Naona niweke thread hii itakayokuwa inajadili mambo yanayohusiana na sisi wachanga
Kwanza nianze kwa kuuliza: Hivi Wachaga ni kabila, au ni mkusanyiko wa makabila? Maana makabila mengine mengi wenzetu wana lugha moja ya kikabila. Ila sisi tuna vilugha zaidi ya 10 tofauti! Kwa nini?
Kwa mfano mimi nikiandika kwa kichaga cha kwetu (kiseri) kusema "Naomba maji ya kunywa", ni "Nglihemba mringa wenywa"
Hivi kwa wale ambao sio waseri, hapo mtasemaje? (naamini lugha zitatofautiana sana)....
Ngi Terewa muda weena.....shitehewa muha ,ngiterewa Mringa wonyo..etc.
Haha hata wapare ni mkusanyiko wa makabila.Pengine ingawa ni wengi wamchanganya, makabila mengine yalifanikiwa ua lugha nyingine.
Thats the power of these guys.Ni self contained culture..imebeba vionjo vya kutosha wapa changamoto ndani ya kilimanjaro kwa kiasi cha kuwafanya wawe flexible wakitoka nje.
by the way wengine si makabila kihivyo ila jinsi familia zao zilivyokuwa loose ktk kuingiliwa na lugha nyingine.Mfano kuna wazungumzaji wengi tuu wa lahaja zote ambao wamekuwa affected na kiswahili kiasi cha kufanya lugha ikiongelewa basi mzungumzaji w akiswahili anaweza sikia..Hii hata kwa Wapare, wasambaa imeingia sana...
Ni wachache sana jua lugha zao kwa asilimia zaidi ya 95...nakumbuka mzee wangu alikuwa akinipia maneno ya sahihi ya vitu km pikipiki, magari, majina ya vyakula, matukio etc nilifurahi kwa jinsi ilivyo romantic...by far kiswahili pamoja nakupewa umuhimu na mwendelezo ktk sayansi.
Hakina maneno sahihi ktk issue km imagination, kebehi, majigambo, ...kuna maneno hata ktk kiingereza huwezi yapata ila ktk kichaga cha kwetu....huwa naya feel sana.
Ushishangae sana kwani siku zinavyokwedna utakuta lugha nyingi zikisemwa kwa kutoahowa kiswahili au kingereza.