiko Matakatifu pamoja kama ilivyo hivi leo na wala hawakuwahi wao wenyewe kwa mafundisho ya mdomo au nyaraka zao kupotosha waamini kama anavyofanya huyo jamaa yenu.
 
Uja


Ujaelewa Boss.......Yaani yeye kama yeye aanze kujifahamu asili ya kwake kwa wale ambao wapo au apate mtu ambaye anawafahamu wao lada babu na bibi zake wazaa wazazi wake....ndivyo nilivyomaanisha Mkuu.


Akishakufahamu hiyo historia ya ukoo ndio inamsaidia nini sasa? Ninaelewa sana unachotaka kukieleza hapa.Una maanisha eti aufahamu mti wake wa ukoo na kisha auvunje na atupilie mbali maagano yake? Kama ndivyo, hayo mafundisho ni uongo! Nakuuliza swali: hivi wewe kaka yako akiwa na Mali nyingi asikugawie au kukupa mtaji wa biashara siku akifa na wala usipate sehemu ya urithi wake ina maana siku moja huko mbeleni watoto wako au wajukuu wako nao watatokea wawe matajiri sababu tu ya utajiri wa kakako huko nyuma?

Hivi leo kwa mfano: Manji, Malinzi,Rugemalila na wengineo wanaoshitakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi sasa hivi huko mbeleni watoto,wajukuu au ndugu zao wengineo wa koo hizo Mtawalia (respectively) nao watakuja kushitakiwa au kukutwa na hayo makosa ya uhujumu uchumi hata kama hawatakuwa wametenda makosa hayo?
 


Nenda kamuone daktari.Hata Yesu hakuwahi maisha yake yote hapa duniani kuonana au ku-deal na wachawi! Kwa hiyo jaribu kutafuta tiba ya kisaikolojia.
 
Reactions: SIM

Samahani sitaki jikuza kwa hili....mimi taaluma yangu ni mwanasaikolojia..sijataka sema hicho ulichokifikiria....to know your family background can solve even biological traits or genetic factor before to solve environment and nurture world......hivyo ni muhimu kutrace your origin.......ahsante Mkuu
 
Nyumba nyingine sijui zikoje, mi siku moja nmeona mavitu siyaelewi mchana wa jua kali nliamka nduki, nikabeba nguo za kazini nikahamia kwa ndugu nikaacha nyumba.....nlirudi baada ya miezi 3 kuijia vitu, shwain yule maza hausi
Ukimwaga chumvi au maji ya Baraka ndo umeyaamsha
 


Kama unaye Kristu na bado unaamini kuna nguvu nyingine ya kukutemesha basi huyo yesu wako siyo tunayemjua wote.Atakuwa ni yesu ambaye hakukamilisha kazi yake sawa sawa! Hivi kweli Yesu aliyeshuka duniani akafa na kufufuka hakutosha kumdhibiti shetani kiasi kwamba shetani angali bado anatamba? Kasome vizuri Biblia upya.
 
Jini mkata kamba huyo alikua anakujia kwa madoido..

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 

Kama uliyaona kwa macho ungeyapiga picha ukaya-post Insta kwa Mange au FB na hivi leo ungekuwa ushahidi tosha.
 
Kama Mungu wa kweli hawezi kumpa mtu laana, pia hawezi kumpa mtu kifo. Maana kifo ni kama laana kuu.

Tunaona kifo kipo.

Unakubali kwamba Mungu huyo hayupo?

Sent from my Kimulimuli


Kwa uelewa wako kifo ni laana,siyo? Kwa hiyo kuzaliwa ni laana? Kuota matiti ni laana? Kuota mvi ni laana? Kutoka kutembea umenyooka na kisha kutembelea mkongojo uzeeni ni laana,siyo? Mwanamke kukoma kwenda hedhi ni laana ,siyo?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…