Wachawi wanavyoiba nyota za watu wanafanyaje?

Mkuu kuna jamaa huko mwanzoni aliandika umchekie yeye ni amezaliwa November 22nd. Naona umemruka
Namba zako za bahati ni :3, 12, 21, 30

Una bahati ya kuzaliwa

Kazi nzuri kwako ni yoyote inayohusiana na mauzo (sales) sababu unaongea sana tena bila kuchoka

Kazi nyingine nzuri kwako ni zile zinazohusiana na masuala ya utalii na shughuli za nje (outdoor activities)

Mchawi wako mkubwa ni kuongea bila kufikiri, kutumia hela hovyo na kupenda sana kuwa huru
 
Kazi nzuri kwako ni u-nesi, siasa na uandishi wa habari

Namba zako za bahati ni
2, 7, 11, 16, 20, 25

Wachawi wako wakubwa ni
Tabia ya kubadilika badilika(kinyonga) , kukata tamaa , kuchunguza chunguza vitu, kutokujiamini, na kutapeliwa kirahisi
Mkuu niangalize hii 27/9
 
Sio KILA nyota ya mtu inaibiwa kumbuka hawa wapumbavu sio kwamba wanayo nguvu kubwa kuliko wote,kama unayo nguvu ya Mungu awakusogelei sio wewe tu hata uzao wako ikiwemo hata ulio tumboni,wakisogea tu kutaka kuchezea nafsi yako,mali yako, watoto wako nk upigwa shoti kali kama moto wa gesi na awakugusi tena.
Hawa wapumbavu waganga na wachawi nao ni waoga pia Ili wakuroge ni lzm wafanye test kukupima kwenye radar zao wanapima nguvu iliyomo ndani yako kama ni kubwa kuliko yao hawataki shali na wewe.
Hata kwenye usafiri mfano basi wakitaka kutoa kafara kwa kusababisha ajali ambayo mara nyingi huwa wanaliangusha au kuyagonganisha magari hapa unakuta dereva kaacha njia kamfata mwenzake au wanaifanya barabara inakua moja kwa kuifanya iwe nyembamba mara paa uso kwa uso kama katika basi hilo walilokusudia kuna mtu anayo nguvu ya Mungu uharisha na awaligusi gari hilo maana upigwa shoti hatari.Wanatumia kifaa kinaitwa (icds) asidiizi ni testa za kichawi kupima nguvu aliyonayo mtu kabla ya kumdhuru kichawi.
Nipende kuwatia nguvu hawa wapumbavu hawana lolote wala chochote cha kushinda nguvu aliyopewa mwanadamu na Mwenyezi Mungu wanachoweza ni kutia uoga na hofu, hofu ndio silaha kubwa hawa wapumbavu uitumia kudhuru.
Kama wamepanga kutoa kafara kwenye gari lakini katika mmoja wa wasafiri alimuomba Mungu ailinde safari hio tayari hapo kunakuwa na nguvu ya Mungu kwa vipimo vya radar yao hawawezi lisogelea,na wakishindwa kuliangusha ukumbana na adhabu kali Sana toka master wao yaani shetani ikiwemo kutakiwa kutoa kafara ndugu au mtoto wao au mtu wa karibu,so ukiwa na ndugu, au rafiki mchawi tambua upo kwenye risk ya kutolewa kafara.Wachawi na waganga ni mateka wa shetani wengi wapo kifungoni kwa matishio wakitoka,wakiacha watauwawa na kupelekwa kuzimu kutumika kimateso ambayo wao uyashuhudia, mchawi na mganga wanayo password ya kuingia kuzimu kupokea maagizo.Mchawi na mganga awanywi damu labda kidogo lakini damu utolewa sadaka kwa shetani.
Kwann ulimwengu wa Sasa Siri za giza ziwe wazi,Mungu karuhusu tuzijue siri zao Ili tusiwaogope,ukishamjua adui sio tishio tena kwako.

Interesting nimekumbuka story ya Lwanda magere alivyokuwa akitumwa kupindua magari ya abiria, jaribio likifeli basi adhabu yake ni kuua ndugu yako tena yule unayempenda hasa.
 
Kuibiwa nyota cha mtoto,wengine wanaiba hadi ufahamu wa mtu unabaki kama pampula.
 
Uchawi upo na kweli mtu anaweza kuiba nyota yako kwa kupitia alama za kiganja chako

Umewahi kujiuliza watu wanaoenda kwa waganga kwanini huwa wanaangaliwa viganja vyao?

Ni kwa sababu akiona una bahati anakuibia na usiniulizi kivipi maana mimi sio mchawi na ninayapuuza sana ingawa yapo

Wengine huwa wanakuwa na mikosi na mambo yao hayaendi kwa sababu wako karibu na watu wenye husda na jicho la husda kwani kila unapofanya kitu kinaharibika

Kuanzia biashara, Kazi, Ndoa na hata safari basi ujue kuna mnafiki wa karibu unaemuona ni mzuri kumbe hakutakii Jema lolote na wewe kila jema lako unamwambia halafu linafeli

Ila siku ukimjua na ukimlamba block kwa kila sehemu hata salamu basi mambo yako yatabadilika

Huyo sio anaiba nyota yako hapana anaichoma kabisa
Umeeleweka sana mkuu. Mimi juzi kwenye kundi la Whatsapp la ofisi niliwachana na mtu niliyekuwa ni target yangu ujumbe aliupata na baada ya siku moja tukawa na kikao akawa hana amani.Uchawi wa kuiba nyota upo na huwa wakishindwa, wanaichafua .
 
Unajuaje yote haya mkuu?

Kwa mfano nikienda kwa mganga anaweza kuona haya yote?

Yanaonekanaje?
Mambo ya nyota ni mambo ya kiroho na yako katika ulimwengu wa roho. Ni kweli mtu au watu uweza kuiba au kuchukua nyota ya mtu. Yaweza kuwa kwa njia za kichawi, majini, au nguvu zozote zile za giza katika ulimwengu wa roho. Haya mambo yamekuwepo enzi na enzi.
Katika Biblia Mathayo 2:1, 2. Kuna wise men( wenye hekima au Watabiri nyota) waliuliza

"yu wapi mfalme mpya alozaliwa, maana tumeona nyota yake tulipokuwa mashariki".

Hii haikumaanisha nyota kama nyota ya mwonekano. Na utajiuliza kwa nini hawa wisemen watatu ndo waliona hii nyota si wengine. Herode alituma watabiri wakaangalie yu wapi huyu Yesu alozaliwa. Hawa jamaa baada ya kufika kule walimwona Yesu na Mamake. Walipotaka kuondoka waliona nyota ya yule mtoto Yesu imechafuka ikionesha mauaji ya mtoto mdogo asie na hatia. Ndipo Mungu akawambia wasirudi kwa Herode. Mathayo 2:12.

Nimenukuu kutoka katika Biblia kuonesha binadamu tunanyota na nyota ndo muongozo wa maisha. katika nyota unaweza mjua mtu ni nani na atakuwa nani. Haya mambo yapo katika Ulimwengu wa roho. Hawa watabiri wa nyota tayari walishaona nyota ya mtoto aliezaliwa na walisema mfalme mpya alie zaliwa. Hivyo nyota ya Yesu ilionesha ni mfalme. Hii ilimuuzi Mfalme Herode na kuamru watoto wadogo miaka 2 hadi 0 kuuwawa.
Maswala ya wizi wa nyota ni somo refu saana. Kwa kifupi!
Viganja vya mkono uonesha nyota ya mtu. Hii ni pamoja na nyayo.
Paji na macho uonesha nyota ya mtu.

Kuwa makini na mtu anae kutazama sana katika paji lako au machoni huku kakaza macho yake. Na hasa anaweza kukuangalia wakati weye umeyumbisha macho umuoni uzuri. Kuna uchawi wa macho. Nchini Ethiopia, uchawi huu hutumika hasa mtu anapokuwa na kinyongo nawe, au kijicho. Hivyo uchukua nyota yako nawe kubaki unaangaika sana.

Kuna kitabu kinaitwa "Mind of an Eye" kama sijakosea ni kikubwa kwa wingi wa page. Na pia ni kipana. Kimeeleza mengi juu ya nguvu za jicho. namna binadamu unavyoweza kubadilika hata ukatoweka mfano upo Dar lakini ukafika Mwanza hata arabuni. kinafundisha uponyaji na mambo mengi katika ulimwengu wa roho.

Hivyo jicho linaweza chukua nyota ya mtu. Ndo maana mtu anaweza sema fulani kaniangalia kwa jicho baya. Jicho linanguvu za ajabu kwani uweza kuona hata yalofichika.
Nyayo au kiganja kimebeba mwili wa mwanadamu. Taswira ya mtu unaipata katika nyayo au kiganja chake. Ndo maana wengine, uchota nyayo za mtu ili kummaliza. Au uchukua maandishi ulioandika kwa viganja vyako. hata kama ni karamu ilikamatwa na kiganja hivyo ni rahisi katika ulimwengu wa roho kuchukua reflection yako.

Kuna kuchukua nyota yako kupitia jina la ukoo wako, jina la ukooo linanguvu na hasa kama ni la babu yako. haya majina hutumika kukujua vizuri wewe na ukoo wako. Nguvu zenu kiroho na nyota yako.
Mchawi hawezi kuroga kama yupo kawaida, mpaka ajibadili aingie katika ulimwengu wa roho. ndiyo maana huwezi mshika au hata kumuona.

Anapoamua kuonekana kuna jambo au pia wewe katika ulimwengu wa roho unanguvu. Hivyo kuichukua nyota yako itahitajika kwanza aifahamu, na afahamu ukoo wako kisha katika ulimwengu wa roho anaiiba au kuichukua nyota yako.

Na mara nyingi hawaichukui wawe nayo wao lah asha. Wanaiondoa tu kwako ili pengine usifanikiwe, uteseke, au tu uangaike. Kwani ni ngumu nyota ya mtu kutumika kwa mwingine. Hivyo wakiichukua maana yake wanaondoa baraka zako, wanakufunga. isipokuwa hawawezi kuitumia nyota yako.

Narudia tunatumia tu neno nyota uchukuliwa, si kwamba wanaichukua waitumie hapana. Uwezi tumia nyota ya mtu mwingine kwa sababu kila mtu anapozaliwa uzaliwa na nyota yake. Kikubwa wanaiondoa ile nyota kwako, kwa sababu za husuda, roho mbaya, na mengineyo ili ubaki ukiteseka na usifikie ambacho nyota yako inaonesha hapa duniani ungekuwa nani, au mtu wa namna fulani.
Hivyo nyota yako ufichwa mahala. Ndo maana katika maisha omba, ombea wanako au familia. Ili Mungu akulinde weye na familia yako. Unajua kuna watu wa ajabu ktk hii dunia, mtu akiona weye ni mzuri ktk jambo fulani au umefanikiwa kiasi fulani basi anakumaliza kwa ulimwengu wa roho.
Japo kuna watu wanajifanya hawaamini haya mambo lakini yapo. Yana nguvu sana. Kuwa makini na watu ulionao karibu. Hao ndo wakwanza kwa kijicho na husuda. Mtu hata kama si mchawi atakuendea kwa wataalamu au waganga ili waiharibu nyota yako. Usifanikiwe! Kila siku utajiona ni mtu wa mikosi na balaa. Au unajitahidi kufanya hiki hakiendi. Wanafunga nyota yako!
 
Fanya Sanaa na utakuja kunishukuru

Wewe ni msanii wa kuzaliwa, Angalia hata jina lako hapa JF

UNA Nyota kubwa ya kuwa mtu maarufu mkubwa

Una nyota kama ya SIMBA

Pia una tabia ya ubishi na unaweza kumbishia mtu yoyote

Kuna wengi wanaokuloga na mkuu wa hao wachawi kwako anaitwa EGOISM
Na Mimi mkuu nichekie
 
Kuibiwa nyota cha mtoto,wengine wanaiba hadi ufahamu wa mtu unabaki kama pampula.
Baadhi ya Walimu, manesi na madaktari wanatajwa sana kwenye wizi huu wa ufahamu wa wanafunzi na wagonjwa.

Tutapataje kupona namna hii?

Ole wako Korazini Ole wako Bethsaida kwa kuwa mambo haya yangelifanyika Tiro na Sidoni wangelitubu siku nyingi!
 
