Wabunge wetu wanaidharau bendera ya nchi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wetu wanaidharau bendera ya nchi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Jun 29, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kwa kila anaeangalia vipindi vya Bunge la Tanzania katika TV ataona ni jinsi gani wabunge wanavyoikanyaga Bendera ya Taifa hili la Tanzania ,kwa vyovyote vile iwavyo wanaidharau Bendera yetu hii ambayo inaposhushwa kwenye mlingoti haitakiwi iguse chini ,iweje wabunge wawe wameitandika kwa marefu na mapana na halafu wanaikanyaga kwa viatu vyao vilivyojaa mavi ya kuku ? Hii ni dharau na jeuri au ndio ustaarabu ? SIjawahi kuona Nchi yeyote ile imeweka bendera yake chini na viongozi wanaikanyaga iwe ndani ya bunge au sehemu nyengine yeyote ile.
  Kwa kuhisia tu mbunge anapoikanyaga pale huwezi kujua anapitiwa na fikira gani zaidi ya kuwaza kejeli ?
  Je huu ni uungwana maana hata Raisi hatandikiwi Bendera .
  Naomba kuwasilisha hoja ya kuondolewa zulia hili la bendera ya Taifa ndani ya Bunge letu ili liwe tukufu vinginevyo halifai kuitwa Bunge takatifu wakati linaichafua na kuikanyaga bendera ya Tanzania kwa viatu
   
  Last edited by a moderator: Jun 30, 2009
 2. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  hili nilishalisema nikaambiwa naina mind vutu vidogo vidogo..that was 2005
   
 3. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Hata mimi ina niboa, hakuna utofauti wa kukanyaga katiba ya nchi ukasema ni karatasi tu, hakuna utofauti na kuchukua ukurasa wa Kitabu cha nyimbo kanisani ukapulizia moto. Kama Nguku wa Zabanga Sese seko alichukia alipoona mwanamziki mmoja ametandika mapazia kitambaa cha suti yake (Hear say) Iweje Bendera yataifa ikanyagwe? Je kutakuwa na watu kuipenda nchi yao hapo? ZURIA la BUNGE litanduliwe mara moja!
   
 4. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Breaking news itumike ipasavyo???
   
 5. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Ndiyo kuashiria kuwa wanaikanyaga na nchi pamoja na wananchi wake. It's a shame.
   
 6. Komamanga

  Komamanga JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2009
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  huuu ni ujinga wa hali ya juu huku wenyewe bila kutambua wanajionea sawa tuuu
   
 7. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Nafikiri laana inaanzia hapo. Sijui ni mganga gani huyo aliwadanganya!
   
 8. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  tatizo viongozi wetu ni mbumbu ,wanafanya bendera ya nchi red carpet? kweli jamaa hawa ni hovyo hovyo mambo yao.
   
 9. G

  Gashle Senior Member

  #9
  Jun 30, 2009
  Joined: Mar 30, 2007
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Labda maoni haya yatolewe Mzee Sitta akiwa keshaachia, mbabe yule! Maskini yaliyomkuta Mzee Cheyo jana katika kupitisha bajeti ya wizara sijui ya ofisi ya Makamu wa Rais yanatia huruma. Nafikiri kuna haja ya jamaa kupeana semina elekezi na kuambiana kuwa heshima kitu cha bure. Kuwa upinzani sio kosa la jinai jamani, ni mtazamo tu! Tena mi ningependekeza wasiitwe Wapinzani (maana jina la negativity nyuma yake), labda waitwe Mbadala wa Serikali.
   
 10. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #10
  Jun 30, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hii nilisha itoa vilevile hata kwa michuzi sio bungeni bendera inakanyagwa hata viwanja vya ndenge wanapopokewa viongozi wa nchi mbalimbali hivi hata huyu Rais wetu ambae ni bingwa wa ziara labda anaweza kutuambia kati ya nchi ambazo amekua akizitembelea kuna nchi ambayo wakati akipokelewa katika viwanja vya ndege kwa zulia jekundu kunakishiwa kwa bendera ya taifa sadam Husein wakati wa vita na marekani katika hotel zote kubwa mlangoni aliweka mazulia yenye bendera ya marekani kupinga uvamizi huo.Naona kama viongozi wa CCM wanaona hivyo sawa basi waweke bendera ya CCM kwenye majamvi hayo Kama walilalamika tarime kwa bendera yao kuvalishwa mbwa na kukanyagwa inakuaje katika hili hawalioni?
   
 11. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2009
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  mbona ile sio bendera ni rangi tu za bendera nnaamanisha zimepambwa kwenye zulia

  na hata kwenye jezi za wachezaji wa taifa ni rangi haimaanishi mtu akiangusha fulana au kukanyaga amekanyaga bendera kwa ina rangi ya bendera

  la kama ni kuspeculate kisiasa na tuendeleeeeni
   
 12. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sasa wao wafanyaje na huku ndio kuwaganyaga kila mtanzania wa Taifa hili
   
 13. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mkuu Mwiba hujashtuka tu.
  Hawana haja na bendera, nina hakika wanapopita kuikanyaga hawafikirii wala hawahisi chochote zaidi ya akaunti zao na totoz zilizofurika huko dom kwa ajili yao.
  Wapo wale fanatics, ndo kabisa hawana habari nayo kwao wao wanajua bendera ya kweli ni ile ya Tanganyika na si hilo Tambara la kufunikia majeneza.
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Unaweza kusema ni rangi za bendera,ila mpangilio uliotumika unawakilisha bendera ya Tanzania na si vinginevyo ,kwa mfano ukiwauliza watoto wa shule waliowahi kutembelea mle ndani au hata mtazamaji wa luninga katika vipindi vya bunge ni wapi imetumika bendera ndani ya ule ukumbi wa Bunge ,watakueleza kuwa ni kwenye zulia la sakafu na huko kwenye jezi mtangazaji husema wamevaa jezi zenye strip ya bendera ya Tanzania na hatangazi jezi zenye rangi ya bendera ya Tanzania ,Mtu wa Pwani naona unafananisha jongoo na tandu.
   
 15. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Unanikumbusha watani wangu wa kusini mwa unguja walipokuwa wanabishawenywe kwa wenywe baadhi yao wakisema mavi ya mzungu yanuku bwanaaa!!!!! na wengine wakawa wanasema mavi ya mzungu hayanuku na kama yananuku yasege fanywa sahani kwa kuwa badhi yake walikuwa wanafikiria mika hiyo mavi ya mzungu ndio yaliyokuwa yananywa sahani na wewe hapa unasema eti zile ni rangi tu sasa unakumbuka Mr Sadam hussen alipoweka picha ya mzazi wale Bush katika sehemu ambayo kila mtu apitae huikanyaga na wamarekani walikasikika kwa kitendo kile naimani ungesema kuwa yule sio baba yake bush ni mchoro tu ule .
   
Loading...