SIERA
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 2,789
- 3,407
Dah wadada was kichaga Mungu anawaona!
Mwaka 2017 nilipata ajira mahala Fulani,nilibahatika kufahamiana na dada mmoja wa kichaga,mzuri mwenyewe kaolewa na mchaga mwenzie wamebarikiwa watoto wawili wa kiume.
Tukawa karibu sana mara kwa mara akinieleza changamoto za mahusiano yake,kero yake kubwa ilikuwa ni mumewe ambaye alikuwa hatimizi majukumu yake ipasavyo ya kumpatia pesa za kutosha na wakati yeye anajua anazo.Yule Dada alinishangaza kwa mdomo wake alinisimulia ameenda kwa mganga kampa mganga laki 5 amuue huyo bwana,mganga akamwambia chagua siku akachagua siku ya jpili,hapo nasimuliwa Ni alhamisi ameenda kusuka nywele zake nzurii,ananiambia kesho naenda karume kununua masweta ya watoto Ilala maana tutasafirisha Moshi ni baridi...Ndugu zangu niliona KIZUNGUZUNGU,nilimuombea huyo mbaba Kama mtoto niliyemzaa jamani nilimugopa yule Dada sana..Basi bwana kufika hiyo jumapili ya ahadi Mjuba kaamka mzimaaa,bidada kapagawa, jumatatu ilivyofika asubuhi mbio mpaka alipofikia huyo mganga anaambiwa kaondoka jumamosi karudi huko kwao Tabora,
Basi kaingia kibaruani Kama saa nne haeleweki anadai mganga kamtapeli..Nilianza kujitoa ukaribu nae taratibuu ,nahisi aligundua Kuna siku nikawa nae akaniambia yaani najuta yule shetani aliyenipitia nimeshatubu...Hapo ndio nilijua true colors za wachagaaa..
Wanawake na wanaume wa kichaga wanapenda ushirikina sana sana haswa linapikuja swala la mali Yaani lazima ushirikina uingie wengi wao..
Na kwenye ishu za kuuwa wanawake wao wanapenda sana ushirikina