Kazi nzuri kwako ni u-nesi, siasa na uandishi wa habari

Namba zako za bahati ni
2, 7, 11, 16, 20, 25

Wachawi wako wakubwa ni
Tabia ya kubadilika badilika(kinyonga) , kukata tamaa , kuchunguza chunguza vitu, kutokujiamini, na kutapeliwa kirahisi
..."Wachawi wako wakubwa ni
Tabia ya kubadilika badilika(kinyonga) , kukata tamaa , kuchunguza chunguza vitu, kutokujiamini, na kutapeliwa kirahisi"...

Mkuu Nashukuru sana..
Naomba unisaidie jambo moja kufaham wachawi wangu ... ni tabia nilizo TUPIWA ili nisifanikiwe na watu au ni ASILI tu ya nyota yangu????

Na je! Kuna njia yoyote ya ziad ya kuziondoa Au niseme TIBA yake ni nini auipoje???

Ntashukuru sana ukinifahamisha mkuu
 
NILICHOJFUNZA NDANI YA UZI HUU
-> Nlahisi kdogo kupambana na roho
Unayoihisi kuliko kupambana
na roho Ambayo hata kuihisi uhisi

"Ngoja NIJARIBU kuelezea nlicho jfunza katika uzi huu NIONE kama NTAWEZA"

Hapo juu ni mstari wa kwanza nilioanza kuandika ila kipindi nilpo fka kuandika neno NIJARIBU akili yangu ikani alert hapa kwamba umevamiwa na mchawi wa kutojiamini ... nkasema ngoja niandike mstari ambao hautokuwa na nguvu Za kutojiamini na mstari wa pili ambao umekamilika ukiwa umejawa na nguvu ya kujiamini ndani yake ni huu apa ( nyota safi kabis)...

"Ngoja nielezee nilicho jifunza katika uzi huu".

Tunaendele na nilichojfunza sasa..
Ambacho nlikuwa sina picha nacho juu ya tabia/nyota ni kwamba tabia ni roho au watu kabisaa

Nmesema ni watu kwa sababu roho katika ulimwengu wa roho ni sawa na watu katika ulimwengu wa wanyama

Apo mwanzo kabla ya uzi huu na wakufunzi kufundisha juu ya nyota nlkuwa sina hii alert ya kuona kwamba saiv roho gani au mchawi gani kanivamia katika hisia zangu,


Kwa mfano nlpokuwa naandika paragraph ya kwanza unconsciously nlkuwa sioni mlango ambao roho/mchawi wa kutojiamini anaingilia..
Ila baada ya kupata picha ya wachawi wangu ni kutojiamini,tabia kubadilika badilika nk... sasa mentality nawaona ,
kwa sababu nimezchukulia hizo tabia kama watu .
Hiyo inamaana kwamba unapojisikia au unapo hisi kutojiamin maana yake kwamba mchawi wako kawasili mwilin mwako au kwenye nyota yako au kwenye tabia yako

Uzuri ni kwamba hisia zote Za kutojiamini au uvivu nk.. ukzchukulia kama watu wachawi wako unaziona znavyokuvamia kwenye mwili wako

Kingine nahisi.... Hisia ni njia ya kukuonesha mchawi gani kakuvamia
Ukijihisi uvivu jua kabisa wanyamwez wa kutotaka usifanikiwe wAnafanya kazi yao , au kbuyu walichokuwekea kmetkisika uko .. hahah

Nilitaka kumalizia na mstari
"Sijui nmeeleweka", ila nmegundua kuwa huo ni mlango wa mchawi kutojiamini anao ingilia

............. ........... ....... ........... ..........


shukrani kwa walimu wote wanao hakikisha jamii inapata uelewa sahihi wa nyota
 
habari za uchawi ni uongo na utapeli . Tuanze zungumzia nyota , nyota na binadamu wanamahusiano yapi sijaona uhusiano kati ya hydrogen za kwenye nyota na binadamu duniani.
tuje kwenye uchawi, mchawi anawezaje kuzuia binadamu mwenzaje asifanye jambo tena kwanamna ambayo sio kisheria wala kimafizikia. Habari za wachawi ni zakusimuliwa hamna mtu huja kusema amemshuhudia mchawi bali husema amesimuliwa.
ndugu zangu watanganyika tuwekeze kwenye sayansi ya kweli tuachane na hekaya hizi mambo hayo ni yazamani sana hayana ukweli wala uhalisia
 
Back
Top Bottom