Kuniambia nirudie katika uzi wa awali usio na jina wala namba katika ulimwengu wa hyperlink kunaonyesha hama huna ulijualo, ama umepotea njia.Rudia katika uzi wa awali.....nilikuuliza nini. Na kama huelewi Kiswahili tafuta mtu wa kukusaidia ajuaye hiyo lugha.
Wewe hujawahi kupatwa na shida kama ya mwenzetu,Tumeshajadili sana haya mambo humu kuhusu imani za uchawi,wachawi na pilikapilika zao lakini naona watu wana vichwa vigumu! Ninyi munaogopesha watu na hayo "madude" yenu hamna kazi zingine za kujiongezea kipato? Kanisa Katoliki halina mafundisho juu ya uchawi wala wachawi.Kanisa lilishaweka wazi kuwa hayo mafundisho ya kutapeliana na ni ya kukopa.Wewe Charismatic inakuwaje unapingana na mafundisho mama? Hamna njia nyingine ya kujipatia vipato hadi mchukue nafasi kutapeli watu namna hii?
Wewe hujawahi kupatwa na shida kama ya mwenzetu,
Shetani yupo na anafanya kazi tena kabisa.
Nina mke wangu alikuwa na shida za majini nafahamu karaha alizokuwa anapata hasa nyakati za usiku,au akiwa kazini.
Nashukuru kituo cha karismatiki kimenisaidia sana.
Wewe umeandik haya kwakuwa hayajakufika.
SawaSijasema usali kwa kuomba kitu kimoja tu Bali na-discourage kuomba kwa ajili ya vitu visivyokuwepo.Ni kupoteza muda kuomba dhidi ya uchawi,majini,mikosi na au laana.Mambo hayo hayapo na hivi ku-concetrate nayo ni kupoteza nafasi na nguvu zako.
Huko ndo nimefanikiwa mkuu,ndiyo ujue Yesu yupo na anaponya.kama ni ishu ya counseling,nikuombe siku moja ukiona mtu kapandisha mashetani umfanyie hiyo counselingHayawezi kunifika kwa sababu hayapo! Mchunguze mkeo atakuwa na matatizo mengineyo tu ila wewe hujui tu.Hukupaswa hata kwenda huko Charistimatiki.Ungetumia tu counselling angeachana nayo hayo mambo.Wewe utakuwa mwanaume-mwanamke.Una homoni kiasi zinazokaribiana na za mwanamke.Hungekuwa hivyo,ungemu-counsel tu hayo anayohangaika nayo hayapo na hivi asongeshe maisha.
Kuna tofauti kubwa sana kati ya mtu mwenye dini ya kikristo na mwenye imani ya kikristo.........Huko ndo nimefanikiwa mkuu,ndiyo ujue Yesu yupo na anaponya.kama ni ishu ya counseling,nikuombe siku moja ukiona mtu kapandisha mashetani umfanyie hiyo counseling
Kuniambia nirudie katika uzi wa awali usio na jina wala namba katika ulimwengu wa hyperlink kunaonyesha hama huna ulijualo, ama umepotea njia.
Post a link here.
Or shut up.
Huwezi kumfunza mtu ikiwa hata wewe mwenyewe huwezi kuuhakikishia umma wa JF kwamba hiyo post unayosema ipo kweli na si habari uliyoitunga tu.Ni kutaka kukufunza kuwa ujinga wa kuuliza swali hilo hilo kila mara unachosha.
Wachawi hawapalekwi hospitalini mama.Nenda hospitali
Wachawi wapo na wanatutesa sana sisi tuliozaliwa kwenye dini.hatujui cha mganga wala nini.
Kuna sehemu niliajiliwa nilikoma nilikuwa silali nachelewa kuamka nikamuuliza jirani akanambia kama sina kinga ya mwili nitateseka. akasema huku hutoweza kuishi.
Niliteseka nikataka kuacha kazi mama alinipa moyo nisaliii yaan nikisali kama ndo nawaita kwa Kasi
Nilienda kanisani nikachukua maji ya baraka na rozali nasaliiiiii mwisho wakapungu.
Nilitoka nilipokwenda chuo sikurudi. Sasa hivi ni mkubwa najua jinsi ya kusali ahasaaa ni maneno gani ya kusali ninapoishi kwa sasa mjini kuna wachawi huwezi amini. Wasomi wake za watu wabibi, na wanaume wachache.
Sijui nini kinanitokea kwa sasa yaan nina uwezo wa kusali na kumwona mchawi tangu mnaingia ndani. Hata niende kutembea sehemu kama kuna wachawi usiku naangaika sipati usingizi na mchawi akiingia ndani lazima nimuone.
Siku moja nimelala nilimwona Ness fulani akaja kanichezea kaniniga, asubuhi nikamwambia mwenye nyumba akasema huyo nesi ni mwalim wa wachawi. Nikakumbuka nilisali kizembe usiku nilikuwa nimechoka Ikabidi niende dukani kwake kununua dawa. Nikamwambia "shingo inauma usiku kuna mama alininiga ila akirudi kwangu hatotoka atabaki ndani hadi asubuhi." Akajisemesha wewe una uwezo gani nilimwambia nasali huwezi kuingia kwangu nisikujue.alianza kuja kupitia sura za watuwengine.ila maombi ndo kila kitu
Biblia yangu inalala kwenye mto na rozali, maji ya baraka hayakosi.nalala vizuri
La kufanya sali sana kabla hujalala kama unavaaga night dress ivae kwa kuigeuza.na kama utaweza weka maji kwenye jagi yaweke nyumbani mchawi hawezi kukugusa. Hizo njia mbili kwao ni mwiko.
Akikuta umegeuza nguo atarudi. Na akikuta maji wanasema anaona kama bahali. Mchawi akiguswa maji dawa zake uisha nguvu.so hawezi kuingia ndani