Wachawi kutumia wanyama wanafanya kile wafuasi wa Mungu walichoshindwa kufanya

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,632
15,439
Wachawi wanaweza kupanda mkuki, ufagio au ungi wakasafiri hadi nje ya bara kwa sekunde.

Wanaweza kuwaamrisha fisi, mamba, paka, mijusi hata mbwa kufanya wanachotaka wakati wowote bila kubisa.

Ni aibu kubwa mtu kujiita mfuasi wa Mungu mwenye nguvu zote wakati huna uwezo kwa Kucheza na vitu vya asili katika mlengo chanya. Mfano kuagiza kwa tamko moja ujikute uko DSM bila nauli kufumba na kufumbua.

Kwenye Biblia waliweza sisi kimetukumba nini.

Yesu aliongea na upepo ukamsikia na kutii.

Petro aliongea na maiti ikaamka.

Elisha aliongea na shoka ikaelea.

Philipo alisafiri hadi Gaza kufumba na kufumbua kutokea samaria bila chombo chochote kwenda na kurudi.

Musa aliongea na bahari ikaachia njia.

Nini chanzo cha huu uchovu wa kiroho kiasi kwamba wacha Mungu wanazidiwa miujiza na wafuasi wa kashetani kaadui mufirisi.

Tatizo ni nini?
Mungu wa siku za mwisho kapoa makali?

Sisi ndio tunazingua?

Wanatuzidi ujanja gani katika ulimwengu wa roho hawa jamaa hadi mida hii naandika wako wengi tu angani wanakula route mikoani bure.
 
Cyo mishen tuliyopewa.tumepewa maagizo ya kuwafanya watu kuwa wanafunz wa yesu kwakubatiza kwa jina la baba na mwana na roho mtakatifu.hayo mengine ni ya ziada
 
Hayo amesema yanatakiwa yaambatane na hilo zoezi.

Unadhani kwa nini wale wa kwanza waliopewa hii mission kazi yao iliambanatana na kishindo hicho lakini hii ya kisasa kama imechuja na ukioma hata mtu anasema anafanya maajabu basi ni ya kuforce au mazingaombwe
 
Mbona kuna mengi tu mkuu ata yesu akija ata toa macho tu.

1. Kuwasiliana na mtu na kifaa( simu) hata kama yupo bara jingine.

2. Kuona matukio mbalimbali duniani kwenye kifaa tu chumbani kwako .( television) .

3. Watu zaidi ya 200 na mizigo kupaizwa angani kwenye chombo ( ndege) bila kuanguka chini.

4.kifaa kama gari kutembea kwa mwendo kasi zaidi ya farasi kikiendeshwa na mafuta tu huku kikiwa na abiria wa kutosha.

5.Majengo marefu kuliko mnara wa babel na Mungu kavunga.

6.kamera ,drone za kivita, umeme, rocket , meli kubwa kabisa za kifahari na mambo mengi tu ni maajabu tosha Yesu mwenyewe akija atazima fegi
 
Nawaza wachawi wanavyotumia mijusi
Mchawi anatumia kiumbe chochote au kitu chochote. Kuchagua viumbe na kujiogopesha ni uongo.
Kikubwa na wewe ukiwa na Mungu unauwezo wa kuamuru chochote hlikiwemo hivyo viumbe vya kichawi kufanya unachotaka.
 
Mbona kuna mengi tu mkuu ata yesu akija ata toa macho tu.

1. Kuwasiliana na mtu na kifaa( simu) hata kama yupo bara jingine.

2. Kuona matukio mbalimbali duniani kwenye kifaa tu chumbani kwako .( television) .

3. Watu zaidi ya 200 na mizigo kupaizwa angani kwenye chombo ( ndege) bila kuanguka chini.

4.kifaa kama gari kutembea kwa mwendo kasi zaidi ya farasi kikiendeshwa na mafuta tu huku kikiwa na abiria wa kutosha.

5.Majengo marefu kuliko mnara wa babel na Mungu kavunga.

6.kamera ,drone za kivita, umeme, rocket , meli kubwa kabisa za kifahari na mambo mengi tu ni maajabu tosha Yesu mwenyewe akija atazima fegi

Nakumbuka wakati mitandao ya jamii inaanza,wafuasi wa dini walikua wanasema ni mitandao ya shetani/freemason,chakushangaza sasahivi wamejazana huko kuomba sadaka
 
Wachawi wanaweza kupanda mkuki, ufagio au ungi wakasafiri hadi nje ya bara kwa sekunde.

Wanaweza kuwaamrisha fisi, mamba, paka, mijusi hata mbwa kufanya wanachotaka wakati wowote bila kubisa.

Ni aibu kubwa mtu kujiita mfuasi wa Mungu mwenye nguvu zote wakati huna uwezo kwa Kucheza na vitu vya asili katika mlengo chanya. Mfano kuagiza kwa tamko moja ujikute uko DSM bila nauli kufumba na kufumbua.

Kwenye Biblia waliweza sisi kimetukumba nini.

Yesu aliongea na upepo ukamsikia na kutii.

Petro aliongea na maiti ikaamka.

Elisha aliongea na shoka ikaelea.

Philipo alisafiri hadi Gaza kufumba na kufumbua kutokea samaria bila chombo chochote kwenda na kurudi.

Musa aliongea na bahari ikaachia njia.

Nini chanzo cha huu uchovu wa kiroho kiasi kwamba wacha Mungu wanazidiwa miujiza na wafuasi wa kashetani kaadui mufirisi.

Tatizo ni nini?
Mungu wa siku za mwisho kapoa makali?

Sisi ndio tunazingua?

Wanatuzidi ujanja gani katika ulimwengu wa roho hawa jamaa hadi mida hii naandika wako wengi tu angani wanakula route mikoani bure.
Siku hizi unaongea Ukweli mtupu Asante kwa hilo!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom